Nafikiri kijana anayejenga katika usawa huu anatakiwa apewe heshima yake

Aisee ndio hivyo senior.

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Weee!! Mi nikiolewa naenda kuishi kwa mume hata km ana chumba kimoja, kwangu sifugi mtu.!!
Ila akinizingua nabeba bag langu narudi kwenye mansion yangu 🤣🤣🤣
Kumbe hujaolewa; jimbo lipo wazi na husemi!
 
Labda choo...ila nyumba yoyote hata iwe chumba kimoja...kwa dar andaa kuanzia mil50
Huu ndo ujinga mnodanganyana kisha mnazeekea kwenye nyumba za kupanga.

Kujenga ni kuamua tu ww mwenyewe ili mradi unafanya kazi inayokuingizia kipato.

Endeeni kudanganyana hivo, unaweza jenga kidogo kidogo hata miaka 5 kwa malengo ukiyojiwekea ni ww tu

Nina rafk yangu kipato chake ni kidogo tu hakizid laki 3 kwa mwez ila anajenga kidogo kidogo nyumba ya vyumba 3, chumba kimoja master, kuna sebule na sehem ya kulia chakula pia na choo kingine cha ndani.

Huu mwaka wa pili anajenga mdogo mdogo ameshapaua kaweka madirisha, saiv anajichanganya apige plasta.

Tena ni hapa hapa dar mbezi kwa msuguri kiwanja alinunua million 3 .

Sasa nyie endeleeni na akili zenu za kitoto hivo hivo
 
Mie nmekuelewa kwamba gharama za ujenzi zipo juu ni kweli unaweza kata tamaa ukaacha. Zamani nilikua nashangaa kuona maboma yameachwa mpaka tofali zmeanza kubadilika rangi kwa sasa naelewa.
 
Af majanki kibao skuiz wanajenga masta, uku daslam miji mipya watu wanajenga kwa kasi ya ajabu, kila nkitinga site nakuta mijengo mipya sio chin ya miwili imeinuka
 
Kujenga ni kuzika pesa ,tukutane kidimbwi tumwagilie moyo
Ukimaliza kumwagilia moyo unaamka asubuhi una hangover za kutosha huna hata mia, supu hata haiteremki na hela zote umekomba na bado kaunta una deni!

Kesho kutwa kodi inaisha, bili ya maji na umeme vinakuandama, ukicheki kwenye akaunti balance inasoma afu 19 tu!

Nyumbani mamako na babako wanakulilia shida, kupiga kizinga kwa wana unaona soo coz ndo kwaanza ni tarehe 2.

Ukicheki umri unakimbilia 35, huna nyumba, huna kiwanja, huna demu wa kueleweka, huna hata mtoto, wewe unapita na wahudumu wa bar tu coz ndo nyota yako ilipo! huna hata baiskeli!

Endelea kumwagilia moyo sisi Acha tuzike pesa.

Miaka 20 ijayo huna maisha, unaanza kutembelea historia, ooh mara enzi zangu nilikuwa hivi na vile kumbe ni janja janja ili uwapige vijana ukware, wakikunyima unaanza kuacha laana, laana zako zitampata nani wakati huo mtaani unaitwa mzee wa ovyo?
 
Mkuu hongera sana
 
Kiukweli wanawakatisha tamaa watu wenye nia thabiti ya kujenga. Sh. milioni 50 kwa Dar unajenga nyumba nzuri ya vyumba 3 iliyokamilika kila Idara. Labda fence ndio hutaimaliza kwa ujenzi huo. Wanaowatisha wenzao ambao ndio wanajitafuta kujenga waache hiyo tabia. Kwenye Jukwaa hili tupo katika kujifunza, kutiana moyo na kutafuta fursa.
 
Dah 🥴. Mm ninapata 500+ lakin raman Ina chumba na sebule, toilet na naifanyia mpango ipungue. Naona kama kwa kipato changu sitoboi.

Kumbe ni kuamua tu
Nb: kiwanja ninacho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…