Kuwa watofauti ukipambana pata sehemu za kumwaga kama wenzio ikiwa ngumu, usiumie.... tafuta sehemu tofauti inayopitika kiasi fuata taratibu weka mzigo wako utafika mkuu....
Siku nyingine unakaa Tu mjini angalia nguo gani zinavaliwa sana..
kama target yako wanachuo basi
pensil skirt
vimini jeans
Skin jeans
Track suits
koti jeans.
Nisiongelee sana hapa pambana alafu uwe na bei special Yan mtu anakuja kwako anajua unauzaga koti jeans Kali 10, au pensil skirt Kali unauzaga 10 (bei usibadikishe Sana)
Kwenye viatu mimi nakwambia
tafuta viatu vya kike changanya na raba za mtumba kali sama za kike chukua hapo karume hata ukikuta raba Kali 5000 chukua wewe utazofua utauza 10 Hadi 15....
Kuwa makini katika bei yani maana lengo ni kufika lakini sio kwa kupaa Ila kwa mwendo wa taratibu...
Viatu na raba zako kali, Uza kwa bei ya kishkaj
alafu pia jitahidi ujenge ukaribu na wateja...siku nyngne huko status unapost wateja wakiwa na bidhaa yako unawasifia na kuengage nao watoto wakike huwa wanafurahi sana na kuwa permanent buyers pia huwaleta wenzao .