Mkuu nimekucheck pm ila naona kimyaMkuu ulivyojielezea nimekumbuka maisha yangu enzi za saidia fundi kule Iringa na Njombe daah hadi nimetamani nikupe tu hiyo hela ukipata utarudisha, ukikosa kurudisha basi utakuwa umesogeza gurudumu la maisha mbele na huenda ukaja kusaidia kizazi changu mbeleni au ukaja kuifanya dunia iwe mahali salama pa kuishi, tuwasiliane!
Ninakuzingatia mkuuMkuu nimekucheck pm ila naona kimya
Sawa mkuuUsichezee riba Mkuu, hela ya riba inaenda haraka kama uyoga, kwa biashara changa sikushauri uchukue mkopo wenye riba, Nenda kwa watu binafsi wakukopeshe bidhaa/pesa ukifanya huduma uzirudishe.
Unaweza kupata hiyo hela na riba ikawa asilimia arobaini, kumbuka biashara hiyo ni changa.
Habari wana JF,
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, mimi ni mhitimu wa chuo kikuu ngazi ya shahada (degree) kati ya chuo kimoja hapa nchini. Kuna mradi/biashara moja nataka kuanzisha ila nakwama kwenye mtaji (Ambao kwa makadirio sio chini ya Milioni Moja).
Nimewaza sana na kuwazua, suluhisho nilopata ni kukopa,tatizo linakuja kwenye kuweka dhamana. Sina cha maana chochote kinachofikia thamani ya huo mkopo naotaka kuchukua. Nimepata wazo la kuweka dhamana vyeti vyangu vya taaluma (o level,advance mpaka chuo) ili niweze kujikwamua na hili janga la ukosefu wa ajira na kuweza kujiajiri mwenyewe. Nina uhakika wa hii biashara kutiki asilimia 90 hivyo sibahatishi katika ilo.
Nina maswali kadhaa yana rindima kichwani mwangu, nayo kama yafuatavyo;
1. Ni nani mtu sahihi wa kunikopesha na kuvitunza vyeti vyangu mpaka pale nitapomaliza mkopo (bila kutapeliwa vyeti vyangu)?
2. Ni nani wa kumface na kunikubalia kunipa huo mkopo kwa dhamana ya vyeti vyangu?
3. Kuna taasisi au benki yenye kukopesha kwa dhamana ya vyeti vya mhusika?
NB: Nipo tayari kuandikishiana mbele ya mashahidi na mwanasheria. Pia nipo tayari kukopeshwa kwa riba hisiyozid 40%.
Nakaribisha ushauri na maoni yenu au msaada wa nini cha kufanya kutimiza lengo hili husika.
😅😅😅😅😅😅😅😅 Umenichekesha sana mdogo wangu.Sidhan kama ni rahis kuvitelekeza vyeti kwa mkopo wa Milioni moja. Nashukuru kwa mchango wako mkuu
Shukran sana mkuu kwa kuntia moyo,huwa nazidi kumuomba sana MunguHii hali ilinikuta mwaka 2017 nilipo acha chuo NIT , nika ja mtaani. Maisha ya mtaa bado kidogo yanichanganye akili. Nashukuru MUNGU , akanitoa kwenye stress hizi. Mi ushauri wangu nimpe bro , Asisahau kusali
Nino vyeti, mimi wamenitelekezea kadi za magari na hati za nyumba.Anadhan ni kazi rahis kuvitelekeza vyeti uyu[emoji28][emoji28]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Nino vyeti, mimi wamenitelekezea kadi za magari na hati za nyumba.
Hapa siku nitageuka kuwa trafic na kukamata magari.
Mimi kuna Jamaa kanichia hati ya nyumba mwaka unaenda wa tatu sasa, kila nikimtafuta anabadili namba na nikimpata ni sound tu.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Biashara hii nzuri ila changamoto ndio kama hizi sasa