Heshima kwenu wadau, nijuavyo mi ni kwamba binadamu ana mihimili mikuu mitatu. Kwanza ni roho, pili ni mwili na tatu ni nafsi.
ROHO nafahamu ni ile pumzi ya uzima kutoka kwa mungu mwenyezi, ambayo ipo connected na Mungu mwenyewe.
MWILI ni Physical appearance ya mtu ambayo inajumuisha milango yote ya fahamu. Kwa suala la NAFSI bado sijalipatia ufumbuzi.
Naomba mwenye elimu zaidi atujuze.
Nafsi wewe mwenyewe.
Ukisoma kitabu kiitwacho Biblia, sehemu ya mwanzo sura ya pili mstali w saba. Mwanzo 2.7 pameeleza kuwa Baada ya kuumbwa binadamu akapuliziwa pimzi. Ndipo binadam akawa nafsi hai.
Ieleweke wazi kwamba binadamu hana nafsi, hivyo usisumbuke kuitafuta nafsi mwilini mwa binadamu. Bali huyo mtu ndio nafsi.
Andiko linasema binadamu akawa nafsi. Yaani baada ya kupuliziwa tu pimzi akawa nafsi.
Hivyo mkuu usihangaike kutafuta nafsi ipo wapi? Hata wewe ni nafsi.
Ukiulizwa wewe ni nani.. Jibu kuwa wewe ni nafsi.