Nafuu tusiwe na utambulisho kuliko singeli kuwa utambulisho wa muziki wa Tanzania

Nafuu tusiwe na utambulisho kuliko singeli kuwa utambulisho wa muziki wa Tanzania

Batswana wanajitambulisha kwa muziki na uvaaji wao...
Hata sisi twende na singeli ya asili achana na akina Dula

View: https://youtu.be/XPr1fdCWglA?si=oQ6kZnW1PKdMEBBT

Singeli inajulikana mikoa mingapi? Hili jambo sidhani ni la viongozi kupanga. Waachie wananchi waamue. Kinachofanya Tanzania iwe na ugumu wa kuwa na mziki au vazi la taifa ni kuwa makabila yapo mengi sana hivyo kuja na kitu common itakuwa ngumu.
 
View attachment 3241007

Waziri amekengeuka. Wametumia kigezo gani kuifanya singeli ndiyo alama ya Taifa?

Muziki wenyewe umejaa matusi nafuu ingekuwa taarab kwa kuwa yenyewe ina mfumbo. Singeli huwezi kusikiliza na watu unaowaheshimu kama wazazi au watoto, abadan.

Pili ukikuta muziki wenyewe unavyochezwa, ni mtindo wa kukosa maadili tu. Wanawake wanavaa madera mostly bila chupi, halafu wanakamata ardhi then makalio yanakuwa juu ndiyo wanaanza kuyatikisa

Kuna wimbo wa Dulla Makabila una mstari ufuatao "nakupenda wewe na huyo bwanako" ndio uwapelekee duniani utawaeleza maana yake nini? Ujinga mtupu.

Wadau wa muziki mshaurini Waziri Kabudi asitishe UCHAFU huu
Singeli Haina hadhi ya kuitwa muziki Bali NGOMA za kienyeji za kizaramo. Hivi haya maongezi yanayoitwa singeli yanaweza kudokilizwa nje ya Tanzania au kutoboa kimataifa?
 
Singeli inajulikana mikoa mingapi? Hili jambo sidhani ni la viongozi kupanga. Waachie wananchi waamue. Kinachofanya Tanzania iwe na ugumu wa kuwa na mziki au vazi la taifa ni kuwa makabila yapo mengi sana hivyo kuja na kitu common itakuwa ngumu.
Kiswahili hakikuwa kwa Tanzania nzima bali kilisambaa kwa mfumo wa elimu na uelimishaji kuhusu umuhimu wake.
Congo wana aina nyingi ya muziki ila uliopitishwa wakaupambania hadi umekuwa utambulisho wao.
 
Basi na hiyo singeli iachwe isambae, kama inapendeka. Wewe unaona ni fair ku-declare mziki unaochezwa sehemu ndogo tu za mkoa mmoja kuwa ni wa taifa? Mziki ambao wengi hawakubali na hawataki kabisa kuusikia. Kwa nini umma usipewa nafasi ya kuamua?
 
Back
Top Bottom