Nafsi ni kitu gani?


Nafsi wewe mwenyewe.
Ukisoma kitabu kiitwacho Biblia, sehemu ya mwanzo sura ya pili mstali w saba. Mwanzo 2.7 pameeleza kuwa Baada ya kuumbwa binadamu akapuliziwa pimzi. Ndipo binadam akawa nafsi hai.

Ieleweke wazi kwamba binadamu hana nafsi, hivyo usisumbuke kuitafuta nafsi mwilini mwa binadamu. Bali huyo mtu ndio nafsi.

Andiko linasema binadamu akawa nafsi. Yaani baada ya kupuliziwa tu pimzi akawa nafsi.

Hivyo mkuu usihangaike kutafuta nafsi ipo wapi? Hata wewe ni nafsi.

Ukiulizwa wewe ni nani.. Jibu kuwa wewe ni nafsi.
 
Mwanadamu hana miili mitatu mkuu bali mwanadamu ana sehemu kuu tatu yaani mwili, nafsi na roho.

Nafsi ni sehemu ambayo mawazo, hisia na utashi unapatikana.

Mwili kazi yake ni kutoa viashiria kama mtu anatawaliwa zaidi na nafsi yake au roho yake.

Ni kwa ufupi tu.
 
Vyote nisisi ndio tumetengeneza kwa lugha katika uhalisia hamna hata kimoja
 
ROHO: NI hali ya uhai "activeness" in things and animals
Nafsi : ni msingi wa utambulisho tuu, cha hali ndani yake"Identity" Mfano unaposema nafsi yangu mimi nafsi yake yeye.
 
there is only consious no subconcious...kuna watu wanaweza kusimamisha hali tofauti ambazo unaweza kusema ni involuntary....utofauti ni kwamba hatupo makini na consious yetu.
 
Mind: the element of a person that enables them to be aware of the world and their experiences, to think, and to feel; the faculty of consciousness and thought.

Soul: the spiritual or immaterial part of a human being or animal, regarded as immortal

Immortal: living forever; never dying or decaying

Kwa ufupi kabisa mwili ni mwili huu tunaouona,nafsi ni kama akiri ya roho,sehemu ya ufahamu ya roho,inayofanya maamuzi na kureason.Kwa habari za hukumu itakayohukumiwa ni nafsi ya mtu,roho inaangamia kama nafsi ikiangamizwa kwa sababu roho inabeba nafsi,huwezi tenganisha au naweza sema kila nafsi kuna roho inaandamana nayo.
 


Wadau naomba tafadhali na mimi nitoe mawazo yangu, Mtu nI Roho ana kaa katika Mwili na anayo Nafsi. Kama Mungu Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.

SisI tumeumbwa tukawa Triune being (1Thesalonike 5:23).

Nafsi inajengwa na element tatu za Mind as a leading part of the Soul (Nafsi) Will (Nia) and Emotions (Hisia)

Kwenye Mind ndio tuna intellect, Kwenye will ndio tuna Choices na Kwenye Emotions ndio tuna feelings. Hizi zinamtofautisha Mwana damu na lower animals.
 
nimekuelewa....
 
wanasayansi walifanya jaribio la kuchunguza roho wakati mtu anapofariki walimchukua mtu wakamweka katika box la kioo liliojaa maji mara baada ya yule mtu kukaribia kukata roho waliona maji yanatoa kitu kama povu walipochunguza kwa kina hakuna walichoona NB quran inasema wanakuuliza kuhusu habari za roho wambie roho ni katika mambo ya allah sw isopukuwa binadam tumepewa kwa kiasi kidogo sana ktk ilimu yake kwa watu aliowachagua hvyo basi hakuna mtu mwenye majibu sahihi ya mwili roho nafsi akili kwa sabab mwili huliwa na wadudu baada ya kufa lkn roho hurudi kwa allah sw nafsi ni matamanio yani yanweza kuwa mazuri au mabaya ila akili ni maamuzi yanaweza kuwa sahihi ama la.nafsi ikishatamani akili hupewa jukuma kuamua
 
wewe unachanganya madesa.
Nafsi ni kitu kingine Roho haikai kwenye Moyo...Roho na Nafsi vyote vipo kwenye ulimwengu wa Roho (Vitu visivyoonekana...na akili na Moyo vipo kwenye ulimwengu wa Mwili (Vitu vinavyoonekana)
Nafsi ni Identity yako wewe, ndio inayokutofautisha na binadamu mwengine yeyote yule kwenye huo ulimwengu wa nafsi. yenyewe hubeba riziki zako zote, uelewa na Vipaji vyote ulivyonavyo. Na nafsi haifi, itadumu milele na milele...ila muda ukifika, itauacha mwili wako. Unapoona watu wanapandwa na majini..ni kuwa wanaruhusu nafsi zao zikae pembeni, ili mwili wao utumike na hao majini. kwa wale wa kufanya Meditation, huwa wanazisafirisha nafsi zao na kwenda mahala pengine, huku wakiuacha mwili wao pale ulipo. ila wakibugi stepu, wanaweza wasirudi tena kwenye miili yao. na ndo amaana watu hufa.
hatujui mengi zaidi ya ulimwengu wa roho, na ndio maana wachawi na wengineo wanao uelewa mwingi zaidi wa dunia hiyo ya vitu visivyoonekana kwa macho ya mwili.
 
Roho ni ile pumzi tunayopuliziwa na mungu mwenyewe. na hii roho ndo kiunganish pekee kati yetu na mungu. siku hizo pumzi zitakapokata na ndo mwisho wa uhai wako hapa duniani.
Yah, Roho ni kama Activator/Verification/Password ya Wewe. Ni Daraja kuu kati yako na Mungu. Bila roho, hauwezi kuwa kiumbe chochote kile. Ni Mungu mwenyewe anajua, na ndio aliyokupulizia kukuumba, inaishi kizazi na kizazi kwa kuzaliana...e.t.c; na kwa kupitia hiyo, unapopiga goti na kusali, unatumia mawasiliano yako uliyonayo na Mungu, kuwasiliana naye mojakwamoja. na ndio maana anakusikia, na anaweza kukujibu au laa. nadhani ukijiuliza kwanini unafumba macho ukisali, utapata jibu sahihi, sio?
 
Vyote nisisi ndio tumetengeneza kwa lugha katika uhalisia hamna hata kimoja
Uhalisia upo, ukifanya utafiti yakinifu na kusoma kwa bidii, ndugu.
penye elimu ifuate, ili uijue, na sio kuishia nje....na kusema unayoyajua wewe
 
Nafsi: ni ufahamu unaomtambulisha mtu, ni utambuzi unaoidhinisha na kudhihirisha uwepo wa mhusika.
Kitabu cha mwanzo kinaeleza jinsi Adam alivyoumbwa toka mavumbini, Mungu alimpulizia pumzi ya uhai na Adam akawa nafsi hai.

Nafsi(soul) is self identity that presents a person.
 
Uhalisia upo, ukifanya utafiti yakinifu na kusoma kwa bidii, ndugu.
penye elimu ifuate, ili uijue, na sio kuishia nje....na kusema unayoyajua wewe
Labda huo utafiti ulioufanya ni upi?na umesoma wapi? Kabla hujafika hata mbali Nafsi ni nini? Na ipo wapi? Na kwanamna gani tunaweza kuifahama kama sio human invention
 
Labda huo utafiti ulioufanya ni upi?na umesoma wapi? Kabla hujafika hata mbali Nafsi ni nini? Na ipo wapi? Na kwanamna gani tunaweza kuifahama kama sio human invention
Soma vitabu vya Falsafa, na kisha pitia Maandiko ya Dini..utapata baadhi ya Majibu.
kama unataka niwe Tutor wako...pole sana. watafute wanaojua zaidi wakuelekeze
 
Soma vitabu vya Falsafa, na kisha pitia Maandiko ya Dini..utapata baadhi ya Majibu.
kama unataka niwe Tutor wako...pole sana. watafute wanaojua zaidi wakuelekeze
Nafsi inavyomaanisha kwa Falsafa ni tofauti naunayo maanisha? Kwa falsafa nafsi ni sawasawa na Mind!!
Dini ndio ipo njee kabisa hata wanaloelezea hawawezi kudhibitisha.
Wala sijasema wewe uwe Tutor wangu ninacho omba ujibu hayo maswali kusema nikasome vitabu nisawa nakuniambia nikasome mawazo ya mtu mwingine na wakati wewe unauwezo wakutoa uwelewa wako juu ya kitu unachoamin.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…