Nafsi inapoghadhibika

Nafsi inapoghadhibika

Sectarian thinking is no virtue at all! Marehemu Baba yangu alikuwa muislam safi, na alipigania uhuru bega kwa bega na wazee wengine kama Mwl Nyerere, Mzee Sykes etc.

Lakini daima nitataja ushiriki wake katika kupigania uhuru wa Tanzania kwa misingi ya uzalendo, usawa, haki, na kamwe sitatumia feelings za uislamu wake kuelezea ushiriki wake kwenye independence movement[emoji120]
 
Asingekuwa anatumia kivuli cha udini kuelezea historia angekuwa mwanahistoria mzuri sana,shida yake ameshindwa kutenganisha hicho kitu na ndicho kitu kinachofanya wengi tupuuze maandiko yake kwa kuwa tunafikiri ana lengo lake ovu nyuma ya pazia na nchi yetu tukufu
Steveache,
Hakuna udini katika historia hii ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Kitabu kimefanyiwa mapitio na mabingwa wa African History hakuna aliyesema nimeandika kitabu cha dini.

Library of Congress wamekikatalogi hawakukiweka kitabu upande wa dini.

Kunipuuza si kitu chepesi.

Ungepuuza usingekuja hapa kunijibu ungepita wima.

Kitabu hiki kinakwenda toleo la nne Kiingereza na Kiswahili na kiko katika Cambridge Journal of African History nk. nk.

Si kama napiga zumari langu mwenyewe ila nakufahamisha kuhusu historia hii unayodhani kuwa imepuuzwa.

Hiki ndicho kitabu kilichofanya uandikwe wasifu wa Julius Nyerere ili kutafuta ukweli wa historia ya TANU.

Watafiti na waandishi Waandishi wa Wasifu wa Julius Nyerere walikuja nyumbani kwangu mara mbili kunihoji kuhusu maisha ya Mwalimu Nyerere na Abdul Sykes wakati wa kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hicho wewe unachokiita "kivuli," ndicho kilichafanya kitabu changu kije na taarifa mbazo hakuna aliyekuwa anajua zipo.

Yapo mengi lakini tosheka na haya kwa sasa.
Mimi si mtu wa kupuuzwa.
 
Sectarian thinking is no virtue at all! Marehemu Baba yangu alikuwa muislam safi, na alipigania uhuru bega kwa bega na wazee wengine kama Mwl Nyerere, Mzee Sykes etc. Lakini daima nitataja ushiriki wake katika kupigania uhuru wa Tanzania kwa misingi ya uzalendo, usawa, haki, na kamwe sitatumia feelings za uislamu wake kuelezea ushiriki wake kwenye independence movement[emoji120]
Hardwood,
Hakuna aliyefanya hivyo.

Tatizo ni kuwa kuna hofu ya Uislam basi kuwa majina moja baada ya jingine na mazingira ya dua na visomo ndilo tatizo lao.

Wangependa yasielezwe haya katika historia hii.
 
Raia Mwema Jumatano 3 March, 2019

Mwaka wa 1950 uongozi wa TAA ulikuwa chini ya Dr. Vedasto Kyaruzi kama Rais na Abdulwahid Sykes akiwa Katibu na ikaundwa TAA Political Subcommittee (Kamati ya Siasa ya TAA) iliyokuwa na pamoja na Rais na Katibu, wajumbe hawa wafuatao: Sheikh Hassan bin Ameir aliyekuwa Mufti wa Tanganyika, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Steven Mhando na John Rupia.

Katika kipindi hiki cha mwaka wa 1950 Abdul Sykes alikuwa katika majadiliano na Chief David Kidaha Makwaia akimtaka aingie TAA wamchague kuwa rais kisha waunde TANU yeye akiwa rais wadai uhuru wa Tanganyika.

Kwa kuwa hapa tunazungumza nafasi ya dini katika historia ya uhuru wa Tanganyika napenda kueleza kuwa Chief David Kidaha Makwaia hakuwa Muislam ingawa alikuwa mtoto wa Chief Makwaia Mohamed Mwandu.

Wakati huu Abdul Sykes alikuwa mmoja wa viongozi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) lakini hili halikuingia katika fikra zake katika kumtaka Chief Kidaha Makwaia kuongoza harakati za kudai uhuru wa Tanganyika na uhuru ukipatikana awe Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika.

Juhudi hizi hazikufanikiwa.

Mwaka wa 1951 Waingereza walimpa uhamisho Dr. Kyaruzi na kumpeleka Jela ya Kingolwira, Morogoro kisha wakamuhamishia Nzega.

Hamza Mwapachu yeye akahamishiwa Nansio, Ukerewe na yote hii nia ya Waingereza ilikuwa kuivunja nguvu TAA Makao Makuu, New Street kudhoofisha juhudi za kuunda chama cha siasa.

Mwaka wa 1952 Mwalimu Julius Nyerere alipelekwa kwa Abdul Sykes na Joseph Kasella Bantu.

Wakati huu Abdul Sykes alikuwa Kaimu Rais wa TAA na Katibu.
 
Mkutano wa TANU Mnazi Mmoja 1950s

Inategemea watu watakavyoitumia dini.

Dini inaweza kutumika kuwaunganisha watu na pia inaweza kutumika kuwagawa.

Mikutano ya mwanzo ya TANU pale Mnazi Mmoja ilifunguliwa kwa dua na watu wakisoma Surat Fatha na kutikia dua hiyo kwa pamoja.

Aliyekuwa akiongoza dua hii alikuwa Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.

Leo ni tabu sana kwa mtu kuamini kuwa hali ilikuwa hivi kuwa hata mikutano ya ndani ya TANU pale New Street ilikuwa ikifunguliwa na kufungwa kwa dua na Nyerere akiwapo.

Mwalimu Nyerere katika hotuba yake maarufu kwa Wazee wa Dar es Salaam Ukumbi wa Diamond wakati wa kustaafu urais mwaka wa 1985 alieleza kuhusu dua aliyofanyiwa na akashiriki nyumbani kwa Mzee Jumbe Tambaza.

Hotuba hii imekuwa maarufu sana khasa kipande hiki anachoeleza jinsi yeye Mkristo alivyopokelewa na Waislam wa Dar es Salaam akiwa na vijana wenzake Abdul Sykes na Dossa Aziz.

Hawa vijana wawili Abdul Sykes na Dossa Aziz, marafiki wa Baba wa Taifa ndiyo waliompeleka Mwalimu Nyerere kwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir kumtambulisha na kutaka msaada wake akubalike kwa Waislam na kuanzia siku ile Sheikh Hassan bin Ameir na Nyerere walikuwa wazalendo wawili wakisaidiana katika kudai uhuru wa Tanganyika Sheikh Hassan akiuza kadi za TANU ndani ya misikiti ya Dar es Salaam alikokuwa akidarsisha.

Turejee kwenye visomo na dua wakati wa kudai uhuru.

Lilikuwa jambo la kawaida sana wakati ule kwa Waislam waliokuwa katika mapambano na ukoloni kutanguliza mambo yao yote kutaka msaada wa Allah.

Hili lilikuwa jambo lililokuwa linakuja hata bila ya kufikiri.

Mwaka wa 1949 kabla ya mgomo wa makuli wa Bandari ya Dar es Salaam, walifanya kisomo na dua kubwa na baada ya hapo ndipo walipoingia barabarani kwa maandamano kama ishara ya kuanza mgomo.

Abdul Sykes alihusika sana katika mgomo huu.

Mwalimu Nyerere kwa hiyo hakuwa kiongozi wa kwanza katika harakati kufanyiwa kisomo na Waislam.

Mwalimu Nyerere yeye haya hakuyajua kwani alizikuta harakati katikati.

Abdul Sykes alikuwa Market Master Kariakoo Market nafasi kubwa sana wakati wa ukoloni na yenye wasaa na fursa za kutosha.

TANU ilipoanza Abdul Sykes akawa anauza kadi za TANU pale sokoni na Nyerere alikuwa hapungui ofisini kwake.

Special Branch wakiwafuatilia na siku moja Abdul Sykes akavamiwa na mkubwa wake Mzungu, Town Clerk ambae soko lilikuwa chini yake.

Abdul na huyu Mzungu walipambana kwa maneno makali Abdul akidai kuwa TANU kilikuwa chama halali na si kosa kuwa na kadi zake.

Hofu iliyotanda pale sokoni ilikuwa Abdul atafukuzwa kazi.

Abdul wakati ule Abdul alikuwa kijana wa miaka 30.

Wazee wafanyabiashara pale sokoni akina Sharif Mbaya Mtu, Mshume Kiyate, Shariff Abdallah Attas, huyu alikuwa mfanyakazi wa soko, mkusanyaji ushuru wa nafaka pale sokoni walijikusanya na pakafanyika dua kubwa ya kisomo na wakachinja mnyama.

Hii ilikuwa ndiyo dua ya kwanza kwa TANU kufanya kisha zikafuata dua aliyofanyiwa Rashid Ali Meli na ile ya Nyerere.

Rashid Ali Meli yeye alikuwa mweka fedha wa Dar es Salaam Municipal Council.

Rashid Ali Meli alifungua safe yake ofisini akatoa fedha kuikopesha TANU akamkabidhi Iddi Faiz Mafungo aliyekuwa Mweka Hazina wa TANU ili aziingize katika mfuko wa safari ya Nyerere UNO.

Siku ya pili wakaguzi wakaja ofisini kwake kufanya ukaguzi bahati nzuri hawakuanza na kukagua fedha taslimu.

Ilikuwa wazi kuwa endapo wakaguzi watagundua kuwa kuna upungufu wa fedha Rashid Ali Meli atashtakiwa kwa wizi na atafungwa.

Taarifa hizi ziliipofika ofisi ya TANU kitu cha kwanza kabisa ikawa pafanywe dua.

Baada ya kisomo hiki cha Rashid Ali Meli kikafuatia kisomo cha Lindi alichofanyiwa Baba wa Taifa na Sheikh Mohamed Yusuf Badi mwaka wa 1956 kisha ikafuatia dua ya Mnyanjani, Tanga kabla ya kwenda Tabora kwenye mkutano wa Kura Tatu uliotishia kuigawa TANU katika mapande mawili.

Picha hizo hapo chini ni Mkutano wa TANU Mnazi Mmoja miaka ya mwanzo ya TANU, picha ya pili ni kushoto Sheikh Suleiman Takadir, John Rupia naJulius Nyerere. Picha ya tatu ni Soko la Kariakoo kama lilivyokuwa katika miaka ya 1950 na picha ya nne ni Shariff Abdallah Atttas. Picha ya mwisho kulia ni Lawi Sijaona, Abdul Sykes, Julius Nyerere na Dossa Aziz katika hafla Ukumbi wa Arnatouglo kumuaga Nyerere safari ya pili UNO 1957.

Namaliza kwa kusema kuwa hivi ndivyo Waislam walivyoitumia dini yao katika kuleta umoja wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika umoja ambao hivi sasa haupo tena kwani uhuru ulikuja na changamoto zake na moja ya changanoto kubwa ikawa kuzuka kwa uadui dhidi ya Uislam ikawa chochote kinachowahusu Waislam hakiangaliwi kwa jicho la kheri na wale walioshika madaraka ya serikali.

Taratibu hata historia hii ya wazalendo hawa waliopigania uhuru ikawa haitakiwi na zikafanyika juhudi kubwa na za makusudi kuwafuta mashujaa hawa katika historia ya Tanganyika.

Wazee wetu wameonyesha kuwa dini inaweza kutumika kuwaunganisha watu.
Bahati mbaya sana leo dini inatumika kuwabagua watu.

MWISHO
 
Steveache,
Hakuna udini katika historia hii ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Kitabu kimefanyiwa mapitio na mabingwa wa African History hakuna aliyesema nimeandika kitabu cha dini.

Library of Congress wamekikatalogi hawakukiweka kitabu upande wa dini.

Kunipuuza si kitu chepesi.

Ungepuuza usingekuja hapa kunijibu ungepita wima.

Kitabu hiki kinakwenda toleo la nne Kiingereza na Kiswahili na kiko katika Cambridge Journal of African History nk. nk.

Si kama napiga zumari langu mwenyewe ila nakufahamisha kuhusu historia hii unayodhani kuwa imepuuzwa.

Hiki ndicho kitabu kilichofanya uandikwe wasifu wa Julius Nyerere ili kutafuta ukweli wa historia ya TANU.

Watafiti na waandishi Waandishi wa Wasifu wa Julius Nyerere walikuja nyumbani kwangu mara mbili kunihoji kuhusu maisha ya Mwalimu Nyerere na Abdul Sykes wakati wa kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hicho wewe unachokiita "kivuli," ndicho kilichafanya kitabu changu kije na taarifa mbazo hakuna aliyekuwa anajua zipo.

Yapo mengi lakini tosheka na haya kwa sasa.
Mimi si mtu wa kupuuzwa.

Mzee,ukubali ukatae udini uliokujaa umekutafuna sana na huo ndio udhaifu wako mkubwa,inawezekana usijione lakini hadhira inayosoma maandiko yako inaliona hili.

Tokea nijiunge humu JF sijawahi kuona andiko lako hata moja lisilo na mwelekeo wa kidini,naendelea kusema wengine hata hatukusomagi ila tunapitiaga michango ya wachangiaji wengine tu ktk mabandiko yako na ndio hao tunaowaquote,hapa nimekujibu kwa kuwa umeniquote personally la sivyo ningekupuuza kama navyokupuuzaga siku zote na mabandiko yako ya kìitikadi yenye lengo la kujaza watu chuki.
 
  • Thanks
Reactions: T11

Steveachi,
Ikiwa wewe unaona mimi naandika dini wajuzi wa tafiti na historia hawajaniona hivyo.

Hawa mfano wa Oxford University Press East Africa wamenishirikisha katika mradi wa kuandika vitabu vya kiada kwa shule za msingi na wamechapa kitabu changu, "The Torch on Kilimanjaro," (2007) sasa kipo toleo la pili.

Wamenishirikisha pamoja na waandishi wengine kutoka Afrika katika kitabu, "The Mermaid of Msambweni," (2008)(African Anthology).

Oxford University Press New York mradi wa Harvard wa Dictionary of African Biography wamenishirikisha kama mwandishi katika kundi la zaidi ya waandishi 500 kutoka nchi tofauti.

Hizi ni volumes 6 na nimeandika historia ya Kleist Sykes (1894 - 1949).

Nimealikwa University of Iowa na Northwestern University Illinois, Marekani kuzungumza historia hii tunayojadili hapa.

Nimealikwa Zentrum Moderner Orient, Berlin Ujerumani kuzungumza na kuandika chochote nitakacho na ukifika katika maktaba yao utaikuta paper yangu, "Tanzania: "A Nation Without Heroes."

Hili la kuwa mimi naandika dini nalisikia kwenu tu na sababu yake mnataabika kusoma nini Waislam walifanya katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Wachapaji vitabu wakubwa duniani na vyuo vikuu wananitafuta.

Hamuipendi historia hii na ndiyo sababu iliwezekana kuandikwa historia ya TANU iliyofuta mchango wa Waislam.
 
Inawezekana pamoja na kushirkishwa kwako na kutokana na kuchanganya kwako mambo ya udini na historia ndio maana hayo machapisho yako yanabakia maktaba kwako tu kama maoni yako binafsi na hayachapishwi kwetu tuyaone kwa uwazi
 
Maktaba kwangu vipi ilhali vitabu vyangu vimechapwa na Oxford University Press na vinauzwa madukani?

Kitabu cha Abdul Sykes kinasomeshwa vyuo vikuu Ulaya na Marekani kama rejea muhimu katika historia ya Tanzania.
 
Duh,kweli nafsi imeghadhabika

Kila la kheir
 
Nguvu darsa la mtandaoni si sawa na darsa unaloliona kwa macho ukatambua kuwa hawa jana walinisikiliza kwa hiyo nitaendelea nilipokomea jana.

Kwenye mtandao unazungumza na watu wapya kila dakika.

Kuna waliokuwapo toka mwanzo wa darsa na kuna wengine darsa wamelikuta liko katikati.

Ikiwa wewe upo toka mwanzo na darsa lile ushalisikia huna sababu ya kujichosha una delete au unapita wima unasoma mambo mapya.

Mtandaoni mwalimu hawezi kusema hili nilishalieleza hivyo atalieleza upya au ataweka link mtu aingie na kusoma.

Huna sababu ya kuteseka katika mtandao unaweza ku-delete, kupita wima hufungui hata ku-block kuondoa bughdha.

Naamini umeelewa.
[/QUOT
Noted mzee!
 
La hasha mzee Mohamed Said ,nachoamini religious sentimentals zinatakiwa zikae mbali sana ukitaka kueleweka vizuri hata na wasio wa upande wako,hata kama unaupenda sana upande wako
Steve...
Nimekueleza kuwa kazi zangu zimepitiwa na mabingwa na hakuna hata mmoja aliyeona kuwa kuna dini ndani yake.

Tatizo lako wewe unataabika kwa kuwa historia hii ni historia ya Waislam.

Unashindwa kutofautisha baina ya Waislam na Uislam.
 
Unafahamu malengo ya hao unaowaita ni mabingwa?

Unafaham ya kuwa inawezekana kutokuambiwa kwako wewe ni mojawapo ya malengo yao ili yatimie?

Wanaoona mbali wanasema na kukemea,wao hawakukemea ili matakwa yao yaendelee kutimia na hiyo ndio furaha yao.
 
Kwani wao ndiyo waliowatuma Chuo Cha CCM Kivukoni waandike historia iliyokuwa siyo?

Mimi nisingeandika kitabu cha Abdul Sykes kama ingeandikwa historia ya kweli.
 
Mbona hakuna mapingamizi kutoka vyuo vingine tena vikuu kabisa kukosoa hiyo historia unayodai kuwa imepotoshwa??
 
  • Thanks
Reactions: T11
Mbona hakuna mapingamizi kutoka vyuo vingine tena vikuu kabisa kukosoa hiyo historia unayodai kuwa imepotoshwa??
Steve...
Katika duru za kisomi kitabu hupingwa maudhui yake na kitabu kingine.

Nimekipinga kitabu cha Historia ya TANU cha Abubakar Olotu na cha Kivukoni kwa kitabu cha Abdul Sykes.

Hivi ndivyo inavyotakiwa iwe.

Lakini unaweza pia ukakihoji kitabu kwa maswali kwa njia za kistaarabu si kwa lugha kali, kuzomea na kuitana majina.

Kitabu cha Kivukoni hakikukidhi viwango kiasi kwamba hata Idara ya Historia Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam hawakifanyii rejea.

Yaani hakisomeshwi kwenye kozi yeyote.
 
Steveachi,
Ikiwa wewe unaona mimi naandika dini wajuzi wa tafiti na historia hawajaniona hivyo.

Hawa mfano wa Oxford University Press East Africa wamenishirikisha katika mradi wa kuandika vitabu vya kiada kwa shule za msingi na wamechapa kitabu changu, "The Torch on Kilimanjaro," (2007) sasa kipo toleo la pili.

Wamenishirikisha pamoja na waandishi wengine kutoka Afrika katika kitabu, "The Mermaid of Msambweni," (2008)(African Anthology).

Oxford University Press New York mradi wa Harvard wa Dictionary of African Biography wamenishirikisha kama mwandishi katika kundi la zaidi ya waandishi 500 kutoka nchi tofauti.

Hizi ni volumes 6 na nimeandika historia ya Kleist Sykes (1894 - 1949).

Nimealikwa University of Iowa na Northwestern University Illinois, Marekani kuzungumza historia hii tunayojadili hapa.

Nimealikwa Zentrum Moderner Orient, Berlin Ujerumani kuzungumza na kuandika chochote nitakacho na ukifika katika maktaba yao utaikuta paper yangu, "Tanzania: "A Nation Without Heroes."

Hili la kuwa mimi naandika dini nalisikia kwenu tu na sababu yake mnataabika kusoma nini Waislam walifanya katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Wachapaji vitabu wakubwa duniani na vyuo vikuu wananitafuta.

Hamuipendi historia hii na ndiyo sababu iliwezekana kuandikwa historia ya TANU iliyofuta mchango wa Waislam.
Acha habari za hatuipendi historia, kwanini tusiipende?

Umekua unatumia utetezi wa kuaminika kwako na vyuo mbalimbali kwamba wao mbona hawaoni udini

Wao hukai nao JF, haya ya uislamu unayasema huku, kule unataja majina tu

Huku ndio tumekushtukia kwamba ni mzee mmoja anayezeeka vibaya
 
Back
Top Bottom