Nahitaji kukopa benki ya CRDB kwa dhamana ya nyumba

Mchakato wa Bank ni mgumu kidogo, hawatoi mkopo kwa vile una dhamana. Wanakupa mkopo wakijoridhisha una uwezo wa kuulipa. Uwezo wa kuulipa ni either kupitia mshahara kama umeajiriwa au kupitia biashara kama unashighulika na biashara.

Kama ni muajiriwa ni rahisi. Wala huitaji kuweka dhamana, mshahara wako tu ni dhamana kwao.

Ila kama ni mfanya biashara. Hakikisha uwe na vifuatavyo.
1. Biashara yenye umri zaidi ya miaka 3
2.mahesabu ya biashara ya miaka 3
3. Leseni
4.TIN
5. Usajili wa Brela
6. Tax clearance
7. Statement ya bank inayoonesha mzunguko wa miezi sita.
8. Dhamana
9. Makisio ya mapato ya mwaka.
10.return za brela kama ni kampuni.
11. Stock ya bidhaa dukani
12. Kama ni shughuli za tender, mikataba ya kazi

Kama vyote umekamilisha, mchakato wa mkopo ni ndani ya wiki 3.

Kila la kheri mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…