Nahisi nimekuwa mlevi wa Coffee, natamani kuacha

Chakorii

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
18,773
Reaction score
51,429
Habari ya jioni wana JF. Mko salama jamani?😊

Ninaimani kichwa cha habari kinajieleza vyema.

Yes! natamani sana kuacha kunywa coffee hususani espresso.

na

cappuccino.

Nisipokunywa Kwa asilimia 60 siku yangu inakuwa ya hivyo sana🥲

Nifanye nini ili niweze kuacha kunywa?

Kama kuna mtu yeyote humu ndani ana changamoto ambayo anahitaji utatuzi (msaada) tafadhali drop your comment hapa unaweza pata msaada.

Si ndio jamani ee💃💃💃💃💃
Ehee🧚‍♀️🧚‍♀️🧚‍♀️
 
mkuu hutaki kuishi miaka mingi embu pitia hapa hivi. ..

BBC walishawai kuandika makala moja hivi kuwa wanywa kahawa huishi miaka mingi link hii hapa

 
pia makala hii....



nimalize kwa kusemaa jaribu kutafuta replacement ya kahawaa.. yan upunguze kunywa kahawa uanze kula chocolate... kupunguza addiction
 
Mimi nilikuwa natengeneza viungo vya chai mwenyew Huwa naweka tangawiz na pilipil manga kidogo sahiz naona hali mbaya natumia pilipili manga nyingi na tangawiz kwenye chai Yani chai had iniwashe hasa ndo najielewa
Hiv Haina madhara kiafya?
 
Sijaelewa ulichoandika chief
Unakunywa kiasi gani kwa siku au mara ngapi? Bila shaka wewe siyo mnywaji sugu kama unavyodhani. Kuna nchi inaitwa Finland nenda uone jinsi watu wanavyokunywa kahawa! Kuanzia asubuhi mpaka jioni kila siku. Tena siyo instant coffee bali ile iliyokaangwa na kusagwa. Na ni moja ya nchi zenye watu wanaoishi maisha marefu. Kwa ujumla ni kuwa kahawa haina madhara. Labda kama unachanganya na sukari nyingi! Jaribu kunywa kavukavu na utakuja kuona kahawa bila sukari ni nzuri kuliko yenye sukari.
 
Anko anza tiba ya maji na ndimu ama changanya na asali kidogo
 
Mimi nilikuwa natengeneza viungo vya chai mwenyew Huwa naweka tangawiz na pilipil manga kidogo sahiz naona hali mbaya natumia pilipili manga nyingi na tangawiz kwenye chai Yani chai had iniwashe hasa ndo najielewa
Hiv Haina madhara kiafya?
Sijawahi kusikia kuwa vina madhara, tangawizi au pilipili manga. Zaidi nimesikia wanasema ni vizuri kwa afya. Ni Bongo tu pilipili manga haitumiki kwa wingi lakini nchi za Asia na hata Ulaya, pilipili manga inatumika sana kwenye kupikia na ku-marinate nyama.
 
Angalia mazingira ya Finland then uje ufute ulichoandika

Sent from my LND-L29 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…