U wapi utakatifu wako?
I wapi imani yako kwa Mungu wako?
Mbona hukumbuki la kukuweka hai mpaka sasa? Huna kesi polisi, wala huko kwenye kitanda cha hospital
Una simu janja, una bando na una muda wa kuingia JF kuandika haya! Unapaswa kumshukuru Mungu pakubwa mno...
Kuna wengine hawana hata uwezo wa kumiliki smartphone
Kuna wengine hawana hata pa kulala.wako kwenye korido za watu wanapigwa baridi..
Kuna wengine muda huu wameshauza kila kitu hana cha kuuza tena
Kuna wengine wananuka madeni na hawakopesheki tena
Kuna wengine kesho vyombo vinatolewa nje kodi wameshindwa kulipa
Kuna wengine wanauguliwa na ndani hawana senti tano...Nknk
Shida inapokukamata wakumbuke na hawa kisha Mshukuru Mungu sana
Imagine umemaliza mwaka bila kazi na bado upo hai..mzima wa afya.. Hili pekee ni kubwa sana!
Usijione mnyonge
Usikate tamaa
Usipoteze tumaini
Mungu hatakupa jaribu kukuzidi, Mungu hatafunga milango yote, kuna mmoja utakuwa wazi ..Kumbuka hata usiku uwe mrefu kiasi gani kutapambazuka...!
Mungu katika Biblia Takatifu anatuasa tusiogope..na hili neno USIOGOPE limerudiwa mara 365 kwenye Bible! Tafsiri yake ninini? Hupswi kuogopa hata siku moja maana yeye yu pamoja nawe...!
Bado una nafasi ya pa kuweka mgongo upumzike
Bado una nafasi ya kuweza kuandika hata hii mada
Back una nafasi ya kuweza kupata chochote cha kutia kinywani bila shida
Bado una nafasi ya kuweza kuoga na kubadili nguo..Mshukuru sana Mungu
Kama huumwi
Kama huna kesi
Kama after iko vizuri
Kama akili iko sawa ... Tayari una mtaji mkubwa sana wa kuendelea na mapambano... Mshukuru Mungu kwa hilo...
Don't give up for in the darkest hours of time there is always a twinkle of light to lead you through...!
Nimeamua kuandika hii mada kama nilivyoahidi baada ya kusoma hapa JF kuwa Lulu binti aliyepitia mitihani mingi katika maisha yake ya usichana anakaribia kuolewa! Nikasema inawezekana miaka ya uharibifu imekwisha! Kuna neno linasema.... Natazama kutakuwako miaka saba ya neema na miaka saba ya...
www.jamiiforums.com