Naheshimu Kamati ya Usajili ya Simba SC, ila nauliza Shiboub tuliyemwacha ana tofauti gani na huyu Kanoute tunayemsifu leo?

Aliachwa shiboub, akasajiliwa Rally bwalya.
Hakukua na makosa yoyote hapa tena ilikuwa move sahihi zaidi.
Tukija kwa kijana Mpole, hii ni habari nyingine.
Box to Box.....Utamuona anazuia utamuona anashambulia ( kwa ufasaha).
Na mimi nashangaa wanaolinganisha wachezaji ambao hawakupishana kwenye kikosi. Ni miaka miwili tangu Shiboub aachwe hadi Kanoute asajiliwe, sasa utaulizaje sababu ya kuachwa na kusajiliwa kwa hao? Ingefaa swali liwe kwa nini tulimuacha Shiboub tukamsajili Rally Bwalya, hapo walau kuna swali. Eti mtu leo aje aulize kwa nini tulimuacha Laudit Mavugo tukamsajili Perfect Chikwende, wakati katikati yao kuna misimu kibao imepita!
 
Hawa ndio wabongo, wakiamua kuzua tu wanazua.
 
Sharaf Eldin Abrahaman Shibob,sidhan kama nipo sahihi hapo kwenye jina ila alikuwa bonge la player ni Simba tu vile tunapenda kuharibu vipaji vya wachezaji
Tunapenda majina Kanoute, Sakho tukiona majina hayo tunajiona kama kina Kanoute wa West ham united. Ndio yale kama ya Yanga Juninho wakadhani wamekuwa Liverpool. Tuwe wa kweli mchezaji mzuri wa West Africa atakuja huku kwetu kakosa sana ataenda Belgium.
 
Mara nyingi ni ngumu sana kulinganisha wachezaji waliokaribiana viwango. Kwa mtizamo wangu mimi naona Kanoute kamzidi Shiboub kwenye vitu vingi kama vifuatavyo:
1. Kanoute japo ukimwangalia kwa wasiwasi anaonekana laini laini lakini anakaba na anafika sana mwilini kwa wachezaji wa timu pinzani zaidi ya Shiboub.
2. Kanoute ana pumzi sana kuliko ilivyokuwa kwa Shiboub. Shiboub alikuwa anacheza vizuri dakika 35 - 40 baada ya hapo upepo unakata haonekani tena uwanjani. Na hii inatokana na Shiboub kuwa na umri mkubwa sana.
3. Kanoute ni "box to box" wakati Shiboub alikuwa anaweza kucheza kiungo cha juu vizuri tu.
4. Kanoute ana jicho kali na anapiga pasi kwa usahihi zaidi ya Shiboub.
5. Kanoute yupo "fast " sana lakini Shiboub alikuwa "slow"

Kwa Kanoute ni mechi moja tu ameonyesha umahiri wake. Iwapo atashindwa kuendeleza alichokifanya jana nitakuwa tayari kubadili mtizamo wangu hapo juu.
 
Hivi shiboub ana cheza timu gani kwa sasa
Kama sikosei yuko algeria,yule jamaa anajua sana mimi ni Yanga lakini karibia msimu wa pili huu kuna jamaa wa kamati ya usajili uwa nawashtua wamsajili shiboub but inaonekana kumchomoa huko aliko mpunga mrefu
 
Nimepitia comments za watu hapa lakin naona kuna baadhi ya watu ni weupe sana ktk kuchanganua mambo.

We unafaa uwepo ktk kamati ya usajili.

Sio hawa wenzetu vitu vya nyuuma wanavileta leo.

Simba hii kweli ya ni kuilam kamati?

Eti watu wamefura kwa kupigwa jana
[emoji15] ile Tp Mazembe wamekamilika.

Mnataka tuletewe Timu za kawaida ili tushinde kwa kupata ushindi?

No Simba ya sasa tushatoka kule

Nlipenda ule mfumo ktk kikosi cha jana kilichoanza wageni walikuwa 2 tu.
 
Ni kweli mkuu lakini tuonyeshe ukomavu kwa kuwavumilia watu kama hao pale tunapopishana nao kwenye maoni. Kikubwa watu kama hao lazima wawepo kwenye jamii ili jamii ikamilike. Tukatae tukubali tunaweza kukaa watu 100 kuangalia mechi fulani au kumtazama mchezaji fulani "specific" na kila moja akaja na hoja yake tofauti kabisa na mwingine anavyoona. Na yote hii inatokana na "background" ya kila mmoja kwenye mpira.
 
asee we acha tu ata ka kahata niliumia sana
 
[emoji119]
 
Yaani tangia Mchambuzi Farhani wa Clouds FM aseme kuwa Kanoute ni the box to box Midfielder basi kila Mtu sasa akimuelezea Kiungo Kanoute ni lazima aseme neno box to box ili mradi nae aonekane amechambua na anaujua Mpira.
 
Sadio Kanoute na Sakho wamekuja na Sakho alikuwa mchezaji bora wa Tuengue Fc ya Senegal.

Isack na Ernest Boakey walikuwa key player wa Yanga na kuipa ubingwa wakitokea Ghana.

Kubwa zaidi Vicent Bozou kama unakumbuka alisajiliwa Yanga akicheza national team ya Togo kama regular starter kikosini mpaka ameondoka Yanga akiwa regular starter katika kikosi cha timu ya taifa ya Togo. Vipi na yeye alikuwa hana nafasi huko ulaya ?
 
Angebakizwa huyu Rally Bwalya mngemjua? Nani ambaye Kakudanganya kuwa Shiboub aliachwa na Simba SC kwa kushuka Kwake Kiwango? Msilolijua ni sawa na Usiku wa Giza.

Hivi angekuwa ni mbovu ( kashuka Kiwango ) Klabu hiyo Kubwa na Tajiri Kiasi ya nchini Algeria ingemsajili na angekuwa anakiwasha kama afanyavyo sasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…