Nahitaji kukopa benki ya CRDB kwa dhamana ya nyumba

Nahitaji kukopa benki ya CRDB kwa dhamana ya nyumba

Wakuu,ligi ndio hizooo

Naombeni kujua ABC ili kuweza kupata mkopo katika bank ya CRDB kwa dhamana ya nyumba siitaji kiasi kikubwa kama milioni 8 tu inatosha ningependa kujua masharti yao riba zao kuhusu kurudisha hata wakinipa wiki inatosha nitarudisha zote na riba ya nusu kwa nusu m8 kwa m16 matumizi yatakuwa kama ifuatavyo nampa, yanga win, nampa city win nampa liverpool nampa ×1 real madrid jumla odd 8 nikiweka m6 mara 8 mana m2 za kula bia siku ya pili narudisha crdb pesa yenu tafathar wakuu nipen mwongozo
Mchakato wa Bank ni mgumu kidogo, hawatoi mkopo kwa vile una dhamana. Wanakupa mkopo wakijoridhisha una uwezo wa kuulipa. Uwezo wa kuulipa ni either kupitia mshahara kama umeajiriwa au kupitia biashara kama unashighulika na biashara.

Kama ni muajiriwa ni rahisi. Wala huitaji kuweka dhamana, mshahara wako tu ni dhamana kwao.

Ila kama ni mfanya biashara. Hakikisha uwe na vifuatavyo.
1. Biashara yenye umri zaidi ya miaka 3
2.mahesabu ya biashara ya miaka 3
3. Leseni
4.TIN
5. Usajili wa Brela
6. Tax clearance
7. Statement ya bank inayoonesha mzunguko wa miezi sita.
8. Dhamana
9. Makisio ya mapato ya mwaka.
10.return za brela kama ni kampuni.
11. Stock ya bidhaa dukani
12. Kama ni shughuli za tender, mikataba ya kazi

Kama vyote umekamilisha, mchakato wa mkopo ni ndani ya wiki 3.

Kila la kheri mkuu.
 
Back
Top Bottom