Nahisi mshawahi kumuona Nelson Ntombela Raia wa Afrika Kusini kwenye mitandao ya kijamii?

Nahisi mshawahi kumuona Nelson Ntombela Raia wa Afrika Kusini kwenye mitandao ya kijamii?

mahingah

Senior Member
Joined
Oct 4, 2016
Posts
198
Reaction score
275
Bila shaka umekutana sana na picha hii katika mitandao, mfahamu mhusika wa picha hiyo. Nelson ni mkazi wa Kagiso, Krugersdorp nje ya mji wa Johannesburg, amezaliwa April 6, 1987 akiwa ni mtoto wa mwisho kati ya watoto saba.

Nelson amekulia katika mitaa ya wahuni, alikuwa muhuni pia wakati wa utoto mpaka akiwa mtu mzima, mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 16 tu alifungwa katika gereza la watoto kwa makosa ya ukabaji wa kutumia silaha.

Hata akiwa gerezani aliendelea kuwa kiongozi wa makundi ya kihalifu yaliyokuwepo kwa siri gerezani, alikutana na makundi mengine ya kihalifu na akawa kiongozi wao, na hata alipoachiwa miezi kadhaa mbeleni, mtaani kuliendelea kuwa chini ya utawala wa makundi yake kama kawaida, kiufupi alikuwa jambazi.

Nelson aliendelea na ujambazi kwa miaka mingi zaidi hali iliyopelekea mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 26 kukamatwa tena na kufungwa gerezani miaka mitatu baada ya kupatikana na hatia ya kubomoa nyumba na kupora mali.

Mwaka 2014 akiwa jela mama yake mzazi alifariki, likawa pigo kubwa sana kwake na hii ilimsaidia kujiapiza kuwa ataachana kabisa na ujambazi na kuishi maisha ya amani atakaporudi uraiani.

Baada ya kutoka jela akaanza kujihusisha na kuigiza filamu akitumia jina la Chicken, hili ni jina alilopewa na wanakijiji wa kule alikozaliwa kutokana na tabia yake ya wizi wa kuku wakati akiwa mdogo. Filamu yake ya kwanza kabisa inaitwa Rhythm City (series) iliyoanza kutoka mwaka 2007, yeye aliikutia mwaka 2017 ikiendelea.

Kutoka hapo Nelson alianza kuona mafanikio makubwa katika kuigiza filamu kwani aliendelea kuonekana katika filamu na TV shows nyingi kama Isidingo, Generations: The Legacy na Isithembiso.

IMG_20210113_150611_160.jpg
IMG_20210113_150616_073.jpg
 
Yaani sijaambulia kitu maana sijui ni nani adi iwe habari
Nilitaka kuandika kitu kwenye komenti yako ila nimekumbuka leo nimejiapiza kuwa "sitahukumu wala kulinganisha mazuri kwa mabaya kawa siku nzima ya leo!
 
Back
Top Bottom