Habari wana JF,
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, mimi ni mhitimu wa chuo kikuu ngazi ya shahada (degree) kati ya chuo kimoja hapa nchini. Kuna mradi/biashara moja nataka kuanzisha ila nakwama kwenye mtaji (Ambao kwa makadirio sio chini ya Milioni Moja).
Nimewaza sana na kuwazua, suluhisho nilopata ni kukopa,tatizo linakuja kwenye kuweka dhamana. Sina cha maana chochote kinachofikia thamani ya huo mkopo naotaka kuchukua. Nimepata wazo la kuweka dhamana vyeti vyangu vya taaluma (o level,advance mpaka chuo) ili niweze kujikwamua na hili janga la ukosefu wa ajira na kuweza kujiajiri mwenyewe. Nina uhakika wa hii biashara kutiki asilimia 90 hivyo sibahatishi katika ilo.
Nina maswali kadhaa yana rindima kichwani mwangu, nayo kama yafuatavyo;
1. Ni nani mtu sahihi wa kunikopesha na kuvitunza vyeti vyangu mpaka pale nitapomaliza mkopo (bila kutapeliwa vyeti vyangu)?
2. Ni nani wa kumface na kunikubalia kunipa huo mkopo kwa dhamana ya vyeti vyangu?
3. Kuna taasisi au benki yenye kukopesha kwa dhamana ya vyeti vya mhusika?
NB: Nipo tayari kuandikishiana mbele ya mashahidi na mwanasheria. Pia nipo tayari kukopeshwa kwa riba hisiyozid 40%.
Nakaribisha ushauri na maoni yenu au msaada wa nini cha kufanya kutimiza lengo hili husika.