Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 3,092
- 5,386
Wapendwa
Nimekuwa nafuatilia mtandao wa kusafirisha mizigo hasa toka nje ya nchi nikaona kuwa tunayo Lulu kama sio dhahabu tuliyo lalia nayo ni shirika la posta;
Hili shirika lina mtandao mzuri sana nchi nzima pamoja na magari ya kusafirishia mizigo vifurushi pamoja na store za uhakika za kutunza mizigo.
Kwa hii karne ya sasa ambapo watu wengi hasa vijana kupenda kununua mitandaoni na kusafirisha kwa njia zingine zikiwemo DHL na wenzake ambao ni zaidi ya mara mbili ya gharama za shirika la posta
Naona kunahaja ya kuchukua hiyo fursa
Hili shirika likichukua nafasi yake vizuri wala hakutakuwa na haja wafanya biashara wa Mikoani kufuata mizigo kariakoo na maduka mengine ya Jumla jijini Dar??? badala yake limeachia nafasi yake ichukuliwe na mabasi ya Abiria kwa ufanisi usio na ushindani
Kwa mawazo yangu; kinacho kosekama shirika la posta na kukwaza watu ni upotevu wa bidhaa hasa hizi ndogondogo zinazotoka nje za gharama kubwa kama simu, computer nk
Hebu atokee mkurugenzi aliyoko tayari kuwalipa watu kitu kikipotea mikononi mwao.....kwa kuwakamata wezi na na kuwachukulia hatua stahiki...tuone kama shirika la posta halitakuwa Millionea ndani ya miaka mitano
Sioni kwa nini wafanyakazi wa Shirika la Posta wasilipwe mishahara na marupurupu kama wa TRA?
Natamani kupata fursa ya kushiriki kujenga uchumi kupitia shirika letu la posta!