Salaam! Kuna ile hali huwa inamtokea mdogo wangu, kuna watu ambao mara nyingi humtabiria mema kama vile kuja kuwa kiongozi mkubwa n.k
Mfano mara nyingi hukutana na hizi kauli "ahsante sana utakuja kufanikiwa", " wewe ni mkombozi", "wewe ni kiongozi" n.k
Kauli hizi huambiwa hata na watu ambao hawajawahi kukutana hata siku moja. Pia huyu dogo ana sifa fulani za tofauti na ana tabia fulani za ajabu ajabu, mfano ulaji wake ni wa kushangaza, hali chakula kutoka nje ya kwetu.
Pia shuleni aliwahi kuwa wa mwisho kisa alikataa possible ya mtihani uliovuja, yaani ni kama hajali, na hayupo serious hivi. Kikubwa kilichonileta hapa ni kuwa ana tabia za kujitenga sana japo ana heshima. Jamani naombeni ufumbuzi wa kumfahamu huyu dogo.
Wataalamu nawasilisha!
Kama tokea zamani alikua na tabia hizo basi sio tatizo hilo ni tabia tu kuna watu wanatabia hizo.
Kama kipindi cha utotoni alikua mchangamfu anaongea mambo hayaendani na umri wake, afu mwoga sana kwenye matukio ya kutisha basi huyo ndio hawa tunaowaita ma introvert.
Sasa kumjua mtu kama huyu ni ngumu labda mzazi wake ambaye karithi tabia kutoka kwake(kwahiyo anajua kua hii hi copy yangu).
Mtu mwingine tu kumsoma ni shuhuli maana mara nyingi muonekano wao na vitu anavyowaza ni mambo mawili tofauti! (Body language haiendani na dhamira ya anachokizungumza(hapa utakuta mtu anachekesha, watu waliomzunguka hawana mbavu ila yeye hacheki au anatabasamu kwa mbali ila kiuhalisia nafsini mwake amefurahi vibaya mno na anavyohisi yeye kafurahi kama watu wengine).
Hata kwenye salamu unasalimiana na mshikaji kwa bashasha kama zote yani ila muitikio wake unakua wakinyonge tabasamu kwa mbaali! hapo moja kwa moja unaweza kuona mshikaji anadharau kumbe wala, ila nae nafsini alikua na vibe kama lote na nidhamu ya kutosha ila hata yeye hajui kua muonekano wake kipindi mnasalimiana haukuendana na bashasha zile.
Kwahiyo watu wa namna hii kiujumla kwa nje wanaoneka ni kauzu,wanadharau, waajiskia sana, ila ukimpa kazi au maelekeza ya kufanya utagundua mambo ni tofauti kazi inapigwa kwa nidhamu (kazi sahihi mahali sahihi na wakati sahihi (hakuna polojo)). Hapa ndio unakuta mtu nanamtukuza kwa kua hakutarajia kabisa.
Swala la unafiki... kujipendekeza kwa mtu kwa lengo fulani,uongo/polojo kwao ni kichefuchefu, kama unasikiaga masikini jeuri ndio hawa.
Kama unataka kujua upande wa pili wa huyo dogo nenda shule anayosoma hasa dalasani kwao ulizia hivi huyu akoje? Utatajiwa sifa nyingine ambazo zitakuacha mdomo wazi.