Nahitaji kukopa milioni 9, makato yakoje?

Nahitaji kukopa milioni 9, makato yakoje?

Ruyama

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2019
Posts
367
Reaction score
563
Habari,

Ninahitaji kujenga nyumba simple mshahara wangu laki 5 je nikisema nijilipue NMB au CRDB nivute mkopo wa million 9 nitakuwa nakatwa shillings ngapi?

Msaada please [emoji120]
 
Makato yanategemea kipato chako na muda wa marejesho.

Watembelee benk husika watakupatia hesabu kamili. Ulizia zaidi ya benki mbili. Ulingalishe ubora wa huduma sio lazima CRDB tu
 
Kama vile mkopo mkubwa sana ukilinganisha na pay yako.

Japo waweza katwa miaka 3 lakini makato yatakuwa si chini ya shilingi laki tatu monthly.

Kopa mil.5 usimamishe pagala kwanza. Kuezeka uje kukopa tena.
 
Habari,ninahitaji kujenga nyumba simple mshahara wangu laki 5 je nikisema nijilipue NMB au CRDB nivute mkopo wa million 9 nitakuwa nakatwa shillings ngapi? msaada please [emoji120]
Mbona hili jukwaa mnalikosea heshima?
Mkopeshaji yupo na unamjua,kwanini usimuulize anayekukopesha?
 
Habari,ninahitaji kujenga nyumba simple mshahara wangu laki 5 je nikisema nijilipue NMB au CRDB nivute mkopo wa million 9 nitakuwa nakatwa shillings ngapi? msaada please [emoji120]
Kwa mda gani utataka ukatwe?
 
Kwanini usitafute hela angalau milioni nne ukasimamisha tofali halafu ndio ukope ufanyie finishing angalau ile hela ya pango itakusaidia kwenda kwenye makato ya mkopo. Ila ukikopa uanze kujenga nyumba kwa milioni 9 naona nyumba haitaisha na utabaki na makato ya bank na huku unapoishi kuna kudai kodi
 
Kopa tu dogo, kama uko serikalini unaweza kurejesha kwa miaka mi-5 Tenaaaa! Makato yatakuwa kama 333,000 kwa mwezi utabakiwa na kama 170,000 kwa mwezi (ila kama hiyo laki 5 ni take home). Deni hilo utarejesha kwa miezi 60 na utawapa benki zaidi ya 6 m kama interest! Kazi kweli kweli!!
 
Habari,ninahitaji kujenga nyumba simple mshahara wangu laki 5 je nikisema nijilipue NMB au CRDB nivute mkopo wa million 9 nitakuwa nakatwa shillings ngapi? msaada please [emoji120]
Ukubwa wa makato yako utategemeana na muda wako wa mkopo ( u
Uhai wa mkopo ).

Ukikopa miaka mingi, utakatwa pesa kidogo ila deni utalilipa kwa muda mrefu sana na jumla ya pesa utakayorejesha itakuwa KUBWA.

Na vice versa is true.
 
Shukrani [emoji120]
 
Kopa tu dogo, kama uko serikalini unaweza kurejesha kwa miaka mi-5 Tenaaaa! Makato yatakuwa kama 333,000 kwa mwezi utabakiwa na kama 170,000 kwa mwezi (ila kama hiyo laki 5 ni take home). Deni hilo utarejesha kwa miezi 60 na utawapa benki zaidi ya 6 m kama interest! Kazi kweli kweli!!
Kumbee[emoji44]
 
Kabla hujakopa nenda CRDB wakupe maelezo halafu nennda NBC wakupe maelezo ya mikopo na riba yao kisha fanya maaamuzi.
CRDB riba ipo juu sana zaidi ya NBC ila kabla ya kuamini maelezo yangu na wewe fuatilia kwanza.

NB chukua mkopo wa muda mfupi
 
Back
Top Bottom