Nahitaji jukwaa nifanye stand up comedy

Nahitaji jukwaa nifanye stand up comedy

Ni kijana wa chuo mwaka wa kwanza
Nimejihusha kwenye comedy hii
Nilifanya siku moja chuoni kila mtu aliipenda
Kwa sasa nimeamua kuingia moja kwa moja katika comedy hii
Kila siku najifunza vipya kutoka
Kenya
Nigeria
Marekani
Hapa Tanzania kwetu
Kwa sasa najiona nipo vizuri
Tatizo ni bado mdogo sana ,sijulikani,sijui hata stage nitaipata wapi,

Natamani atokee mtu yeyote anisapoti kwa hili
Nina imani ataipenda kwakweli
Nipo creative na hii sanaa
Nina jokes nyingi
Sina sapoti
Au kama kuna pati yeyote niitwe nafanya hata bure ili unione
Ukinisapoti wewe Nina uhakika na faida utapata kwa hili

Jaribu kunisapoti utaipenda kwakweli

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, haina haja ya kutafuta wadhaamini na majukwaa moja kwa moja sbb ni ngumu na wengi wanaoitwa wanajulikana. Usiwaone Joti na wengine wanang'ara ukadhani waliibuka tu na kujulikana. Walijenga jina kwanza.
Kwa ulichokifanya ni mwanzo mzuri, kbsa wa kujulikana, usiangalie pesa kwanza sbb utapotea kwa sasa haujulikani.
Hapo chuo, kuna sherehe mbali mbali, omba kushiriki kama Mc hata kama usipopata u MC omba hata dk 10 au 20 kuchekesha. Mfano, kwenye mikutano hapo chuo, kabla hawajaanza mkutano, nenda mbele chekesha au kwenye sherehe za dini fanya comedy,(Usitangulize pesa), taratibu, utaanza kuwa maarufu chuo, na chuo kina watu wengi, kwahiyo kupitia hao watu wataanza kukuomba ukaburudishe katka sherehe zao. Kwenye sherehe za mitaani, nenda ukaombe U MC wakikunyima usikasirike, waombe dk 20 tu (Usiombe pesa) za kuchekesha, ukifanya kama sherehe 5, wao wenyewe wataanza kukaalika na hapo utakuwa ni mwanzo wa mafanikio yako. Mc pilipili alianza kwenye masherehe.
Usikimbilie kwa wadhamini ndugu yangu, utakuwa sawa na mtumwa. Kufika kwenye level ya mafanikio siyo mchezo, inabidi ukomae kweli.
Uaminifu na kujituma ndiyo ngao. Jenga jina kwanza hayo mafanikio yatakuja baada ya kujenga jina
 
Mkuu asante sana
Yaani mkuu umeandika vitu muhimu
Nafanya hivyo kuanzia sasa
Nina imani umenionesha njia
Asante mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom