keypass, Pole sana mkuu kwa tatizo ambalo unahisi ni kubwa sana katika maisha yako.
Mkuu pili nikupongeze kwa huruma ambayo imekuingia kwa mkeo nakuona kwamba humridhisi kama ambayo umenukuu.
Lakini tatu nakuhakikishia kwamba wewe ni mzima zana kiafya (usishangae) una nguvu safi tu za kiume wala huna tatizo lolote katika afya yako.
Ila tu nadhani utakuwa unakutana na hali zifuatazo.
1. Kwanza ulipoanza siku ya kwanza na mkeo hukuenda mbio ndefu na hapo ukaanza kujihisi kwamba una tatizo kumbe ni kawaida kwetu wanaume na hali hiyo ikaanza kukutia hofu.
2. Wewe hujakaa na mkeo mkajadili juu ya hilo jambo ambalo linakukumba. Kosa kubwa tunafanya wanaume ni kwamba kwa matatizo madogo kama haya hasa ya nguvu za kiume hatushei na kuwambia wake zetu kwamba hili suala liko hivi na vile.
Tunachofanya ni kujaribu kutatua wenyewe bila wife kujua yaani tunataka na tunatarajia au wewe unatarajia kwamba siku moja wife umpigie show kali saana mpaka aone kwamba kumbe hukuwa na tatizo sasa hiyo haitokuja kutokea kamwe. Lazima ukae na mkeo.
Ukikaa na mkeo utapata faida zifuatazo:
Kwanza utakuwa huru pale unapokuwa nae mana hautakuwa na la kuhofia kwa sababu kama tatzo lako ameshalijua tayari sasa wala hautakuwa na shida ya kutaka kujikakamua na kuanza kufikiria "Sijui nitakojoa mapemaa,atanionaje ikitokea na leo?" hapo tendo la ndoa lazima umalize mapema tu,tendo la ndoa linataka akili iliyochangamka.
Mwambie mkeo kistaarabu na utashangaa ambavyo atakutia moyo na kuanzia hapo utakuwa umeutua mzigo.
3. Wewe unachodhani ni kwamba eti ukimaliza round ya mwanzo basi unadhani kwamba kidume ataunga na la pili kabisa wakati kumbe lazima kuwe na muda kwa mwanaume na hayo ndio maumbile wala usipingane nayo.
Kikawaida mwanaume mshindo wa kwanza unawahi.
4. Huenda mkeo ni wale ambao ukishakojowa yeyye ndo basi tena hana la kufanya yaani kila kitu anakuachia wewe ufanye na kama staili ni moja tuuu mpaka mwisho.hapa inahitaji kukaa na mkeo muelimishane vizuri tena kistaarabu na kihisia sio mnaongea juu juu tu.
Lakini nataka nikuambie kwamba kama una mficha mkeo hilo tatizo huku ukitaka siku moja yatokee maajabu,basi jua mkeo anachodhani kwamba wewe humjali au unamfanyia kiburi juu ya hilo hali au unamkomoa.
Ila ukikaa naye chini ukamuelezea basi na yeye ataona kwamba Kumbe mume naye hapendi na anaona huruma.Hapo ataondoa dhana mbaya kwako.
Mkuu hilo tatizo sio wewe wa kwanza.kwa kufupisha.
-Kaa na mkeo mzungumze,sio ukimaliza unakuwa bubu na kuanza kujawazia kichwani na kukata tamaa.
-usitumie viagra,baki katika asili,mapenzi hayana maigizo.
-kuwa romantic na mzowee sana mkeo mpaka ifikie hatua una mpa zile stori zako unazohisi ni za aibu kama hiyo.
-kumbuka kwamba kinachokumaliza ni hofu ya kutaka mkeo asijue tatizo lako lakini ameshajua na hapo ni kumfungukia.
Ukimfungukia utakuwa huru ukiwa naye na hapo penzi litanoga sana na utafungua moyo bila dawa yeyote ile.
Ndoa tamu mkiwa wawazi baina yenu.