Nahitaji fundi anayeweza kufunga injini ya toyota kwenye Vogue

Inawezekana kabisa hiyo bila shida, wengi wanaobisha ni wanabisha tu ili wabishe basi.
 
INAWEZEKANA ILA UTAZAIMIKA KUBADILI ENGINE MOUNTING, GEARBOX NA CONTROL BOX NA SOME WIRING SYSTEMS KWA UJUMLA ITAKUKOST KIASI.
 
nipe namba mkuu
 
Kuweka engine nyingine inawezekana inabidi fundi azingatie power ya engine mpya na body weight ya gari ili gari iwe na uwiano mzuri wa power to weight ratio.

Kama unafatilia mbio za magari kuna gari ya yule mzee Taylor ni Nissan Silvia ila amefunga engine ya 1g na ameswap.
 

usimcheke hii kitu nimeshuhudia.... range rover vogue ikifanyiwa swap ya engine ya 1KZ pamoja na gear box yake
 
nyundo2017 Naomba kuisoma hii sayansi, ukifanikiwa kumpata huyo fundi. Nilishawahi sikia kipindi flani engine za magari tofauti unaweza kuswapp.

Toyota 1KZ engine na 1HZ zinakaa kwenye range vogue sema inabidi ubadili na gear box.... kuna garage inaitwa 0-60 wanafanya hyo kazi fresh
 
inawezekana kabisa wala asikupinge , swali je hiyo engine ya vogue ni ya diesel au petrol na hiyo ya toyota ni ya diesel au petrol

kwa alivyosema ni cruiser engine bila shaka itakuwa ni 1KZ na hii nimeshuhudia mara nyingi watu wakiswap kwenye range sema huwa wanabadili na gear box....

kuna watu hapa wanamtisha mleta mada wakati hata hawajui kitu kinachoitwa engine swap..

mleta mada aende kinondon garage inaitwa 0-60 garage watamfanyia hyo issue tena wale ni wataalamu watampa hadi ushauri mwingine
 
Mm na kazi ya kufanya modification ya estima hybride kuifanya iwe ya kawaida.baada ya kuua mfumo wake wa gearbox ilikata chain.

So natumia engine ile ile zaidi cha kubadili ni front cover pully ya engine unaweka sterling power,compressor,ortanelta,adjust ya fenbelt na nyuma unabadilisha flywhell pamoja na gearbox mchezo umekwisha..

Mbona haya mambo wazungu wanayafanya sana why ss tunatishana?? Sema kitu kimoja wabongo ss ni wavivu na waoga sana..

Mm natafuta mtu mwenye rx8 iliyokufa engine nataka ni swap engine ya subaru bila kubadilisha gearbox yake..
 
Mkuu ukifanya modification ya Mazda Rx8 kuiwekea engine ya Subaru itakuwa ni moja ya kazi nzuri kutokea.

Mimi naamini inawezekana ukija fanikiwa naomba utupe mrejesho.
 
Kuna jamaa alipachika injini ya Rav 4L kwenye Landrover Freelander. Hivi ninavyoandika hapa limesimamia mawe mpaka sasa bode kalii! Inasikitisha sana.
Nipe namba yake,mie nimefunga injini na giabox za rav 4 kwenye freelander huu ni mwaka wa 4 inadunda
 
Hii gharama yake yawezakuwa kiasi gani yaani kununua body la vogue,injini na gearbox ya 1kz oamoja na ufundi
 
Hii gharama yake yawezakuwa kiasi gani yaani kununua body la vogue,injini na gearbox ya 1kz oamoja na ufundi
body mara nyingi halina bei moja maana inategemea na anayekuuzia anakuuzia bei gani na condition ya body lenyewe na year of manufacture

kuna moja la vogue 2009 nilikuta linauzwa 10.5 million
 
Wabongo kwa uoga tumezidi. Hivi kama mtu kitu hukijui au hukiwezi kwa nini usikae kimya? Mleta mada achana na baadhi ya wapuuzi humu, wasikutie uoga. Fanya utafiti wao vizuri, tafuta mtu anaeweza kazi alafu fanya ulichokusudia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…