Nafikiria kufanya maamuzi haya magumu japo naumia sana

Nafikiria kufanya maamuzi haya magumu japo naumia sana

Wakuu kiufupi nina mke na mtoto mmoja wa miezi 9 sasa. Tumekuwa tunaishi kwa kutegemeana kama mke na mme kwenye mambo mbalimbali. Nilibahatika vibaya kupoteza kazi baada ya kuwa mkataba wangu umeisha mwishoni kwa mwaka jana.

Tangu hapo mke wangu anaonyesha dharau waziwazi. Kiufupi ni dharau ambazo kiukweli chanzo chake ni kupungukiwa kipato japo nafanya bidii za biashara used naingiza pesa kiasi japo sio kama nilivokuwa napata salary. Mke wangu anabiashara yake nimemkuta nayo japo niliingiza pesa kama kutanua biashara iwe kubwa.

Cha kushangaza kafikia hatua hadi baadhi ya pesa nilizompa siku sio nyingi anakatalia ikabidi nimfate ofisini kwake ni chukue alivogoma nika force tukaharibu simu yake akaenda police kunichukulia RB kwamba nimemfanyia fujo japo hawakuja kunikamata na hii ni mara ya tatu kunishtaki kwa mambo ya kipuuzi mara zile mbili alinipeleka kwa mjumbe.

Sina amani na hataki tuachane mfano juzi nikamwambia ngoja nimwachie nyumba au nimtafutie room akae na mwanae mimi nikatafute pesa siku nikipata nitarudi amegoma na hapa tunapoishi kodi imeisha.

Sasa ninafikiria kumtoroka asijue nilikokwenda, najuwa hana hela ya kupanga chumba kwa sasa na hapa tulipo sasa nimesha mwambia mwenye nyumba naondoka. Yaani wakuu kuna madhira kibao hadi nafikiria na kuwaza mambo magumu sana.

Naandika lakini nahisi kama hamtanielewa maana ni mambo magumu sana. Sijawahi kumcheat mke wangu na sina demu mwingine lakini naishi nae ndani kama kaka na dada hata haitaji nimguse.

Ana kiburi kama chote jeuri imezidi hana hekima kabisa sometime hana aibu hata mbele za watu anaweza jibu hovyo tu.

NAMPENDA MWANANGU HIKO NDO KINANIUMA KUMUACHA LAKINI NAHISI NI KIFUNGO KIBAYA SANA KUENDELEA KUISHI NA HUYU MWANAMKE. NADHANI NIKIWA MBALI NAE ANAWEZA ONA UMUHIMU WANGU.

Nimechoka wakuu naomba mawazo uenu pia ikiwa utaguswakunishauri. Hatujafunga ndoa bado ni wachumba najulikana kwao na anajulikana kwetu.

Ahsanteni.
Nimeishia alipokushitaki polisi.Namaliza kwa kusema hauna mke una mzazi mwenziyo aliyekuwa anahitaji mtoto siyo mume katafute mke.
 
Pole Sana kwa yaliyokufika mkuu, lakini hapa tatizo linaonekana Ni la muda mrefu. Ukweli ulio uchi Ni kwamba huyu mwanamke hakupendi na hakuwahi kukupenda Bali alikuja kwako kwa ushawishi hasa wa uchumi wako.

Mimi Ni mwanamke nazijua tabia zetu vizuri mwanamke akimpenda mwanaume hatokua na uwezo wa kumjibu jeuri au kumdharilisha hata kwa bahati mbaya, atamheshim kwa pande zote hata akiishiwa majirani hawatojua.

Ondoka Ila mahitaji kwa mtoto hakikisha yanapatikana, usimpige maana mwanamke asiekupenda ukimpiga anaweza akakutafutia Jambo la kukuharibia muelekeo wa maisha kabisaaa. Ukipata pesa oa Moe mwingine mwenye akili timamu.
Ahsante sana aisee
 
Hapa una option 2,

1. Uendelee kua bwege ili usimpoteze mkeo

2. Utambue value yako, uchukue maamuzi ya
ya kiume uendelee na life lako.
There is always a message on how people treat
you, jiongeze uone mkeo anakupa message gani
Ukipata jibu uchague either uwe bwege or a
MAN
I catch you!!
 
Kwani ndugu mjumbe wewe umezaliwa na wa kigiriki?[emoji848][emoji848][emoji848]
Wanawake wa kibongo wanafanana na wanaume wa kibongo.
Haki vile mkuu tunafanana juu Hadi chini ndani na nje,wanawake na wanaume wa bongo mi a complete and full package
 
Wakizishika huwa wana viburi hatari, wanazitumia hukooo halafu wakiishiwa ndio wanajirudi eti tuwaheshimu!! Malipo ni here here[emoji1787][emoji1787]
Ahhh binadam sisi bhana michosho Sana na ulisema uendekeze mapenzi unaweza ukavaa chupi kichwani buree, Sasa Cha kufia Nini eee
 
Kusema nshapoa sio kweli ila acha niseme ahsante...maana nikicheki watoto wanavyoteseka I wish nisingemchunguza mke wangu au kureact baada ya kugundua ana ni cheat.
Mke kuchiti ni hatua mbaya sana yani inaboa kinyama maana hata ule upendo haupo tena unabakia na sonona tu.
 
Mke kuchiti ni hatua mbaya sana yani inaboa kinyama maana hata ule upendo haupo tena unabakia na sonona tu.
Ni kweli ndo maana nikaamua maamuzi magumu ya kumpiga chini sema sasa watoto ndo wananipa Sonoma nyingine inabaki kusema ni agheri nisingeoa maana hawa wanawake ni vichomi balaa
 
Ichi kiburo chenu baadae kitawatesa saaana
Mkuu Wala usinielewe vibaya Yani wakati mwingine huwa tunakua viburi kutokana na historia,na ili kuuepusha moyo na maumivu na Ile historia isijirudie unaamua kuwa na heshim tu ili maisha yaendelee bas na Wala sio kiburi
 
Back
Top Bottom