Yawekana ukawa na mantiki kwenye content ya unachokiongelea, lakini napingana na wewe hapo kwenye kusema "Waafrika wana laana"
Nchi yoyote unayoiona imepiga hatua kwenye jambo lolote, basi siasa ina mchango mkubwa sana. Kinachotukwamisha Waafrika na Watanzania (to be specific) ni ubinafsi, sio elimu.
By nature, binadamz ni mbinafsi, lakini kiwango Cha ubinafsi kinapozidi Jamii lazima irudi nyuma maana kitakachofatia ni "Every man for himself". Mfumo wa elimu yetu inawezekana haupo vizuri, lakini ukirudi miaka mingi nyuma, mababu zetu hawakusoma, ila Kuna mambo waliweza kuyamudu maana hawakuwa wabinafsi. Kinachofanya niseme elimu sio tatizo kuu, angalia kwenye list ya viongozi wa sekta mbali mbali, wengi wao wamesoma nje ya nchi, tena katika mazingira Bora kabisa. Elimu ya hapa nnchini haijawaathiri, isipokuwa ubinafsi ndio unaziba utashi wao.
Kingine, Watanzania wengi tunajifanya hatupendi siasa, tunaamini kuwa inabidi tuwe busy na utafutaji hela na sio maswala ya siasa. Bila kujua hizo hela tunazoenda kutafuta, zinategemea siasa pia. Matokeo yake wafanya maamuzi watafanya hayo maamuzi bila kuangalia maslahi mapana ya nchi, mwisho wa siku impacts zinawarudia wale wanaosema wako busy na utafutaji hela, hawana muda na siasa.
Mimi nadhani, badala ya mfumo wetu wa elimu ungejikita kwanza kutoa elimu ya uraia na maswala ya uzalendo tangia tukiwa shule za msingi. Kwanini nasema hivi, sababu ni kwamba raia wengi wanajua maana ya neno uzalendo lakini hawawezi kuuishi uzalendo kwa vitendo. Mpaka sasa wapo wanaoamini uzalendo ni kuunga mkono serikali au chama tawala.
Kingine ambacho naweza kukukumbusha, mada yako imeongelea madini, Mimi nitazungumzia maliasili zote (madini yakiwepo). Hizi maliasili zimegawanyika ki Kanda. Kuna Kanda zina madini, zingine mbuga au vyanzo vya utalii. Na hata interest za watu zimejigawa hivyo hivyo kikanda, ndio maana leo ukienda Kanda ya ziwa au sehemu zenye madini, vijana/watu wa maeneo hayo wanapenda sana habari za madini, na hata utafutaji wao umejikita kwenye madini ( bila kujalisha elimu yao), na na unaweza ukakutana na Mzee ambae hana elimu yoyote, ila anauwezo wa kutrace vein na kuipata miamba iliyokuwa na madini, kitu ambacho wataalam wanakaa darasani miaka mingi kupata huo uwezo.
Au nenda Arusha, Kilimanjaro, Saadan,Ngorongoro uone jinsi wakati wa maeneo yale walivyo interested na utalii. Kuna wamasai hawajawahi kuingia darasani, ila wanaongea Kiingereza kilichonyooka kuzidi hata wasomi wengi. Nenda Mtwara uone vijana walivyo interested na kilimo Cha zao la korosho n.k
Kwa mantiki hiyo, serikali ikisema iingize mtaalam wa madini, wapenda kilimo na ufugaji hawatopendezwa sana, wapenda utalii hawatopendezwa sana. Badala yake nadhani elimu yetu ingejikita kwenye somo la kujitambua, uraia na maana halisi ya uzalendo na mzalendo mwenyewe. Kuhusu maliasili imeziongelea sana, tumeimbishwa hadi nyimbo kuhusu mbuga zetu, tumeshaambiwa sana tafsiri ya rangi za bendera zetu, lakini angalia tulipo.
Huwezi kumfundisha mtu uzalendo akiwa chuo au sekondari. Shule ya msingi ni msingi wa kila jambo. Somo la uzalendo lianzie kule.
Waafrika hatujalaaniwa mkuu