Nafikiria kwenda Msumbiji, Malawi au Zambia kufanya biashara. Naomba msaada wa mawazo

Nafikiria kwenda Msumbiji, Malawi au Zambia kufanya biashara. Naomba msaada wa mawazo

Unjubinunuk

Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
10
Reaction score
22
Habari zenu tena wadau.. nafikiria kwenda katika nchi za jirani hapa kama Msumbiji, Malawi au Zambia. Yoyote mwenye uzoefu wa namna ya kufanya biashara katika nchi hizi anisaidie na connection hizo.

Mtaji wangu ni mdogo lakini inavyoonekana kwa hizo nchi naweza kufanya jambo likaenda, naomba mwenye uzoefu anisaidie.
 
Nenda malawi huenda utapata wazo la kusaidia kupambana na kimbunga fredy
 
Huko unachoma mafuta yako tu bure mkuu.

Bora ukae bongo utafute pesa, msumbiji machafuko yapo sana....malawi na zambia ni pakawaida tu labda uchukue vitu kama nguo, viatu pale kariakoo upeleke malawi na zambia wengi wanapiga pesa huu upande.

Kuna jamaa angu naye alirudi nyumbani alikuwa zambia anauza maji haya ya kunywa jumla na rejareja saivi ni machinga mkoani hana maisha tena ila alikuwa kabadilika ngozi kwa kunawiri alivokuwa zambia yaani pengine viuno na mengine vilimchanganya maana alienda zambia hana mtaji akakodi mkokoteni akaanza mtaani kibishi ndiyo akafungua ofisi kubwa. Yeye aliniambia corona ndiyo ilimkimbiza zambia ila alikuwa anamenya fresh na kwa sasa hawezi rudi tena bora atulie Tanzania tu.

Malawi kuna kamji kama blantre kapo vizuri kibiashara vingenevyo hizo nchi wanaloga kama wanyakyusa wa mbeya na wakinga.

Mwisho sikushauri uende msumbiji japo wanasema pesa ipo ila ni risk kukaa huko. Kuna ndugu zangu wachagga wametelekeza mali zao huko msumbiji na wengine wamefilisikia huko.

Pesa popote wewe pambana kikubwa amani kaka, wapo ndugu zangu wengine wapo mpaka congo wanapiga pesa sana sema daah wale huwa sina mawasiliano nao sababu wanajisikia sana wanakujaga moshi mwezi wa 12 mwisho wa mwaka na fujo zao za kingese kuwa wana range sijui mercedes.

Mimi mtu akijisikia nami huwa najisikia maana sili kwake. Sema nao wanaconnection na biashara zao nyingine kariakoo nilivosikia, way back waliniambia twenzetu congo tukakufungulie goli la mzigo wa nikawatemea cheche nyingi 😄😄
 
Huko unachoma mafuta yako tu bure mkuu.
Bora ukae bongo utafute pesa, msumbiji machafuko yapo sana....malawi na zambia ni pakawaida tu labda uchukue vitu kama nguo, viatu pale kariakoo upeleke malawi na zambia wengi wanapiga pesa huu upande...

Asante mkuu.. umeelezea vyema. Kuna points muhimu nimenukuu asante sana
 
Na mtoa hoja ebu jitahidi kuonyesha utofauti kidogo na middle class wetu, elezea kwanza wewe mwenyewe interest zako za kibiashara zipo wapi, nini ndoto zako?

Ukiweka hapa then bila shaka utapata mawazo zaidi, mfano labda unafikiria kuanzia na nguo, kununua hapa na kupeleka mazabuka definitely kuna watanzania wanafanya hivyo ni rahisi kukupa the way forward, but sasa inaonekana unataka kutafuniwa kila kitu
 
Msumbiji unaweza kuliwa nyama kama mbuzi,usiende huko komaa bongo
 
Msumbiji unaweza kuliwa nyama kama mbuzi,usiende huko komaa bongo
Ila wenye fedha pale Maputo ni wapopo na Wabongo!,tuache kuwa selfish na kukatishana tamaa, maisha popote duniani, bongo kama hauna chain ni shida, bora kwenda kujilipua Tete
 
Na mtoa hoja ebu jitahidi kuonyesha utofauti kidogo na middle class wetu, elezea kwanza wewe mwenyewe interest zako za kibiashara zipo wapi, nini ndoto zako?,ukiweka hapa then bila shaka utapata mawazo zaidi, mfano labda unafikiria kuanzia na nguo, kununua hapa na kupeleka mazabuka definitely kuna watanzania wanafanya hivyo ni rahisi kukupa the way forward, but sasa inaonekana unataka kutafuniwa kila kitu

Biashara ya nguo na / au viatu ndio nataka nifanye huko..
 
Biashara ya nguo na / au viatu ndio nataka nifanye huko..
Yes mkuu sio biashara mbaya ila unahitajika kuwa very displine, changanya nguo na viatu hasa vya kike na watoto, Zambia ni safi ila usianzie miji mikubwa, jaribu miji njia ya Kaffe hadi kazungura border au Kuja mpaka wa Angola na Zambia, good luck
 
Daaah yani ww mwenyewe mtaji wako siri. Je na wao wakifanya siri dili za uko?
 
Nina uzoefu za zambia. nenda kafanye biashara kule,komaaa sema changamoto ni uzembe wa ubalozi wa Tanzania nchini zambia kushindwa kuelewana na mamlaka za zambia ili kushusha bei ya vitambulisho vya wafanyabiashara wa kitanzania nchini humu (COMESA BUSINESS PERMITS). 5000 kwacha is too expensive and for only 3 months.

Naomba ukichagua zambia upite City market chukua daladala ya kwenda MUMBWA NANGOMA, ushukie Round house bar & guest house kuna mbususu za hatar apo zenye asili ya Mongu na Angola

nawasilisha
 
Asante mkuu
 
Biashara gani inalipa huko?

Back
Top Bottom