Kuna uzushi mwingi kwenye mitandao, parachichi la kienyeji likikaa lenyewe Siku tatu linaiva, Siku tano linaanza kuharibika, dawa za nini, hata ndizi Siku chache zinaiva zenyewe, na ukienda masokoni nyingi zimeharibika na kutupwa kwa kuiva mapema na kukosa soko, kwanini mtu awahishe kuiva ili zioze?
Kuna ka uzushi kanasambazwa makusudi kwa malengo maalumu
Walitoa ripoti kuwa kemikali hizo, hazina madhara kea watumiaji,.., nadhani kwenye moja ya uzi hapa jamii forum walipost barua official kutoka kwenye mamlaka,....😞😞
DOKEZO Wafanyabiashara wa ndizi mbivu Dar huchovya kwenye kemikali ili kuziivisha ndani ya muda mfupi. Afya za watu hatarini nadhani iko kwenye komenti mojawapo humo ndani
Kuna uzushi mwingi kwenye mitandao, parachichi la kienyeji likikaa lenyewe Siku tatu linaiva, Siku tano linaanza kuharibika, dawa za nini, hata ndizi Siku chache zinaiva zenyewe, na ukienda masokoni nyingi zimeharibika na kutupwa kwa kuiva mapema na kukosa soko, kwanini mtu awahishe kuiva ili zioze?
Kuna ka uzushi kanasambazwa makusudi kwa malengo maalumu
Kula kemikali hakukwepeki labda uwe na shamba lako binafsi Kwa ajili Yako na familia Yako.Mfano nyama ya ngombe hapa dar zinazotokea Kanda ya ziwa nyingi zinalishwa ARV Kwa kuamini kuwa zitanenepa,kwenye kuku hapa Dar wanapewa madawa na siku hiyo hiyo anauziwa mteja na kwenye mboga kama mchicha Kwa hapa dar baadhi wanatumia maji ambayo yaliyochanganyika na maji ya kiwandani na watu Wanakula Kwa kuamini ni chakula safi.
Hapo tatizo ni kwamba matunda yanavunwa yakiwa bado hayajakomaa.
Tunda lolote likivunwa kabla ya muda wake,uchelewa kuiva au kuoza kabisa.
Kwahiyo wanaona ni bora kutumia madawa ili yaive haraka.
N:B: Sina uhakika wa asilimia 100 kama niliuziwa chungwa lililoivishwa kikemikali ila kwa dokezo >> hili << nimepata wasiwasi
Nipo Mbeya kwa wiki kadhaa, Nilikuja na mashine yangu ya kusagia juisi ya machungwa, Napenda sana kunywa juisi hii.
Wiki iliyopita nilizinguka soko la soweto nilikuta machungwa mengi yameharibika nikaambiwa msimu ndio unaisha, Ilikuwa ni mida ya saa moja jioni nikaenda soko pale kabwe, machungwa yalikuwa bei sana shilingi 500, nikawa natafuta nafuu nikaona kuna binti anauza machungwa kwa bei rahisi shilingi 300.
Nikafurahi sana nikachukua matano, Nikafika kwenye makazi yangu nikasaga kuandaa juisi bila kutia maji yoyote yani iwe juisi asilimia 100.
Vile nimeshaandaa naanza kuinywa, juisi ilikuwa inanichoma kwenye lips lakini ikifika kwenye ulimi haina shida.
Ilibidi niongeze maji ikawa hainichomi lips.
Leo hii nimeona dokezo kuna mchunguzi huru kaweka ushahidi wa kutosha kwamba kuna kemikali za Calcium Carbide na Etefon 480 zinanunuliwa kwa njia zisizo halali kutoka Zambia zinaletwa Mbeya zinatumika na wafanyabiashara wasio waaminifu kuivisha ndizi na maparachichi, kwa kilichonikuta nimeona itakuwa inatumika mpaka kwenye machungwa.
Habari Wana Jamiiforums wenzangu, ndugu yenu Mwanongwa katika pilika zangu nikakutana na Stori za kwamba kuna Wafanyabiashara wa Ndizi pamoja na Maparachichi ndani ya Mkoa wa Mbeya wamekuwa siyo waaminifu katika biashara hiyo. Kawaida ndizi zinapokomaa huwa zinavunwa na kuvundikwa kwenye sehemu...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.