mimi mtakatifu
JF-Expert Member
- Oct 11, 2019
- 248
- 539
Nimefikisha mwaka tangu nipoteze ajira baada ya kuingia COVID-19.
Kwa sasa nipo mtaani kwa muda mrefu sina shughuli yoyote ya kufanya sababu nilikuwa ni mtu naeishi maisha ya ku-dedicate muda wangu na nguvu zangu kwenye kazi za ofisi.
Sikuwai kuwaza kama kuna siku naweza kukaa bila kupata ajira kwa muda wote huu. Nimeishi miaka mingi ya kuajiriwa na kuna kazi nilikuwa natafutwa bila kuomba.
Leo hii nafanya application hata interview siitwi na nikiitwa sipati feedback. Imefika wakati nikiingia kwenye interview natetemeka nakuwa muoga nashindwa kujibu.
Kifupi maisha yangu yamebadilika yamekuwa magumu sana. Kula imekuwa ya shida na sasa hata kodi nimeshindwa kulipa naishi maisha ya kumkwepa mwenye nyumba.
Kuna kipindi nilikuwa nimeingia kwenye ulevi wa kupindukia nikijaribu kuitafuta relief ya maisha. Afya ilidhoofu majanga yakawa mengi nashukuru nilipata rafiki yangu mmoja alinitoa huko japo mara moja moja uwa narudi kwenye ulevi na kutoka.
Sasa hivi nahisi nimeanza kupata kitu kama kichaa nna hali sio ya kawaida. Naskia hasira kali sana muda wote, nasahau vitu kwa haraka mpaka watu nawasahu kibaya zaidi napata tatizo la ganzi kwenye mwili nikiwa kwenye mawazo. Siwezi kufikiria vizuri mimi ni mwandishi mzuri ila kwa sasa hata uwezo wangu wa drafting umeshuka sana.
Yani nimekuwa naishi kama kasha flani lisilo na kitu.Natafuta unafuu na amani lakini nimeshindwa kuipata kwenye pombe na strehe, kwenye wanawake hata ibadani siipati amani rohoni kwangu.
Kuna muda nataman kama nisiwepo kabisa duniani nisione mateso zaidi yanayokuja mbele yangu.
I am so scared. I cry almost every night pamoja na uanaume wangu na sijui nafanyeje.
Dah naomba Mungu anisaidie nafsi yangu ipone sipo sawa kabisa.