Nahitaji jukwaa nifanye stand up comedy

Mkuu, haina haja ya kutafuta wadhaamini na majukwaa moja kwa moja sbb ni ngumu na wengi wanaoitwa wanajulikana. Usiwaone Joti na wengine wanang'ara ukadhani waliibuka tu na kujulikana. Walijenga jina kwanza.
Kwa ulichokifanya ni mwanzo mzuri, kbsa wa kujulikana, usiangalie pesa kwanza sbb utapotea kwa sasa haujulikani.
Hapo chuo, kuna sherehe mbali mbali, omba kushiriki kama Mc hata kama usipopata u MC omba hata dk 10 au 20 kuchekesha. Mfano, kwenye mikutano hapo chuo, kabla hawajaanza mkutano, nenda mbele chekesha au kwenye sherehe za dini fanya comedy,(Usitangulize pesa), taratibu, utaanza kuwa maarufu chuo, na chuo kina watu wengi, kwahiyo kupitia hao watu wataanza kukuomba ukaburudishe katka sherehe zao. Kwenye sherehe za mitaani, nenda ukaombe U MC wakikunyima usikasirike, waombe dk 20 tu (Usiombe pesa) za kuchekesha, ukifanya kama sherehe 5, wao wenyewe wataanza kukaalika na hapo utakuwa ni mwanzo wa mafanikio yako. Mc pilipili alianza kwenye masherehe.
Usikimbilie kwa wadhamini ndugu yangu, utakuwa sawa na mtumwa. Kufika kwenye level ya mafanikio siyo mchezo, inabidi ukomae kweli.
Uaminifu na kujituma ndiyo ngao. Jenga jina kwanza hayo mafanikio yatakuja baada ya kujenga jina
 
Mkuu asante sana
Yaani mkuu umeandika vitu muhimu
Nafanya hivyo kuanzia sasa
Nina imani umenionesha njia
Asante mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chuki sim yako, jirekodi vipande kadhaa na kisha tupia Facebook, Instagram na YouTube.
Kama kweli unakipaji utaonekana.
Naamini huo ndio msaada mkubwa sana kwako.
Muone Nabii Tittto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…