Nafsi inapoghadhibika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
NAFSI INAPOGHADHIBIKA

Kuna mtu alisema maneno yasiyopendeza miaka miwili iliyopita siku kama ya leo ikabidi nimjibu lakini nilikuwa nimeghadhibika:

"Jack kadri utakavyojua na kujua huwezi ukaifahamu historia ya African Association kama alivyoijua Kleist Sykes na wanae au walivyoijua wajukuu zake Daisy Abdul Sykes na mdogo wake Kleist Abdul Sykes...au nilivyoijua mimi kufikia kuisahihisha historia iloyoandikwa na Chuo cha Kivukoni mwaka wa 1981 au kufikia mimi kuwa mmoja wa waandishi 500 kutoka kila pembe ya dunia walioandika Dictionary of African Biography (DAB), mradi wa Harvard na Oxford University Press, New York (2011).

Hizi ni volume sita.

Huwezi kuijua historia ya Tanganyika kwa kiasi cha kufanya mhadhara wa somo hilo kama nilivyofanya vyuo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania pamoja na Northwestern University, Evanston, Chicago chuo kinachoongoza duniani katika African History...bado hujafanyiwa review ya kazi yako yoyote katika Cambridge Journal of African History...kote huko nimepita "in flesh and blood."

Leo kwa taarifa yako limeundwa jopo likiongozwa na Prof. Shivji linaandika historia ya Mwalimu Nyerere na nimefanyanao mahojiano nyumbani kwangu mara mbili na nimewapa nyaraka na picha.

Wao wameamua kufanya hilo katika kuiweka sawa historia ya uhuru wa Tanganyika na kitabu cha Abdul Sykes ndicho chanzo.

Sidhani kama wewe una lolote la kumstaajabisha yeyote.

Lakini eleza unachojua tutakusikiliza.

Nimetaabika kusema haya lakini imebidi ili tufahamiane vizuri.

Baada ya haya nadhani umeelewa kuwa Mohamed Said si mtu chembelecho, wa ''kulisha watu matango pori.''

Picha ya kwanza kulia: Nakala tofauti za matoleo ya kitabu cha Abdul Sykes, Northwestern University, Chicago, kulia Prof. Shivji, Prof. Saida Othman, na Dr, Ngw'aza Kamata na picha ya mwisho siku watoto wa Abdul Sykes waliponialika kunionyesha Medali ya Mwenge wa Uhuru aliyotunikiwa baba yao mwaka 2011 kwa nchi kutambua mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ally Sykes pia alitunukiwa medali hii kwenye sherehe ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.

 
Sina shaka na uwezo wako uliotukuka juu ya historia ya mwambao huu wa kiswahili, mambo yake, matukio na watu wake hasa jiji letu la "mzizima", Mungu azidi kukuweka mzee wetu wa kariakoo. Mohamed Said

Let's meet at the top, cheers 🥂
 
Unajitaabisha sana kujielezea! Binafsi naamini watu wengi hawatilii shaka usomi na ujuvi wako wa historia na namna ulivyoamua kujibidisha katika kuijua

Watu wengi nikiwemo Mimi tunakupuuza kwa kutaka kutumia elimu na ujuvi wako kupandikiza mbegu na kukoleza mbolea ya ubaguzi hasa wa dini

Unatumia nguvu na juhudi kubwa kutaka kukoleza chuki hasa hasa waislamu wawachukie wakristo kwamba waone wao wanahaki kubwa na uhuru wa Tanganyika kuliko Wakristo

Nikutaarifu tu kwamba, wewe utakufa na maandishi yako yatabaki lakini dhamira yako haitakaa itimie na nafsi yako itaendelee kuogelea kwenye ziwa la moto na kupata adhabu ya kaburi maana unachokitaka hakitatokea!

Kwanini hakitatokea?

Hao wazee wetu waliopigania Uhuru pamoja na Mwl Nyerere, hawakufanya hivyo kwa kusukumwa na dini! Hawakufanya hivyo kwa kusukumwa na ubaguzi!

Nchi zote walizotaka kumng'oa mkoloni kwa kutaka kuendekeza unachokijadili kwa miaka yako yote tangu ufundishwe namna ya kuandika, waliuana wao kwa wao kwanza na akili zilipowakaa sawa ndipo Uhuru ukapatikana. Na hadi leo hizo chuki na visasi bado wanavyo

Tunafahamu huyafanyi haya kwa matakwa yako peke yako, unayoyafanya ni mkakati wa kundi fulani la kipuuzi ambalo mnajiaminisha mnahaki kuliko watu wengine

Unafanya mihadhara vyuo vikuu, unafanyiwa rejea, unasomwa dunia kote, lakini tambua watu wana akili za kuchuja! Hawamezi vyote Kama vilivyo na ndiomaana unaishia kutoa takwimu ya mihadhara na rejea ulizofanyiwa lakini ki uhalisia moyo wako hauna furaha maana matarajio yako ya Waislamu kuwachukia wakristo hayajafanikiwa!

Tunaoana Kama kawaida, tunashirikiana Kama kawaida, tunapata mafasi mbalimbali serikalini na kwenye mashirika mengine kwa kuangalia vigezo vya uwezo na elimu si kigezo cha dini!

Bahati nzuri vijana wa leo wana uwezo mkubwa wa kuchuja mambo wanayolishwa na wazee wenye roho mbaya na roho ya visasi Kama wewe!

Kutwa kucha unahusianisha harakati za ukombozi na dini kana kwamba wazee wetu walikuwa wanaeneza dini!

Utakufa na kihoro na kwa msomi na mtu mwerevu Kama wewe hafai kuendelea kuhubiri na kuhamasisha chuki miaongoni mwa watu

Najua utakimbilia kusema nilete ushahidi wa ubaguzi unaoufanya, lakini hata nafsi yako mwenyewe ukiwa mwenyewe chumbani jaribu kuisikiliza ni ushahidi tosha wa chuki iliyokujaa.

Nimalizie kwa kusema, wanaokusoma na kukusikiliza wanapata kufahamu vitu vingi sana, lakini wanapuuza vitu vingi na kukerwa hasa pale unapohusianisha dini na kupigania Uhuru!

Waliopigania Uhuru wao wenyewe huko waliko wanakushangaa maana hawakusukumwa na hicho unachotaka kutuaminisha. Walisukumwa na ujasiri, uzalendo na matakwa ya kutaka kujitawala!

Wanafahamu kabisa hata hizo dini zenyewe zilikuwa sehemu ya ukoloni na bado ni sehemu ya ukoloni hadi leo! Dini ni utamaduni tu Kama zilivyotamaduni zingine

Hao wazee wako unaotaka kutuaminisha walisukumwa na dini, Kama mwarabu asingeanzia kueneza dini ukanda wa pwani na watu wa pwani wakawa tayari kuipokea, wangeweza kupigania Uhuru wakiwa wanaamini katika imani zao walizokuwa nazo hata kabla ya mwarabu kuja!

Wangeweza kufanya hivyo kwasababu walisukumwa na nafsi na uzalendo wao wala si dini yao!

Unaporudia rudia neno "Waislamu" kwenye maandishi yako huwatendei haki wazee wako hao waliojitoa pasipokusukumwa na uislamu unaotaka tuamini bali walisukumwa na uzalendo na ujasiri uliokuwa ndani yao

Mwarabu anasifika kwa kutumia huo uislamu wake kueneza biashara haramu ya utumwa! Biashara iliyotweza utu wa mtanganyika! Kama unaona ni sifa andika sasa uhusianishe biashara ya utumwa na uislamu!

Wewe ni mtu na heshima zako, unazodolewa na watoto wadogo kisa kutaka kueneza chuki ambazo bila shaka hakuna atakayefaidika nazo
 
Kingjr2, Hivi utumwa ulimfaidisha nani hasa? Hivi msomi wa mision aliyepata kazi nzuri na mshahara mnono alikuwa na haja gani ya kuukata mkono uliomlisha?

Hao waliingia kwenye harakati baada ya kusoma alama za nyakati kwamba uburu umekaribia nao wana fursa ya kutwaa uongozi baada ya Uhuru.
 
King...
Kujitaabisha ni kupata tabu na kudhikika.

Mimi nafarajika na historia hii ya wazee wangu na nisingeiandika ila nilipotambua kuwa ilifutwa kwa makusudi.

Walioifuta walisukumwa na hofu hii uliyonayo wewe hii leo.

Hii ni historia kama zilivyo historia zote duniani ambazo zinafundishwa kama mlango katika milango mingi ya elimu.
 
Inawezekana una point lakini unarudiarudia hayo hayo hadi unatia uvivu kusoma
 
Inawezekana una point lakini unarudiarudia hayo hayo hadi unatia uvivu kusoma
Nguvu darsa la mtandaoni si sawa na darsa unaloliona kwa macho ukatambua kuwa hawa jana walinisikiliza kwa hiyo nitaendelea nilipokomea jana.

Kwenye mtandao unazungumza na watu wapya kila dakika.

Kuna waliokuwapo toka mwanzo wa darsa na kuna wengine darsa wamelikuta liko katikati.

Ikiwa wewe upo toka mwanzo na darsa lile ushalisikia huna sababu ya kujichosha una delete au unapita wima unasoma mambo mapya.

Mtandaoni mwalimu hawezi kusema hili nilishalieleza hivyo atalieleza upya au ataweka link mtu aingie na kusoma.

Huna sababu ya kuteseka katika mtandao unaweza ku-delete, kupita wima hufungui hata ku-block kuondoa bughdha.

Naamini umeelewa.
 
Alwyz,
Amin kwa sote.

Kila taifa lina historia na mapito yake. Msomi yeyote „classical“ hufanya jitihada kuwafanya Vijana wa Leo wakumbuke kuwa vinavyoelea vimeundwa, Lakini nia yenyewe sio kuleta chuki Bali kuhakikisha those positive na points zinazojenga zinawafanya Vijana wa Taifa la Leo na kesho Wawe Bora na wamoja zaidi. Zingatia Hilo.
 


Barua ndeefu utafikiri ya mahaba mkuu. Huyu mzee wetu tunampenda na kumheshimu sana. Wewe kama hupendezewinae kaa pembeni.

Waarabu tunawapenda mzee, ni watu wema kuliko jamii yoyote ile upo hapo, ni ndugu zetu haswaa "Almuslim akhuh Muslim" na ndio waliosambaza uislamu huku east afrika n.k, kama ni utumwa hao ndugu zako wa western ndio walitesa na kuwafunga minyororo mababu na kuwapeleka utumwani kuwatumikisha kwenye mashamba yao na ndio maana watu weusi wamejaa tele huko amerika, brazil n.k.


Usiku mwema!
 
unprojud...
Unadhani kwangu mimi kusahihisha historia ya TANU ni kujenga chuki?

Umekisoma kitabu changu?

Ikiwa bado kisome.
 
Hakuna aliyekukataza kumpenda umpendaye na hakuna aliyekwambia unayempenda wewe lazima apendwe na kila mtu

Kila jamii inao uzuri na ubaya wake isipokuwa Mungu pekee aliye sirini

Hata hivyo, kuendelea kuendelea kuelewesha mtu anayeamini kujilipua, kuua, kujitoa muhanga na kuchukia jamii nyingine iliyoumbwa na Mungu Kama njia ya kuifikia pepo ni ukichaa tu!

Hakika mtaendelea kutawaliwa hivyo hivyo hadi hapo kitakapokuja kizazi kwenu kitakachopata akili na kung'amua kuwa nyie mlirithi upuuzi mkaumeza kama ulivyo na mkauendeleze upuuzi pasipo kuchanganya na akili zenu mlizojaaliwa na Mungu!

Huyu mzee yeye anajifurahisha kusema anafurahi kwamba ameandika historia ya babu zake, lakini ukweli ni kwamba anahangaika kwanini Babu zake hao hawakuwekwa madarakani baada ya uhuru!

Hilo litaendelea kuwatesa hadi akili itakapowakaa sawa na kujua dini ni dini na serikali ni serikali.
 
Sio kweli kwamba unafarijika! Hapo unajifariji tu! Ukweli ni kwamba unaumia na kunung'unika kwanini hawakushika madaraka baada ya Uhuru! Hili liko wazi kwenye maandishi yako mengi

Ukweli ni kwamba tamaa yako ni kuona nchi hii inakuwa ya kiislam kitu ambacho hakitakaa kitokee

Mtu mwerevu Kama wewe tusingetegemea kuona anaeneza chuki ya kidini kwa kizazi na kizazi

Maandiko yako mengi unayaandika kana kwamba waliokuwa wanapigania Uhuru walikuwa wanapigania kueneza dini Kama walivyofanya waarabu na wazungu walipokuja Afrika.

Kumbe kinyume chake hao Babu zako walishiriki kupigania Uhuru kujikomboa toka mikononi mwa wakoloni na si kutoka mikononi mwa dini fulani na kusimika dini nyingine

Harakati zilikuwa kuung'oa ukoloni na kujitawala wenyewe
 
Kingjr...
Kutokana unavyoandika ni wazi hujakisoma kitabu cha Abdul Sykes.

Hapana suala si kuwa wazee wangu hawakushika madaraka.

Kilichonigusa mimi ni kule kuona historia ya TANU iliyoandikwa haina ukweli.

Haiwezekani ikaandikwa historia ya TANU Abdul Sykes asitajwe kukupa mfano mmoja.

Hili ndilo lililowazi katika maandishi yangu.
 
King...
Muhimu kwangu ni kuwa historia iliyokosewa nimeisahihisha.

Ukipenda kuamini kuwa historia iloyoandikwa na Kivukoni ndiyo historia ya kweli ya TANU mimi sina tatizo na hilo.

Wewe ni mtu huru na una haki ya kuamini utakacho.
 

Asingekuwa anatumia kivuli cha udini kuelezea historia angekuwa mwanahistoria mzuri sana,shida yake ameshindwa kutenganisha hicho kitu na ndicho kitu kinachofanya wengi tupuuze maandiko yake kwa kuwa tunafikiri ana lengo lake ovu nyuma ya pazia na nchi yetu tukufu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…