Nahisi mama mkwe wangu ni vampire

Nahisi mama mkwe wangu ni vampire

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Nimekuja ukweni kuwaleta watoto baada ya kufunga shule Ijumaa ya juzi, waje kwa Bibi yao, Babu yao alishatangulia mbele ya haki.

Hapa mama mkwe anaishi na watoto wake wawili wa kike ambao nao Wana watoto, hivyo basi mama mkwe anaishi na wajukuu zake pia.

Kuna kitu kiko very weird nimekiona. Mama mkwe ni mkali sana, ana hasira sana, akianza kupiga, hasira hazimuishi mpaka amuume na amtoe damu huyo anayempiga ndipo hutulia.

Jana nilipofika, mtoto wa nyumba jirani alikuja kuchota maji hapa, akaondoka akaacha maji yanatiririka bombani, mama mkwe akafoka sana kwa hasira na ukali wa juu.

Akaenda kwenye nyumba jirani akakavuta hako katoto, kakapiga sana kisha akakauma Sana mpaka damu zikamtoka, hakika kamjeruhi mtoto wa watu. Wenye mtoto wamepeka malalamiko serikali ya mtaa kesho kaitwa ofisini akajieleze.

Juzi jumapili mjukuu wake wa form 2 ambaye ni mtoto wa shemeji yangu kasahau biblia Kanisani kwa bahati mbaya, kapigwa Sana, Kisha akamuuma begani, kamuachia kidonda kikubwa Sana.

Nasikia ni kawaida yake kuonja damu kidogo, huwa anajikata kidogo apate damu. Hata akipika nyama anatenga ya kwake anataka iwe haijaiva, iwe nyekundu ndani.

Nilikuwa nimepanga tukae Hadi X mas, lakini kwa haya ninayoyaona, asije pandikiza hayo maroho kwa wanangu, kesho naanza maandalizi ya kurudi.

Je, hivi hili nyie wenzangu mnalionaje?
 
Hawa wazee wetu wana mengi moyoni, hatujui kwanini hawayaweki wazi wakapata msaada.

Hilo la damu ni tatizo. Kuna demu tulisoma naye high school, alikuwa na kesi za kung'ata watu.

Malalamiko yakawa mengi hadi walimu wakamwita, akajitetea kwamba anajikuta tu kauma mtu na tayari damu zinatoka. Hata akikung'ata kidogo tu, lazima utoke damu.

Halafu demu mwenyewe mkali kwelikweli
 
Duuh...hilo sasa balaa. Timua vumbi aisee usije ukawa vampire na wewe
 
Jana nilipofika, mtoto wa nyumba jirani alikuja kuchota maji hapa, akaondoka akaacha maji yanatiririka bombani, mama mkwe akafoka sana kwa hasira na ukali wa juu.

Akaenda kwenye nyumba jirani akakavuta hako katoto, kakapiga sana kisha akakauma Sana mpaka damu zikamtoka, hakika kamjeruhi mtoto was watu. Wenye mtoto wamepeka malalamiko serikali ya mtaa kesho kaitwa ofisini akajieleze.
Jana ulifika.. Kesho akaitwa.. 😳
 
Back
Top Bottom