Nahisi sijui chochote kuhusu mahusiano ya kupenda ama kupendwa

Nahisi sijui chochote kuhusu mahusiano ya kupenda ama kupendwa

Roshii

Member
Joined
Apr 19, 2025
Posts
34
Reaction score
56
Habari za wakati huu wana jf
Nimeona bora kuwa mkweli uenda nikapata mitizamo itakayo nijenga juu ya swala hili zima la mahusiano ya kimapenzi..

nina umri wa miaka 30 , mpaka namaliza elimu ya diploma ya uandisi wa ujenzi , sijawahi kuwa na mahusino ya kimapenzi kabisaa. na sikuhitaji kabisa kujihusisha na mahusiano ya karibu na jinsia ya kike

ila Kwa sasa ninaona kabisaaa..Mawazo yamezamaaa kuwahitajia angalau hata kuwa na ukaribu nao..

nakijaribu namna yakuweka ukaribu nao wengi wao hawako interested, bali wako interested na maslahi yao.

Kuna wakati ambao nashindwa kabisaa kufanya kazi!
Wakati mwingine nakosa usingizi nyakati za usiku..!
Nyakati zingine najikuta kama akili zimepoteaa

wale wabobevu wa haya mambo karibu, kwa ushauri
 
Ukisema usikilize comment za watu humu utakata tamaa wengi humu Wana wake zao na waume zao kwenye ndoa zao tuliiii ila wakija ushaur utadhan mpo wote single
Anyway tafuta wanawake wasio na mambo mengi wale wasio na hekaheka na Dunia kama unapenda slay queens lazma ukose usingizi
 
Mtakao kwenda inbox na kutoa yenu kila la kheri... u GT muhimu sana hapa.

Kuna wakati ambao nashindwa kabisaa kufanya kazi!
Wakati mwingine nakosa usingizi nyakati za usiku😴..!
Nyakati zingine najikuta kama akili zimepoteaa😁
🙌🏼Haya yanakujia kiasi hiki umeyajuaje hayo!!!
Je, Unadai unaji.do na wa mtandaoni au wa kusikia squti unapopiga au kipi haswaaa..
 
Back
Top Bottom