Nafurahi kuona ligi ya Tanzania ikikua kwa kasi lakini...

Nafurahi kuona ligi ya Tanzania ikikua kwa kasi lakini...

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
1,842
Reaction score
6,087
Karibuni kwenye huu mjadala.

Kwa miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia kuona ligi ya Tanzania ikikua kwa kasi saaana, yote ikichagizwa na azam media kongole kwao kwa udhamini mnono.

Tumeshuhudia timu Kama Simba, Yanga, Azam wakiwa na uwezo wa kung'oa wachezaji tokea mataifa makubwa tena wakiwa ni wachezaji tegemeo.

Naiona ligi ikiendelea kukua sana na kufatiliwa ndio maana Azam wakaweka mkataba wa kimang'ung'o wa Msovero wa miaka 10.

Wengi tumeshuhudia hile mbugi ya hawa singida hasa wale wa Brazil wake kuna jamaa inaitwa Federico hatari sana. Nafurahi kuona competition itakayo kuepo kati ya Azam na singida big stars kugombania nafasi ya 3/4.

Twende kwenye hoja ya msingi, kiuhalisia ubora wa hizi timu umechangiwa na wachezaji wengi tokea nje ya Tanzania. vipi ubora wa wachezaji wetu wa ndani?

Je, tunapotea Kama taifa kwa kujaza wachezaji wengi wa nje?..je TRA sasa waangalie mpira kwa jicho la biashara waanze kukata kodi Kama nchi nyingine wanavyofanya?.....
 
NO DOUBT, UBORA WA LIGI YETU PIA UMECHANGIWA NA WACHEZAJI WA NJE

Wazawa baadhi yao hawajitumi na kuonesha ushindani na ndio maana leo usishangae unaweza kupanga first XI kwenye kikosi cha Simba au Yanga ukakuta wazawa wanaingia wawili hadi watano lakini wanobakia wote ni wachezaji wa kigeni
 
NO DOUBT, UBORA WA LIGI YETU PIA UMECHANGIWA NA WACHEZAJI WA NJE

Wazawa baadhi yao hawajitumi na kuonesha ushindani na ndio maana leo usishangae unaweza kupanga first XI kwenye kikosi cha Simba au Yanga ukakuta wazawa wanaingia wawili hadi watano lakini wanobakia wote ni wachezaji wa kigeni
Kweli kabisa, matokeo yake CHAN tunajikuta tunapata tabu kwa Somalia
 
Mi naungana nawewe kwenye mkataba wa kinyonyaji wa Azam...TFF kupitia bodi ya ligi wangekua na channel yao inayorekodi mechi na kuwauzia Azam na makampuni mengine kama tunavyoona kwenye EPL haki zakuonyesha mechi wamepewa channel mbalimbali kulingana na zabuni na dau lao kama Multichoices kupitia dstv.

Startimes nao wangekua wanapewa baadhi ya mechi za kuonyesha za NBC timu zetu zingekua mbali kwani watanzania kwa sasa tunapenda sana ligi yetu kweli tunaishukuru AZAM Tv kwa kutufanya kuiona ligi yetu na kukua na kupendwa.

Ilipofika TFF kupitia bodi ya ligi inabidi ijiongeze mpira ni biashara ndomana CAF wana channel yao ndomana ikifika group stage za mashindano yanayohusu CAF utanunua haki ya kuonyesha mpira katika channel yao ndio maana mechi za CAF channel iliyorekodi ni moja na matukio yote yanafanana kitakachotofautiana ni kwa channel zinazoonyesha kwa nchi husika zilizopewa kibali kuonyesha mechi zao

Sent from my SM-G9650 using JamiiForums mobile app
 
Mi naungana nawewe kwenye mkataba wa kinyonyaji wa Azam...TFF kupitia bodi ya ligi wangekua na channel yao inayorekodi mechi na kuwauzia Azam na makampuni ...
Yeah umeongea ukweli kabisa, jamaa walichungulia mbali wakaamua kujipigia miaka 10, simba walishtukia hiyo kwenye haki zao za matangazo
 
Kweli kabisa, matokeo yake CHAN tunajikuta tunapata tabu kwa Somalia
Kumbe nawe umeona. Hili ni tatizo kubwa sana. Huwezi kuruhusu timu kuleta wachezaji wa kigeni 12 alafu utegemee kupata timu ya taifa nzuri.

Tunasema kuwa wachezaji wetu waza wajitume, lakini ukweli ni kwamba hatujawekeza pesa kuwaendeleaza. Wee angalia mashindano ya u20 wanacheza mijibaba mikubwa kabisa. Hii ni kutokana na sie kutokuwekeza kwenye youth developement.

Chukulia tuu kwa wastan timu kama singia wachezaji wakigeni 8 uwalipe wastan wa $2000 per month. Hiyo ni million tako kasoro. Wachezaji wanne maanayake ni $8000 per month. Je ukiwekeza hiyo kwenye vijana chini ya umri wa 14 huwezi kupata quality players baada ya miaka kadhaa?

Tusizuie kabisa wachezaji wa kigeni lakini tupunguze idadi iwe mwisho watano basi. Hela nyingine iwekezwe kwenye youth developement. Tukiwa na mipango ya muda mrefu tutapata mafa ikio lakini kwa style ya sasa tutegemee taifa stars kuendelea kuwa kichwa cha mwedawazimu
 
Mi naungana nawewe kwenye mkataba wa kinyonyaji wa Azam...TFF kupitia bodi ya ligi wangekua na channel yao inayorekodi mechi na kuwauzia Azam na makampuni mengine kama...
Muacheni Azam ... Serikali isingeweza kufanya anacho kifanya Azam
 
Wachezaji wetu wa kitanzania baadhi yao ni wavivu, wanabweteka, hawajiongezi na kuleta ushindani unaotakiwa...
Pia tutambue kuwa hatujawaandaa. Tunawataka hao wa nje kwa sababu wameandaliwa. Wamepiga kwenye academy ndio maana wana misingi bora na tunawataka.

So sio tuu tunaishia kusema wavivu hawajitumi. Problem ni sawa tuu na lile la wanaosoma saint kayumba na wale wa international skuls....kwenye ajira watapata wa international tuu.
 
Back
Top Bottom