Nahitaji faraja yenu wakuu. Kuachana na mtu unayempenda ni msiba mzito

Nahitaji faraja yenu wakuu. Kuachana na mtu unayempenda ni msiba mzito

Nipo hapa baba ma love love ❤️ 😘.karibu PM iko wazi.
Asante.





Kazi ni kipimo cha UTU
 
Amedata na pesa pamoja na status ya jamaa, acha liuwawe tuu, tamaa mbele mauti nyuma
Haya unadhani kila pisi ni pesa tu, sasa adate na pesa wakati juu hapo kaandika binti ndo alikua anampa pesa kijana..

Umeanza kujihusisha na mapenzi ukiwa na umri gani??
Kama ulianza enzi za barehe basi hiki analofanya huyu binti sio la ajabu kwa mabinti waliotupenda enzi hizo huna hata unachompa ila kadata tu na wewe.
 
Nilikuwa kwenye mahusiano karibia miaka miwili mwanaume hataki nifike anapoishi mwaka huu nimelazimisha kwenda kwake anapoishi amenitukana sana na kunifukuza na panga pamoja rungu.

Nilijipa muda akaomba msamaha ila mawasiliano yalikuwa hafifu juzi mwezi huu wa 7 nilimpa taarifa kuwa nitakuwa kikazi Dar ( mkoa anaofanya kazi) alinieleza kuwa nisifike kwake nifanye tu kazi iliyonileta.

Nililazimisha kwenda anapoishi alinipokea kishingo upande ila alinitukana sana na kutishia kuniletea polisi. Asubuhi nilienda kwenye majukumu yangu niliporudi kwake nikakuta amevusha mwanamke.

Majirani walinisikitikia sana wanasema kuwa hiyo ni tabia yake kubadilisha wanawake kila siku hasa bar maids! Nilipomkuta huyo mwanamke ndani nilijisikia vibaya nikatoa ya moyoni kwa huyo mchumba wangu na kuondoka Nimekubali tu yaishe nisije kupata maradhi kwa kung'ang'ania mwanaume mwenye wanawake wengi !

Hapa niliponinayo namaumivu yasiyo elezeka kwa sababu amenioneshea live huyo mwanamke! Majirani wananieleza afadhali hata umeona mwenyewe kuliko wangesema wao tabia yake ya kubadilisha wanawake hasa bar maids .

Huyu aliyekuwa mchumba wangu ni mfanyakazi wa serikali anaepata seminar mikoa mbalimbali ila kila siku ananiomba pesa ninavyomdai anazua ugomvi. Baadhi ya majirani wanasema ni tabia ya kuhongwa na wanawake (anapenda mserereko) kweli nimeamini fimbo ya mbali haiui nyoka

NAHITAJI FARAJA YENU WAKUU KUACHANA NA MTU UNAYEMPENDA NI MSIBA MZITO
ACHA kujibebesha mizigo isiyokuhusu..
Acha "nature" ifanye kazi yake...
"support panapohitajika na unapoweza (usijiumize)

Jipe muda wa kupona moyo na akili yako..
 
real meaning of upendo wa agape

Nilizabwa tu kofi nmegoma kusamehe hadi leo,we mwenzetu hadi panga unashikiwa na unasamehe🙌🏾
Unakubali vipi mwanaume mwenzio anakuzaba kofi msela Roja?
 
Back
Top Bottom