Nahitaji kujenga nyumba Kibaha bajeti milioni 7

Nahitaji kujenga nyumba Kibaha bajeti milioni 7

Nimeassume vyumba vitatu ni roughly tofali 1000 zilizobaki 800 ni sebule,jiko,choo,stoo etc
-Tofali nzima za ujenzi 1500
-Zilizobaki 300 kama vipande maana yake utagawa mara mbili itaenda 600
So jumla ya 1500 + 600 = 2100
Kujenga tofali moja roughly 250 - 400 Average 300

Ufundi 2100 x 300 = 630,000/=
Ko hiyo cost ya ufundi inahusu ring beam wala nguzo au
 
Unaweza kujenga vyumba viwili na sebule na choo ndani ila jiko liwe njee. Vyumba na sebule viwe (8ft x 8ft). Pia uongeze 1.5m hapo iliikamilike.
Hivyo vyumba au tuvyimba? Yaani sebule iwe na mita 2 na point?
 
Nimetumia 12M kujenga 2 rooms moja ikiwa master, public toilet, jiko na sebule lakini nimeishia kuweka bati, milango na madirisha Mkuu. Unaweza kupata picha hapo
Huenda hatujamuelewa boma atamaliza ila cyo mpka bati
 
Nimetumia 12M kujenga 2 rooms moja ikiwa master, public toilet, jiko na sebule lakini nimeishia kuweka bati, milango na madirisha Mkuu. Unaweza kupata picha hapo
Mnajitesa kwa maslahi ya Nani?
 
Bro inategemea jinsi unavyotaka nyumba yako iwe imara,wengine hiyo budget ya jamaa 7mill ilikuwa haitoshi hata kumalizia msingi.

Ushauri wangu kwa mdau aende mdogo mdogo aanze kwanza msingi then apandishe taratibu taratibu haya mambo ya unaingia site kichwani ukiwa na picha ya nyumba iliyokamilika wakati hela yenyewe ndogo itaku-cost maana utataka ubane pesa ili lengo litimie na utashangaa zaidi pale nyumba unafunga lintel juu huku chini msingi unapasuka.

Sasa fundi akikukokotolea hesabu za kurudi chini ukaimarishe kwanza msingi ndo ukaendelee tena juu hapo ndipo mwanzo wakukata tamaa na kuanza kurusha pics mitandaoni kutafuta wanunuzi wa pagale lako.
Inategemeana pia na site, kwa mfano mimi msingi peke yake ilinigharimu 5.8 , zilotumika tofali za inch 6 1350, imagine hapo msingi tu
 
Wakuu nimejichanga nimefanikiwa kukusanya miilliomn 7, nina kiwanja Kibaha, naomba ushauri kwa million 7 naweza kujenga nyumba ya vyumba vitatu, choo na sebule?

Mwenye mawazo ya bajeti hii na aina ya nyumba naombeni mtazamo wenu.
Unajenga nyumba umechanja?
 
Wakuu nimejichanga nimefanikiwa kukusanya miilliomn 7, nina kiwanja Kibaha, naomba ushauri kwa million 7 naweza kujenga nyumba ya vyumba vitatu, choo na sebule?

Mwenye mawazo ya bajeti hii na aina ya nyumba naombeni mtazamo wenu.
Kwa ukubwa wa nyumba unayoitaka, milion 7 haitoshi kumaliza jengo lote
Katika hiyo milion 7, kumbuka kuna pesa ya ufundi pia...ukijibana sana inaweza ikakufikisha mpaka hatua ya mkanda wa juu
Piga hesabu ya chini kabisa
Tofali 3000@1,000= 3,000,000
Cement 60 @ 15,000 = 900,000
Nondo 50 chini na juu@ 25,000=1,250,000
Mpaka hapo imeshafika milion 5+, bado kokoto, mchanga, cement kwa ajili ya zege la mikanda n.k
 
Na ongeza ya ufundi at least 1200,000/=
 
Wakuu nimejichanga nimefanikiwa kukusanya miilliomn 7, nina kiwanja Kibaha, naomba ushauri kwa million 7 naweza kujenga nyumba ya vyumba vitatu, choo na sebule?

Mwenye mawazo ya bajeti hii na aina ya nyumba naombeni mtazamo wenu.
Ni nyumba yenye hadhi ipi hiyo? Nina uzoefu wa kutosha kwa hiyo mambo, iwe simple saaaana, only a singo room and over
 
Back
Top Bottom