Nahisi ndoa yangu inaelekea ukingoni kutokana na tatizo la nguvu za kiume

Nahisi ndoa yangu inaelekea ukingoni kutokana na tatizo la nguvu za kiume

kinachokutesa ni saikolojia ya tendo lenyewe, unapanik sana kuhusu madhaifu yako so unazidi kuharibika kiutendaji siku hadi siku. tafuta mtaalamu wa saikolojia akurekebishe, ongea na mkeo vizuri kuhusu hilo tatizo ili awe anaenda na ww ado ado. Hii inaweza kuwa ni njia moja ya kutatua hilo jambo. kama unahitaji maelezo zaidi uliza tu.
Yaani tena anavyodhani kuwa ndoa itavunjika ndio kabisa anazidisha kumbe hana udhaifu wowote. Huyu jamaa anahitaji msaada tu wa kisaikolojia basi, anapona
 
Karibu sana cheza fresh na mkeo atakutibu kwa asilimia mia. huyo ndo uwanja wako wa kujaribia na kuvuka hilo tatizo. usifanye chochote kama hayuko fresh siku hiyo ili asikuvunje moyo. siku akiwa fresh na mnaelewana fanya nilivyokwambia utaona hatua kubwa siku hadi siku mpaka kupona kabisa.
Chief Mwenyezi Mungu akubariki Sana yaani! Nimekupata vyema kabisa,kuna jamaa yangu ktk kutafuta ushauri aliniambia mke wake alikuwa bega Kwa bega na yeye ktk kutatua hili tatizo,bahati mbaya mimi mke wangu kuna muda tunakuwa pamoja kuna muda ana panick Sana full misengenyo Ila all in all ni muelewa acha nikae nae chini nilifanye hili zoezi pia.Shukran Sana mkuu
 
yan tena anavyodhani kuwa ndoa itavunjika ndio kabisa anazidisha kumbe hana udhaifu wowote. huyu jamaa anahitaji msaada tu wa kisaikolojia basi, anapona
Nimepata kitu hapa,nashukuru Sana acha nifanyie kazi hili pia
 
keypass, Oga tu kila baada ya tendo, hii itakusaidia kurudi katika hali ya kawaida, na kuanza upya kazi.
Acha kupiga nyeto
Acha kuangalia video x
Acha kuangalia video za uchi uchi hasa hizi zenye kuonyesha maumbo ya wanawake.

Tendo la ndoa ni feeling tu, ukianza kupoteza feeling kwa mwenza, Ndio hupelekea hali hiyo.

Vyakula:
Kula supu ya pweza
Kongoro
Juice ya maziwa na tende.

Dawa nyingine ni kuua nguvu tu
 
karibu sana cheza fresh na mkeo atakutibu kwa asilimia mia. huyo ndo uwanja wako wa kujaribia na kuvuka hilo tatizo. usifanye chochote kama hayuko fresh siku hiyo ili asikuvunje moyo. siku akiwa fresh na mnaelewana fanya nilivyokwambia utaona hatua kubwa siku hadi siku mpaka kupona kabisa.
Sawa mkuu acha niyazingatie haya hakika naamini yatanisaidia
 
Kuna mdau huku nilimpa supplement (korean red ginseng) kaniambia inamsaidia sana fanya kuingia mtandaoni ebay/alibaba uagize mkuu, kwanza wewe kuhisi tu una tatizo tayari ni tatizo maana unaingia kitandani ukiwaza leo nitaweza kweli, matokeo yake ndio kama hivyo unafeli tena
 
Mkuu tendo la ndoa huongozwa na hisia. Naamini tatizo halitokuisha kama utaendelea kujiona dhaifu mbele ya mkeo.

Mosi jipe muda wa kutosha wa kumuandaa mkeo, Usiwe na mawazo hasi kuhusu hali yako.
Fanya mazoezi kweli maana isije kuwa unachezacheza ukasema unafanya mazoezi.

Ni vyema wa wakati wa tendo lenyewe ukawa unafikiria vitu vingine kabisa hii itasaidis kukufanya uchelewe kukojoa.

Muone Psychologist Akusaidie.
Shukran Sana Kwa ushauri,nitazingatia hili.be blessed
 
wakati upo sawa ulikua na mahusiano na mke wako huyo au ulikua na mwanamke mwingine?
Mkuu umewaza nilichokua nakifikiria akilini mwangu,,tatizo limeanza baada ya kuoa,,ina maana kabla ya kuoa hajawah ku experience hiyo shida...kuna bint wengine wakiingia kwenye mahusiano (hasahasa wale waliopewa ahadi ya kuolewa) then kwa sabab yoyote ile mkaachana hua wanawafanyia vitu vya kukukomesha ili ndoa yako iyumbe hata kupelekea kuvunjika...jpo sio wote ila wapo wanaofanya haya mambo..
 
Daah kuna mdau huku nilimpa supplement (korean red ginseng) kaniambia inamsaidia sana fanya kuingia mtandaoni ebay/alibaba uagize mkuu, kwanza wewe kuhisi tuu unatatizo tayari ni tatizo maana unaingia kitandani ukiwaza leo nitaweza kweli, matokeo yake ndio kama ivyo unafeli tena
Na kweli huwa najiuliza Sana Hilo suala kama nitaweza au la,Acha nijitahidi kutoa hayo mawazo hasi
 
keypass, Pole sana mkuu kwa tatizo ambalo unahisi ni kubwa sana katika maisha yako.

Mkuu pili nikupongeze kwa huruma ambayo imekuingia kwa mkeo nakuona kwamba humridhisi kama ambayo umenukuu.

Lakini tatu nakuhakikishia kwamba wewe ni mzima zana kiafya (usishangae) una nguvu safi tu za kiume wala huna tatizo lolote katika afya yako.

Ila tu nadhani utakuwa unakutana na hali zifuatazo.

1. Kwanza ulipoanza siku ya kwanza na mkeo hukuenda mbio ndefu na hapo ukaanza kujihisi kwamba una tatizo kumbe ni kawaida kwetu wanaume na hali hiyo ikaanza kukutia hofu.

2. Wewe hujakaa na mkeo mkajadili juu ya hilo jambo ambalo linakukumba. Kosa kubwa tunafanya wanaume ni kwamba kwa matatizo madogo kama haya hasa ya nguvu za kiume hatushei na kuwambia wake zetu kwamba hili suala liko hivi na vile.

Tunachofanya ni kujaribu kutatua wenyewe bila wife kujua yaani tunataka na tunatarajia au wewe unatarajia kwamba siku moja wife umpigie show kali saana mpaka aone kwamba kumbe hukuwa na tatizo sasa hiyo haitokuja kutokea kamwe. Lazima ukae na mkeo.

Ukikaa na mkeo utapata faida zifuatazo:

Kwanza utakuwa huru pale unapokuwa nae mana hautakuwa na la kuhofia kwa sababu kama tatzo lako ameshalijua tayari sasa wala hautakuwa na shida ya kutaka kujikakamua na kuanza kufikiria "Sijui nitakojoa mapemaa,atanionaje ikitokea na leo?" hapo tendo la ndoa lazima umalize mapema tu,tendo la ndoa linataka akili iliyochangamka.

Mwambie mkeo kistaarabu na utashangaa ambavyo atakutia moyo na kuanzia hapo utakuwa umeutua mzigo.

3. Wewe unachodhani ni kwamba eti ukimaliza round ya mwanzo basi unadhani kwamba kidume ataunga na la pili kabisa wakati kumbe lazima kuwe na muda kwa mwanaume na hayo ndio maumbile wala usipingane nayo.

Kikawaida mwanaume mshindo wa kwanza unawahi.

4. Huenda mkeo ni wale ambao ukishakojowa yeyye ndo basi tena hana la kufanya yaani kila kitu anakuachia wewe ufanye na kama staili ni moja tuuu mpaka mwisho.hapa inahitaji kukaa na mkeo muelimishane vizuri tena kistaarabu na kihisia sio mnaongea juu juu tu.

Lakini nataka nikuambie kwamba kama una mficha mkeo hilo tatizo huku ukitaka siku moja yatokee maajabu,basi jua mkeo anachodhani kwamba wewe humjali au unamfanyia kiburi juu ya hilo hali au unamkomoa.

Ila ukikaa naye chini ukamuelezea basi na yeye ataona kwamba Kumbe mume naye hapendi na anaona huruma.Hapo ataondoa dhana mbaya kwako.

Mkuu hilo tatizo sio wewe wa kwanza.kwa kufupisha.

-Kaa na mkeo mzungumze,sio ukimaliza unakuwa bubu na kuanza kujawazia kichwani na kukata tamaa.
-usitumie viagra,baki katika asili,mapenzi hayana maigizo.
-kuwa romantic na mzowee sana mkeo mpaka ifikie hatua una mpa zile stori zako unazohisi ni za aibu kama hiyo.
-kumbuka kwamba kinachokumaliza ni hofu ya kutaka mkeo asijue tatizo lako lakini ameshajua na hapo ni kumfungukia.

Ukimfungukia utakuwa huru ukiwa naye na hapo penzi litanoga sana na utafungua moyo bila dawa yeyote ile.

Ndoa tamu mkiwa wawazi baina yenu.
 
Hiki kitu nimeulizwa na wengi,sijawahi ahidi kumuoa mtu yoyote zaidi ya mke wangu,Ila cha kushangaza kuna baadhi ya marafiki wa kike baada ya kuoa tu wao wakaanza kunichukia.
Yawezekana walikuchukia kwa sababu matarajio yao ilikuwa waolewe na wewe,japo hukuwahi kuwatamkia kama ulivyokwisha sema.
 
Hapana before nilikuwa sawa, enzi za boys nyeto zilihusika sana lakin niliacha na nikahisi kuna tatizo but baadae nikawa sawa bao tatu zikawa kawaida Ila baada ya kufunga ndoa ndio mambo yakuwa lukumba lukumba
Wewe shida ni saikolojia. Yaani kuna siku ya kwanza ulikosea, bila shaka ukapata uoga kwamba mke atakuonaje. Labda mke alionyesha dalili ya kutokuelewa, labda aliguna au kusonya na kila ukianza mechi anakutisha na maneno kama usiniangushe kama jana. Wewe tulia pia mwambie mkeo asikubeze akupe moyo mambo yatakaa vizuri
 
Back
Top Bottom