Huwa najiambia mwenyewe hili limeachiliwa lije kwangu ,lakini najua Mungu ataachilia na uwezo wa kulishinda pia, usiache kumtegemea Mungu, Huwa naamini Kuna wakati nilitakiwa kufa ,ni miaka kama ishirini Sasa , ila kwa imani kubwa sikufa,
Sikufariji kwa maneno yangu ,ila niamini ninalokwambia,ukiwa na matatizo na ukakata tamaa kwa Mungu,(yaani ukaweka pembeni utashi na ufahamu wako wote pembeni na kumwambia Mungu am all yours, kama umeamua nife sawa,ila Mimi Bado nataka kuishi kwa sababu A,B,C na nk, hivo nakutegemea) ,yeye hujidhihilisha zaidi kuliko wakati wowote ule , Jenga utaratibu wa kulalamika kwa Mungu kama vile unavolalamika kwa mpenzi wako au rafiki Yako, hakikisha unakuwa pekeyako, maana waja wakikuona watasema Tayari king'amuzi kimeyumba,. ,. Pia jifunze kushukuru Kila siku ukiamka ukajikuta Bado upo mzima,kwenye kushukuru Kuna nguvu sana sana, it sounds as if unaomba sababu ya kuishi Tena,
Mungu akutie Nuru pamoja na nguvu ,ukazidi katika afya, Mimi nakuombea heri rafiki yangu