Nahitaji Kununua Shrika Letu la Posta - (ningekuwa na uwezo)

Nahitaji Kununua Shrika Letu la Posta - (ningekuwa na uwezo)

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Wapendwa
Nimekuwa nafuatilia mtandao wa kusafirisha mizigo hasa toka nje ya nchi nikaona kuwa tunayo Lulu kama sio dhahabu tuliyo lalia nayo ni shirika la posta;
Hili shirika lina mtandao mzuri sana nchi nzima pamoja na magari ya kusafirishia mizigo vifurushi pamoja na store za uhakika za kutunza mizigo.

Kwa hii karne ya sasa ambapo watu wengi hasa vijana kupenda kununua mitandaoni na kusafirisha kwa njia zingine zikiwemo DHL na wenzake ambao ni zaidi ya mara mbili ya gharama za shirika la posta
Naona kunahaja ya kuchukua hiyo fursa

Hili shirika likichukua nafasi yake vizuri wala hakutakuwa na haja wafanya biashara wa Mikoani kufuata mizigo kariakoo na maduka mengine ya Jumla jijini Dar??? badala yake limeachia nafasi yake ichukuliwe na mabasi ya Abiria kwa ufanisi usio na ushindani

Kwa mawazo yangu; kinacho kosekama shirika la posta na kukwaza watu ni upotevu wa bidhaa hasa hizi ndogondogo zinazotoka nje za gharama kubwa kama simu, computer nk

Hebu atokee mkurugenzi aliyoko tayari kuwalipa watu kitu kikipotea mikononi mwao.....kwa kuwakamata wezi na na kuwachukulia hatua stahiki...tuone kama shirika la posta halitakuwa Millionea ndani ya miaka mitano
Sioni kwa nini wafanyakazi wa Shirika la Posta wasilipwe mishahara na marupurupu kama wa TRA?

Natamani kupata fursa ya kushiriki kujenga uchumi kupitia shirika letu la posta!
 
networthy yako ni tzs???? je unamkaribia rostam aziz interms of networthy????
 
Binafsi naamini sana kwenye soko la ndani ni kubwa sana...
Sasa hivi Vijana wana agiza gadgets za mamilioni kila mwezi na zinalipiwa kwa dola ila zote hazipitishwi shirika letu pamoja na kutosa bei nzuri sana..

Kikubwa sana wanacho ogopa ni wizi wa hapa ndani kwenye shirika... kwani mtu aliyeibiwa mzigo/parcel akiwasiliana na mashirika yaliyotuma..tracking reference inaonesha mzigo/parcel imeingia Tanzania; ina maana mizigo inaibiwa humu kwetu.
Kwa bahati mbaya sana, sijui nini kimewafunga hao wanaolisimamia...hawaoni kama ni tatizo linalopelekea hili shirika kujifunga??
Najua lipo tatizo lingine la speed na accuracy ila hilo ni rahisi kulishuhulikia

Sasa hivi kwa hii technilogia, inatakiwa mtu kutoka mikoani afuate mzigo wake ofisi zetu za Posta za karibu/ kijijini au wilayani na sio Dar au Zanzibar
Yaani inaniuma sana kuona tumelalia dhahabu halafu wafanyakazi wetu wanalia njaa.....

Kimsingi haihitaji kwenda nje ya Nchi kufanya marketing ya shirika letu kwa sasa wakati soko la ndani performance ni 20% ??? tuanze na soko la ndani kwanza na kupata walau 80% support ndio tupanue uigo
 
Una mtazamo mzuri. Shirika likiboreshwa litatoa ajira nyingi sana kwa vijana kusambaza vipeto nyumba kwa nyumba kama majuu.
 
Back
Top Bottom