Nahitaji kufahamu kisima cha maji baridi (yaani maji yasiyokuwa na chumvi) huwa kinapatikanaje..?

George Betram

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Posts
4,672
Reaction score
6,272
Salaam wakuu..!
Nahitaji kufahamu kisima cha maji baridi (yaani maji yasiyokuwa na chumvi) huwa kinapatikanaje..?
Je,inategemea na eneo lako..?
Au ni jinsi/namna ya uchimbaji tu..?
Wataalamu wa hizi mambo naomba mnisaidie kuelewa,maana hapa mtaani kwangu kuna watu huwa wanaenda mbali sana kufuata maji ya kunywa yasiyo na chumvi,nilikua nafikiria kuitumia hii changamoto wanayokutana nayo kama fursa..!
 
Ngoja wahandisi wa maji waje kuelezea.
Mimi sio mtaalam wa haya mambo lakin kwa uelewa wangu nafikir hutegemea vitu viwili.
1.location ya kisima kinapochimbwa.
Eneo lililo karibu na bahari automatically maji yake yatakuwa na chumvi nyingi kuliko eneo lililo mbali na bahari.

2.Depth/Kina Cha kisima
Kadri unavyochimba kina kirefu zaidi ndivyo maji yanapozidi kuwa mazur.
Yaani ukichimba kina kifupi utapata maji yenye chumvi nyingi kuliko ukichimba kina kirefu.
Ni hayo tu machache ninavyofahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana mkongwe...
Kwetu ni mbali na bahari,pia wangekuja wenye ufahamu na hii kitu wangetuambia gharama zake zikoje kwenye kuchimba hicho kisima mpaka uyafikie maji mazuri..!
Ngoja tuendelee kuwasubiri wengine mkuu,huenda nikapata majibu nayoyahitaji..!
 
maji matamu yanategemea na maeneo uliyopo,mfano Tabata pale hata uchimbe ft ngapi bado utapata maji ya chumvi tu lakini ukiwa kama sehemu za vikindu,lugwadu,kazola na magodani kule ardhi yake ni mchanga na hata huendi mbali unapata maji matamu tena meupe sana .nakushauri nenda ubungo maji pale wapo wataalam wao wako na vifaa vya kujua uwingi wa maji na ubaridi wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli inategeamea location na kina cha kisima

Kwa mfano maenea ya mabibo asilimia 99% ya visima kule ni maji ya chumvi hata uchimbe mita ngapi kwenda chini

Lakini maeneo ya chamanzi 99% ya visima ni maji baridi tena matamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wilaya yaHandeni kote ni maji ya chkumvi
 
Iwapo sehemu unayoishi kuna maji ya chumvi...unaweza funga RO system.hii utoa chumvi yote na kuyafanya maji kuwa kama ya bomba 100%
 
Reverse osmosis (RO) is a water purificationtechnology that uses a partially permeable membrane to remove ions, molecules and larger particles from drinking water Hapa Tanzania kuna watu wanauza.ukiagiza china zinaanzia $ 3000 ya kuzalosha lita 1000 kwa lisaa.Kama utauhitaji yupo mtu anaunda na yupo cheap nikulink nae.viwanda kama SAYONA,MAJI POWA wamechimba visima na kufunga RO kisha wanapack maji kwenye chupa na kutuuzia mitaani.Wangekuwa wanapack maji ya dawasa bei yake tusingeweza kitaani
 
Nadhani hiyo mashine inahitaji mtu mwenye mtaji mkubwa zaidi Chief..!
 
Kama ni hivyo,basi nadhani eneo letu litakuwa halina maji baridi,maana kuna watu kama watatu wamechimba visima hapa mtaani kwangu,lakini vyote ni vya Maji chumvi..!
 
Nadhani hiyo mashine inahitaji mtu mwenye mtaji mkubwa zaidi Chief..!
zipo zinaanzia 2M. na ni bora kufunga hii kuliko kila baada ya mwaka kubadilisha mabomba na kufulia maji yasiyotakatisha nguo na kuzipausha na kufubahaa
 
zipo zinaanzia 2M. na ni bora kufunga hii kuliko kila baada ya mwaka kubadilisha mabomba na kufulia maji yasiyotakatisha nguo na kuzipausha na kufubahaa
Sawa...
Pia gharama za kuchimba kisima zikoje mkuu,hiyo ukijumlisha na gharama za kuweka tank..!
 
Sasa mimi nilikua nahitaji kwaajili ya kufanya biashara ya maji hapa mtaani kwetu..!
Inategemea hayo mazingira ulipo Kuna shida kiasi gani ya maji.
Kama mabomba ya maji ya dawasco hakuna kabisa,watu hata hayo maji yenye chumvi kwa mbali wananunua tu.
Hata mahali ninapoishi Mimi Kuna shida ya maji yaani maji ya dawasco hayajafika.
Kuna watu wamechimba visima na wanasupply kwa majirani Kisha wanapokea bili kwa mwezi na wengine wanaenda kununua kwa ndoo.
Kiufupi ni biashara nzuri isiyo na hasara.
Hasara yake ni mpaka mwenyezi mungu aamue kuyakausha maji.
Hata mm nilitaman kuifanya hiyo biashara ila kwa bahati mbaya au nzuri majirani zangu wameniwahi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mimi majirani zangu wameniwahi,ila wote maji yao ni ya chumvi...
Hivyo nilijua kuwa nikipata kisima cha maji baridi ni lazima niwapige "gap" tu..!
 
Hata mimi majirani zangu wameniwahi,ila wote maji yao ni ya chumvi...
Hivyo nilijua kuwa nikipata kisima cha maji baridi ni lazima niwapige "gap"
Dah hapo ni changamoto Sasa.
Kwa sababu hata ukinunua ile mashine ya RO itakugharimu kwenye umeme Sasa sidhani Kama itakuletea faida.
Kwani uko maeneo gani ya Dar?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah hapo ni changamoto Sasa.
Kwa sababu hata ukinunua ile mashine ya RO itakugharimu kwenye umeme Sasa sidhani Kama itakuletea faida.
Kwani uko maeneo gani ya Dar?

Sent using Jamii Forums mobile app
Upo sahihi sana mkuu...
Ndio maana mimi nilijua inawezekana kuchimba kisima moja kwa moja na kupata maji baridi...
Ila nilivyosikia hii habari ya mashine imenikatisha tamaa kiasi,kwasababu ni lazima gharama zitakuwa juu tu..!
Mimi naishi maeneo ya Temeke Kiongozi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…