Nahisi kama nimefikia hatua ya Kukata Tamaa kiwango cha Mwisho. Naomba msaada wenu Ndugu zanguni

Status
Not open for further replies.
JF the home of great thinker's, pole sana kwa changamoto mkuu ila naamini kupitia jukwaa utapata msaada kwani hata mimi mwezi wa 10 nlikuwa nimefikia hatua ya mwsho kabsa

Ila baada ya kuja hapa JF kueleza changamoto zangu kuna ndgu 1 alisave sana sana, haikuwa connection ya kazi ila alinipa pesa ndefu sana kwa maisha yangu, cha ajabu hata simjui na yeye hanijui ila mpka leo nimekuwa nikiwasiliana nae sana.

Hili jukwaa ni la manufaa sana, Usikubali kuchukua maamuzi magumu pasipo kushitaki JF
 
Kweli Kabisa, hata mimi hapo kanishangaza sana, magari yote hayo kwenye nyumba ya kupanga ya nini?
 
Pole sana Sodoku nimemaliza kusoma lakini nimeumia sana. Kuna mambo unaweza pitia magumu hadi ukatamani kumwona Mungu uongee nae. Ila unakuta pia nyakati kama hizi ndizo zinatujenga

Pamoja na yote hayo nikuombe usiache kumwomba Mungu sana, Mwite Mungu ongea nae, muulize na umwambie bila kuchoka.
Kuna mambo mengi sana duniani, mengi na magumu ambayo kwa macho yetu hatuyaoni wala kwa akili zetu hatuwezi ila Mungu anayo majibu.
 
Dah....hongera sana chifu...angalau umehitimu robo ya mafunzo ya Dunia...wengi wetu humu ni mbumbumbu wa maisha..hatujui chochote...angalau wewe umepata bahati ya ufunuo ukiwa bado na nguvu za mwili na akili...wengi humu hatujui tunaambatana na watu wa aina gani katika maisha...kukata tamaa ni mwiko...utasimama tu tena...kwa jasho na damu...na siku ukisimama vizuri usisahau kumshukuru house maid.. wakati mwingine maisha yasipokuwa na changamoto huwa hayanogi [emoji2960]
 
Pole sana Ndugu ila shukuru ata wewe umeweza kufanya kazi miaka yote hiyo mpaka kufikia kumiliki magari matatu kuna wenzako huku kitaa ata baisikeli tunaitazama machoni tu na bado tunaendeleza mapambano shukuru kwa kila jambo.
 
Pole Sana nnjoo wahtsap au sms za kawaida najuwa sina kikubwa ila dah acha tushikane mikono 0672565139
 
Pole ndugu.
Kamwe usiwaze kujiua,hii sio uvumbuzi wa tatizo lako.Mungu aliyeruhusu kuwa hai bado anamakusudi na wewe.Jitie nguvu na matumaini kwamba Mungu atakufanyia wepesi na ukumbuke kuna wengi wanapitia hali ngumu zaidi ya unayopitia.Jitahidi sana kipindi hiki usiwe na uchungu na mkeo/rafiki/ndugu aliyekutenga.Ukibeba uchungu wowote moyoni milango ya upenyo wako inaweza kuchelewa.Usisahau pia kujisamehe na usiwe na uchungu kutokana na makosa yako.

Katika mapito yote Mungu hajawahi kushindwa,hata mimi nilishapitia nyakati ngumusana sikukubali kukata tamaa na MUNGU ALIYENIUMBA NA KUNILETA DUNIANI KWA KUSUDI ALIFANYA NJIA NIKAPATA MPENYO.

Kumbuka nyakati ngumu hazidumu ILA watu madhubuti hudumu.Chagua kuwa mtu madhubuti.
 
Yanasadifu yaliyotokea kwa wale covid 19

Wanawake hawana uvumilivu kabisa .

Wakati wa majaribu hukimbia haraka sana
 
kwanini usitumie elimu yako kujiajiri?

kwa kuwa mil. 6 ambayo ulimpa mkeo kwa ajili ya biashara ikateketea(siyo msimamizi mzuri wa biashara)hivyo uza tena hiyo gari ulionayo ili upate mtaji wa kuanzisha biashara yako kwa kuisimamia mwenyewe.
Mkuu hawezi uza Gari

Ana tatizo la mguu hatakiwi kusimama mda mrefu au kutembea mda mrefu
 
Ulikuwa huishi na mke, ulikuwa unaishi na shetani hukulijua tu.

Pole sana mguu, ndio maisha hayo, pande zote mbili zetu, kila hatua ni somo, pambana, aliyekupa kisha akakupora, anaweza kukupa tena, mitihani tu hiyo.. Pambana lakini usiache kuamini katika kudra zake.
 
Kuna dogo mmoja ametoka huko usukumani juzi Kati kapitia hapa kwetu tumempa Chanel ya kuishi dar

Kwa Sasa anachukua nguo za mtumba pale soko la ilala asubuhi sana sasa 11 anachagua nguo zake kama ishirini hivi zile nzuri

Anarudi home anazipekeka kwa fundi zinareebishwa anazifua na kupipgwa pasi

Dogo Yuko kariakoo anaziuza Kati buku 8-12 na mtaji wake Ni buku 25 tu .

Amepanga chumba kigamboni anajitegemea 100%

Ukitoa aibu na Soni macho mwako mkeo atarudi kesho kutwa

Sio lazima ufanye kazi ulisomea narudi Tena sio lazima ufanye kazi ulisomea kikubwa hela unapata au hupati haijalishi umeipata kwenye AC au juani .

Format ubongo uanze kuona dunia ingine inavyokwenda nje ya ajira rasmj

Huna sababu yoyote ya kujitoa uhai .
 
Polee Sana ndugu, Mungu azidi kukupigania ajira na afya pia!!

Nakuombea mapito yako yawe ya heri December hii!!

Lakini usiruhusu wazo la kujiua likachukua nafasi, jaribu kufikiria ujiua utaumiza wa ngapi?
 
huu ni UTOPOLO MWINGINE,jamaa kashaseme hivi vitu vyote vimemkuta tu hakutegemea na kajitahidi kuweka sawa ikashindikana sasa wewe unaanza kumuhesabia hivyo vigari ashauza na nyumba sijui kila kitu kapoteza vya nini,NYIE NDO WATU MNA MATUMBO MAKUBWA HUKU AKILI YENU ROBO KILO HAIFIKI
 
Mkuu,nakuombea ufanikiwe kumtafutia kazi huyu ndugu yetu.

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…