Nahitaji kujenga nyumba Kibaha bajeti milioni 7

Mkuu tofali fafanua kidogo
Nimeassume vyumba vitatu ni roughly tofali 1000 zilizobaki 800 ni sebule,jiko,choo,stoo etc
-Tofali nzima za ujenzi 1500
-Zilizobaki 300 kama vipande maana yake utagawa mara mbili itaenda 600
So jumla ya 1500 + 600 = 2100
Kujenga tofali moja roughly 250 - 400 Average 300

Ufundi 2100 x 300 = 630,000/=
 
Mkuu nimekuelewa snaa
 
Wakuu nimejichanga nimefanikiwa kukusanya miilliomn 7 , nna kiwanja kibaha ,naomba ushaur kwa million 7 naweza kujenga nyumba ya vyumba vitatu ,choo na sebule. mwenye mwazo ya bajeti hii na aina ya nyumba naomben mtazamo wenu.
Nipo kibaha nitafte nitakushauri bure bila gharama yoyote
 
Unaweza kujenga vyumba viwili na sebule na choo ndani ila jiko liwe njee. Vyumba na sebule viwe (8ft x 8ft). Pia uongeze 1.5m hapo iliikamilike.
 
Inategemea pia eneo unalojenga 'miundombinu na mkoa wenyewe pia'kuna mazingira maji ni shida 'usafiri wa vifaa nk.
 
Mkuu, tofali 1000 siyo chache sana hizo! Au ni blocks?
 
Nimetumia 12M kujenga 2 rooms moja ikiwa master, public toilet, jiko na sebule lakini nimeishia kuweka bati, milango na madirisha Mkuu. Unaweza kupata picha hapo

Hiyo nyumba ni size gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…