Nafsi ni kitu gani?

Nafsi ni kitu gani?

MATHAYO 10:28.

"Inasema. ....Msiwaogope wale wauao mwili lakiniawa wezi kuiua roho .
Afadhali zaidi kumwogopa yule awezaye kuangamiza mwili pamoja na roho katika moto wa jehanamu.

Hapo tuna ona kwamba roho , ina weza kuishi hata baada ya mwili kufa.

Napia tuna jifunza kwamba roho , nayenyewe ina weza kuangamizwa lakini namungu peke yake.

Sasa kama niivyo tuki sema roho nikiumbe tuta kosea??.
 
Mods hebu wekeni utaratibu mpya wa kutoa hizi status... eti mtoa mada naye ni jf-expert member''!!
Usi lala mike kama una ona hilo jina lina nipwaya yani , jf-expert member"!! Sio fibaya kupendekeza niitwe nani nitashukuru pia.
 
kwa faida yako, kuna aina mbili za ufahamu. 'conscious mind' na 'sub conscious mind'. conscious mind ni aina ya ufaham ambao nimeuzungumzia hapo juu. ni ule unatumia milango ya fahamu. ufahamu unadili na mambo ya hiari tu, kama vile kusikiliza, kula na mambo yote unayojiongoza katika kuyafanya. conscious mind ipo kwa ajili ya kuchambua kila tendo ulifanyalo. tukija kwenye sub conscious huu ni aina ya ufahamu hujiongoza wenyewe. hu deal na matendo yasiyo hiari, mfano unapolala conscious mind inakua haifanyi kaz. lakin kinachofanya mapigo ya moyo yaendelee kupiga, msukumo wa damu na kupumua ni sub conscious. i hope nimechangia.......Aseee Upo sawa mkubwa.!
 
Heshima kwenu wadau, nijuavyo mi ni kwamba binadamu ana mihimili mikuu mitatu. Kwanza ni roho, pili ni mwili na tatu ni nafsi.

ROHO nafahamu ni ile pumzi ya uzima kutoka kwa mungu mwenyezi, ambayo ipo connected na Mungu mwenyewe.

MWILI ni Physical appearance ya mtu ambayo inajumuisha milango yote ya fahamu. Kwa suala la NAFSI bado sijalipatia ufumbuzi.

Naomba mwenye elimu zaidi atujuze.

Heshima.

Unaweza kupata mwangaza zaidi juu ya mashauri ya hayo ambayo ungelipenda kuyabaini namna zake za kuzungumzia.

Ninashauri ukisome kitabu hichi: The Aquarian Age Gospel of Jesus, the Christ of the Piscean Age Author Levi H. Dowling

Humo kuna mengi ya msaada mno kwa kadri ya kiu yako ya kutamani kujua mielekeo ya hakika kutambua ukweli.

Ila hapa nitanukuu aya moja na kukutafsiria kama kitekenyo.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Aquarian Age Gospel of Jesus
Injili ya zama za Ndoo ya Yesu


Chapters 8 - 14
Sura 8 - 14


CHAPTER 8
Sura ya 8


Elihu's lessons. The unity of life. The two selfs. The devil. Love the saviour of men. The David of the light. Goliath of the dark.


Masomo ya Elihu. Umoja wa Uzima. Nafsi mbili. Ibilisi. Upendo mwokozi wa Watu. Daudi wa nuru. Goliati wa giza.

AGAIN Elihu met his pupils in the sacred grove and said, TENA Elihu alikutana na wanafunzi wake uani patakatifu na kusema , 2 No man lives unto himself; for every living thing is bound by cords to every other living thing. Hakuna mtu ajiishiye tu yeye mwenyewe; kwa kuwa kila kile chenye kuishi chafungamana kamba na kila kingine chenye kuishi 3 Blest are the pure in heart; for they will love and not demand love in return. Wamebarikiwa wenye moyo safi; kwa kuwa wao wapenda na si kutaka upendo kurejeshwa. 4 They will not do to other men what they would not have other men do unto them. Hawatawatendea watu wengine vile wengine wasingaliwatendea wao 5 There are two selfs; the higher and the lower self. Kuna nafsi mbili; nafsi ya juu na ya chini 6 The higher self is human spirit clothed with soul, made in the form of God. Nafsi ya juu ni roho ya mtu kuvikwa sonafi, iliyofanyika kwa namna ya Mungu 7 The lower self, the carnal self, the body of desires,is a reflection of the higher self, distorted by the murky ethers of the flesh. Nafsi ya chini, nafsi ya mwili wa nyama, mwili wa matamanio, ni mwakisiko wa nafsi ya juu, kuharibiwa uhalisia wa sura yake na aetha nzito za nyama. 8 The lower self is an illusion, and will pass away; the higher self is God in man, and will not pass away. Nafsi ya chini ni danganyiko la kimuonekano, nayo itapita zake; nafsi ya juu ni Mungu katika mtu, nayo haitapita zake 9 The higher self is the embodiment of truth reversed, and so is falsehood manifest. Nafsi ya juu ni ujazwa mwili wa kweli katika namna iliyopinduka, na hivyo ni isikweli kudhahirika 10 The higher self is justice, mercy, love and right; the lower self is what the higher self is not. Nafsi ya juu ni usawa wa haki, rehema, upendo na sahihi; nafsi ya chini ni kile isivyo nafsi ya juu 11 The lower self breeds hatred, slander, lewdness, murders, theft, and everthing that harms; the higher self is mother of the virtues and the harmonies of life. Nafsi ya chini huzaa chuki, usingiziaji, ukosaji heshima, mauaji, uwizi, na kilakitu chenye kuleta madhara; Nafsi ya juu ni mama wa kudra njema na matangamano ya uzima 12 The lower self is rich in promises, but poor in blessedness and peace; it offers pleasure, joy and satisfying gains; but gives unrest and misery and death. Nafsi ya chini ni tajiri ya ahadi, lakini i ni masikini ya ubarikika na amani; yaahidi kupatia starehe, furaha na mapatiko ya kuridhisha nafsi; lakini hutoa kutokutulia na dhiki na mauti 13 It gives men apples that are lovely to the eye and pleasant to the smell; their cores are full of bitterness and gall. Huwapa watu matunda ambayo yenye kuonekana ya kupendeka na mazuri kwa harufu; ndani mwake yamejaa uchungu na nyongo 14 If you would ask me what to study I would say, yourselves; and when you will have studied them, and then would ask me what to study next, I would reply, yourselves. Ikiwa mtaniuliza kipi mngalikusoma kujua ningalisema, ninyi mwenyewe; na mara mtakapokuwa mmezisoma, na halafu kuniuliza kipi tusome kufuatia, ningaliwajibu, ninyi wenyewe. 15 He who knows well his lower self, knows the illusions of the world, knows of the things that pass away; and he who knows his higher self, know God; knows well the things that cannot pass away. Yeye aijuaye vema nafsi yake ya chini, ayajua madanganyiko ya kimuonekano ya ulimwengu, avijua vitu vyenye kupita kwenda zake; na yeye mwenye kuijua nafasi yake ya juu, amjua Mungu; avijue vile visivyoweza kupita. 16 Thrice blessed is the man who has made purity and love his very own; he has been ransomed from the perils of the lower self and is himself his higher self. Amebarikiwa mara tatu mtu aliyeufanya usafi wa moyo na upendo kuwa ni wake; yeye ametolewa gharama za kugombolewa toka kwenye kingo za maanguko za nafsi yake ya chini na yeye mwenyewe ni nafsi yake ya juu 17 Men seek salvation from an evil that they deem a living monster of the nether world; and they have gods that are but demons in disguise; all powerful, yet full of jealousy and hate and lust; Watu wanatafuta kukombolewa kutoka kwenye uovu ambao wao wachukulia kusema ni dubwana la mahala pa chini kuzimu ; na wana miungu ambayo ni mapepo pagaishaji yaliyo na sura ya kujificha; yenye nguvu tele, na hapo hapo kujaa chuki na matamanio ya kimwili;18 Whose favours must be bought with costly sacrifice of fruits, and of the lives of birds, and animals, and human kind. Ambayo fadhila zake lazima kununuliwa na kafara za kigharama za matunda, na za uhai wa ndege, na wanyama, na mwanadamu 19 And yet these gods possess no ears to hear, no eyes to see, no heart to sympathise, no power to save. Na hapo hapo miungu hao hawana masikio kusikia, hawana macho kuona, hawana moyo kuonea huruma, hawana nguvu kuokoa. 20 This evil is myth; these gods are made of air, clothed with shadows of a thought. Uovu huu ni ngano; miungu hawa wamefanyika kwa hewa, kuvikwa na vimvuli vya fikra. 21 The only devil from which men must be redeemed is self, the lower self. If man would find his devil he must look within; his name is self. Ibilisi pekee ambaye toka kwa huyo watu hawana budi kukombolewa ni nafsi, nafsi ya chini. Ikiwa mtu angalikumpata ibilisi wake yeye yampasa kutazama ndani yake; jina lake ni nafsi. 22 If man would find his saviour he must look within; and when the demon self has been dethroned the saviour, Love, will be exulted to the throne of power. Ikiwa mtu angalikumtafuta mwokozi wake yeye hana budi kutazama ndani yake; na pale ambapo ibilisi ametolewa katika kiti chake cha enzi mwokozi, upendo, atainuliwa kwenye kiti cha nguvu. 23 The David of the light is Purity, who slays the strong Goliath of the dark, and seats the saviour, Love, upon the throne. Daudi wa nuru ni usafi wa moyo, mwenye kumchinjilia mbali Goliati wa kiza, na kumketisha enzini mwokozi, Upendo.


Chanzo cha nukuu: The Aquarian Age Gospel of Jesus, the Christ of the Piscean Age
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Baraka
 
Akili ni ule ufahamu wa kuweza kupembua zuri na baya, jema na ovu. na kuna milango mikuu 5 ya fahamu, ambayo akili inaweza kutumia katika utendaji wake. kwa mfano kwa kutumia mlango wa fahamu wa ulimi, akili inaweza kutofautisha maelfu ya ladha. ulimi ni kama kiwakilishi tu, coz kama ukiwa umezimia kwa mfano, hata ukipewa kitu uonje hutoweza kupata ladha, why?? kwa sababu ufahamu wako(akili) haifanyi kaz kwa wakati huo. kwa akili ndo fahamu yenyewe inayokuongoza kufanya shughuli. na ulimi, sikio, ngozi, macho na pua hi ni milango ambayo akili inatumia katika utendaji wake. ntaendelea upande wa roho.
Akili hupimwa na nn?
 
kwa faida yako, kuna aina mbili za ufahamu. 'conscious mind' na 'sub conscious mind'. conscious mind ni aina ya ufaham ambao nimeuzungumzia hapo juu. ni ule unatumia milango ya fahamu. ufahamu unadili na mambo ya hiari tu, kama vile kusikiliza, kula na mambo yote unayojiongoza katika kuyafanya. conscious mind ipo kwa ajili ya kuchambua kila tendo ulifanyalo. tukija kwenye sub conscious huu ni aina ya ufahamu hujiongoza wenyewe. hu deal na matendo yasiyo hiari, mfano unapolala conscious mind inakua haifanyi kaz. lakin kinachofanya mapigo ya moyo yaendelee kupiga, msukumo wa damu na kupumua ni sub conscious. i hope nimechangia.
Umeacha moja unconscious mind
 
Nimetoka kapa ,sijajua nafsi ni nini .
 
Akili ni ule ufahamu wa kuweza kupembua zuri na baya, jema na ovu. na kuna milango mikuu 5 ya fahamu, ambayo akili inaweza kutumia katika utendaji wake. kwa mfano kwa kutumia mlango wa fahamu wa ulimi, akili inaweza kutofautisha maelfu ya ladha. ulimi ni kama kiwakilishi tu, coz kama ukiwa umezimia kwa mfano, hata ukipewa kitu uonje hutoweza kupata ladha, why?? kwa sababu ufahamu wako(akili) haifanyi kaz kwa wakati huo. kwa akili ndo fahamu yenyewe inayokuongoza kufanya shughuli. na ulimi, sikio, ngozi, macho na pua hi ni milango ambayo akili inatumia katika utendaji wake. ntaendelea upande wa roho.
Mkuu umejitahid kuleleza vzr lkn hapa kwenye maana ya akili. Cdhan km IPO sahh sana kwasababu kuna mambo kwako n uovu lkn kwa wengine cvyo, kuna mambo kwako n mema ila kwa wengine c mema, hii haiwez kualalisha kipmo cha akl
 
Mkuu umejitahid kuleleza vzr lkn hapa kwenye maana ya akili. Cdhan km IPO sahh sana kwasababu kuna mambo kwako n uovu lkn kwa wengine cvyo, kuna mambo kwako n mema ila kwa wengine c mema, hii haiwez kualalisha kipmo cha akl
mbona mkuu mi cjatoa kipimo cha akili hapo. mi nimeeleza akili ni nini? na kazi yake ni nini? na milango yake ni ipi? bado cjaeleza kipimo cha akili. but nikipata wasaa ntaeleza.
 
Heshima kwenu wadau, nijuavyo mi ni kwamba binadamu ana mihimili mikuu mitatu. Kwanza ni roho, pili ni mwili na tatu ni nafsi.

ROHO nafahamu ni ile pumzi ya uzima kutoka kwa mungu mwenyezi, ambayo ipo connected na Mungu mwenyewe.

MWILI ni Physical appearance ya mtu ambayo inajumuisha milango yote ya fahamu. Kwa suala la NAFSI bado sijalipatia ufumbuzi.

Naomba mwenye elimu zaidi atujuze.

Katika Biblia, neno “nafsi” hutafsiriwa kutoka neno la Kiebrania neʹphesh na neno la Kigiriki psy·kheʹ. Matumizi ya Biblia huonyesha nafsi ni mtu au mnyama au uhai wa mtu au mnyama.
1 Petro. 3:20: “Katika siku za Noa . . . watu wachache, yaani, nafsi nane, walichukuliwa salama kupitia maji.” (Neno la Kigiriki linalotafsiriwa hapa “nafsi” ni psy·khaiʹ, ambalo ni wingi wa neno psy·kheʹ.
Walawi. 24:17, 18: “Ikiwa mtu ataipiga nafsi [Kiebrania, neʹphesh] yoyote ya mwanadamu kiasi cha kuiua, lazima atauawa. Naye mwenye kuipiga nafsi [Kiebrania, neʹphesh] ya mnyama wa kufugwa kiasi cha kuiua atalipa, nafsi kwa nafsi.” (Ona kwamba neno lilelile la Kiebrania kwa nafsi linatumiwa kuhusu wanadamu na wanyama pia.)
 
Kwa mtazamo wangu nafsi ndio wewe mwenyewe na sio huo mwili...ni kitu ambacho hakiwezi kuonekana kwa kushikwa wala kwa kutumia chombo chochote.

Na kutoonekana kwake hakuondoi maana kuwa hakuna hicho kitu na ili kuthibitisha hilo ndio maana Mungu akatoa angalizo

"Ole wao wenye kudhurumu nafsi zao na za wenzao"

Hii ni kuashiriabkuwa nafsi ndio binadamu halisi na sio mwili.
 
Kwa mtazamo wangu nafsi ndio wewe mwenyewe na sio huo mwili...ni kitu ambacho hakiwezi kuonekana kwa kushikwa wala kwa kutumia chombo chochote.

Na kutoonekana kwake hakuondoi maana kuwa hakuna hicho kitu na ili kuthibitisha hilo ndio maana Mungu akatoa angalizo

"Ole wao wenye kudhurumu nafsi zao na za wenzao"

Hii ni kuashiriabkuwa nafsi ndio binadamu halisi na sio mwili.
bas ni sawa na kusema roho + mwili = nafsi.
 
Back
Top Bottom