Nahisi niliuziwa machungwa yaliyoivishwa kwa kekimikali zilizoanza kutumika Mbeya kuivisha matunda, Mungu atusaidie lakini Idara zetu zimelala mno

Mimi nashindwa kuelewa , kwani Tunda kama parachichi , likikaa lenyewe si Lina iva TU

Sasa kuna haja gani ya kuingia gharana kununua kemikali Kwa ajili ya kuivisha.

Naomba muongozo, sijaelewa kabisa
Kuna uzushi mwingi kwenye mitandao, parachichi la kienyeji likikaa lenyewe Siku tatu linaiva, Siku tano linaanza kuharibika, dawa za nini, hata ndizi Siku chache zinaiva zenyewe, na ukienda masokoni nyingi zimeharibika na kutupwa kwa kuiva mapema na kukosa soko, kwanini mtu awahishe kuiva ili zioze?

Kuna ka uzushi kanasambazwa makusudi kwa malengo maalumu
 
Mimi nashindwa kuelewa , kwani Tunda kama parachichi , likikaa lenyewe si Lina iva TU

Sasa kuna haja gani ya kuingia gharana kununua kemikali Kwa ajili ya kuivisha.

Naomba muongozo, sijaelewa kabisa
Yaani mtu akae tuuu anasubiri hadi litakavyotaka lenyewe kuiva amesubiri tu?

Kwanza sio tu kuiva, kemikali ni kuanzia mbegu hadi viuwatilifu.
 
Watu wanataka yaive haraka, wapige pesa haraka.
Sasa kama ili yaive kwa haraka si yataharibika kwa haraka pia, maana inabidi uwe na wateja wa kuyanunua matunda yalioiva yote,

Au yaki ivishwa na kemikali Yana kaa week 2 bila kuharibika, ?
 
Walitoa ripoti kuwa kemikali hizo, hazina madhara kea watumiaji,.., nadhani kwenye moja ya uzi hapa jamii forum walipost barua official kutoka kwenye mamlaka,....😞😞
Hata kama hazina madhara that is not our standard.

Kama utanisaidia link ya huo uzi nitashukuru
 
Hata kama hazina madhara that is not our standard.

Kama utanisaidia link ya huo uzi nitashukuru
DOKEZO Wafanyabiashara wa ndizi mbivu Dar huchovya kwenye kemikali ili kuziivisha ndani ya muda mfupi. Afya za watu hatarini nadhani iko kwenye komenti mojawapo humo ndani
 
Itakuwa Wana nia mbaya ya kuharibu reputation ya wauza matunda,

Biashara ya kuuza matunda inaitwa ni mali kuoza,
Sasa ndio watumie kemikali ili matunda yawai kuiva ili iweje.

Yan haingii akilini kabisa
 
Kula kemikali hakukwepeki labda uwe na shamba lako binafsi Kwa ajili Yako na familia Yako.Mfano nyama ya ngombe hapa dar zinazotokea Kanda ya ziwa nyingi zinalishwa ARV Kwa kuamini kuwa zitanenepa,kwenye kuku hapa Dar wanapewa madawa na siku hiyo hiyo anauziwa mteja na kwenye mboga kama mchicha Kwa hapa dar baadhi wanatumia maji ambayo yaliyochanganyika na maji ya kiwandani na watu Wanakula Kwa kuamini ni chakula safi.
 
Sasa mbona matunda sokoni yanatupwa kwa sababu yameoza,

Na mengine yakishushwa kwenye fuso palepale TU, baadhi yanakuwa tayari yameoza.

Sasa ndio watumie kemikali kuivisha matunda, haingii akilini kabisa πŸ˜‚
 
Watu wanataka yaive haraka, wapige pesa haraka.
Sasa mbona wauza matunda wengi TU mitaji Yao imekata kwa matunda kuoza,
Kwa hiyo kilicho waponza ni kutumia kemikali.

Labda ungeniambia hiyo kemikali ni kwa ajili ya matunda ya sioze hapo ningewaelewa kidogo
 
Hapo tatizo ni kwamba matunda yanavunwa yakiwa bado hayajakomaa.
Tunda lolote likivunwa kabla ya muda wake,uchelewa kuiva au kuoza kabisa.
Kwahiyo wanaona ni bora kutumia madawa ili yaive haraka.
Sasa mbona matunda sokoni yanatupwa kwa sababu yameoza,

Na mengine yakishushwa kwenye fuso palepale TU, baadhi yanakuwa tayari yameoza.

Sasa ndio watumie kemikali kuivisha matunda, haingii akilini kabisa πŸ˜‚
 
Hatari sana serikali ichukue hatua mapema
 
Mimi nashindwa kuelewa , kwani Tunda kama parachichi , likikaa lenyewe si Lina iva TU

Sasa kuna haja gani ya kuingia gharana kununua kemikali Kwa ajili ya kuivisha.

Naomba muongozo, sijaelewa kabisa
Inashangaza sana hata embe siku hizi kulipata lililokomalia mtini ni bahati,afya lazima zitetereke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…