N:B: Sina uhakika wa asilimia 100 kama niliuziwa chungwa lililoivishwa kikemikali ila kwa dokezo >> hili << nimepata wasiwasi
Nipo Mbeya kwa wiki kadhaa, Nilikuja na mashine yangu ya kusagia juisi ya machungwa, Napenda sana kunywa juisi hii.
Wiki iliyopita nilizinguka soko la soweto nilikuta machungwa mengi yameharibika nikaambiwa msimu ndio unaisha, Ilikuwa ni mida ya saa moja jioni nikaenda soko pale kabwe, machungwa yalikuwa bei sana shilingi 500, nikawa natafuta nafuu nikaona kuna binti anauza machungwa kwa bei rahisi shilingi 300.
Nikafurahi sana nikachukua matano, Nikafika kwenye makazi yangu nikasaga kuandaa juisi bila kutia maji yoyote yani iwe juisi asilimia 100.
Vile nimeshaandaa naanza kuinywa, juisi ilikuwa inanichoma kwenye lips lakini ikifika kwenye ulimi haina shida.
Ilibidi niongeze maji ikawa hainichomi lips.
Leo hii nimeona dokezo kuna mchunguzi huru kaweka ushahidi wa kutosha kwamba kuna kemikali za Calcium Carbide na Etefon 480 zinanunuliwa kwa njia zisizo halali kutoka Zambia zinaletwa Mbeya zinatumika na wafanyabiashara wasio waaminifu kuivisha ndizi na maparachichi, kwa kilichonikuta nimeona itakuwa inatumika mpaka kwenye machungwa.
www.jamiiforums.com

DOKEZO - Mbeya: Kemikali za kuivisha Ndizi zimehamia katika matunda mengine, Wataalam wa Afya watueleze kama ni salama
Habari Wana Jamiiforums wenzangu, ndugu yenu Mwanongwa katika pilika zangu nikakutana na Stori za kwamba kuna Wafanyabiashara wa Ndizi pamoja na Maparachichi ndani ya Mkoa wa Mbeya wamekuwa siyo waaminifu katika biashara hiyo. Kawaida ndizi zinapokomaa huwa zinavunwa na kuvundikwa kwenye sehemu...