Nahitaji kupingwa kwa hoja kwa mambo ninayo amini kuhusu watu weusi

Nahitaji kupingwa kwa hoja kwa mambo ninayo amini kuhusu watu weusi

Hakuna laana Bali tangu mwanzo msingi uliwekwa kwenye uvivu, utegemezi yaani waliopaswa kujenga watu kwenye msingi wa nguvu ya mtu wao waliwajenga kwenye utegemezi ili nawao waje kunufaika na utegemezi huo, mfano jinsia ya kike isisome ili ikatumike kuleta mali kwenye familia kiasi Cha jamii ya kike kuwa dhaifu wa uchumi lakini wangepewa maarifa na kupata nguvu au energy ya kutoa maamuzi ya maana na kuwa na uchumi mambo yangejengeka vizuri, haya jinsia ya kiume ikapewa mfumo wa uvivu yaani utanwa wa kufanyiwa kila kitu hata mtoto mdogo akiwa wa kiume asijiweze kwa chochote katika ngazi ya familia kitu kilichopeleka uvivu ofisini na kwenye kazi kiasi Cha kuchagua kazi za kukaa tu ndo zinapendwa wakati wenzetu hawalali yaani kazi zinafanywa saa 24 kama ni shift basi zitapangwa, imagine mpaka kijana wa kiume kutamani kuwa wa kike ili awe mvivu na asiwe na uwezo wa kujenga Bali asubiri kujengewa, wenzetu miaka kumi na nane ni mtu mzima mwenye maamuzi maana amejengwa katika ability ya kufanya mambo na siyo kufanyiwa lakini sisi baba wa miaka 50 Bado anajidekeza eti jamani wazazi hawanisaidii au watoto hawanipi hela na ukiangalia Nini kilimkwamisha ni ujinga tu aliyokuwa anafanya hasa kuchezea muda wa shule au starehe kwa sana au kuishi bila mipango ya baadaye, Uvivu, Uvivu, Uvivu ndo tatizo la Afrika.
😂😂😂Uvivu ndio laana yenyewe maana inaama kizazi kwa kizazi bado jamii nyingi za watu weusi azijashtuka compared to igbo,kikuyu and chaggas in tz few to mention.

Kuna mahali niliwahi kusoma kwamba wavivu ni wagunduzi wazuri sanaa i.e viti vya matairi maofisini kwa nini sisi Uvivu wetu hauna tija.....jibu ni laaana.
 
Watoto wetu wakimaliza shule hasa Form 4 na form 6 wanaingia kuwa machinga, kuendesha bajaji na Bodaboda huku wakiwa hawana kabisa ufahamu kuhusu rasilimali zao za madini waliyobarikiwa na Mungu.
Hao wanaokuibia madini ndio wanaokuletea story za Mungu wa uongo ambaye hayupo.
 
Nsikuchoshe na Usinchoshe, tusichoshane.

Huwezi kuniambia niendelee kuusifu Uafrika wakati kuna mambo ya kutumia tu akili ndogo tumeshindwa kuyafanya.

Mfano.

Taifa la Tanzania ni moja ya nchi inayopatikana kwenye hili bara la Afrika (BARA LILILOJAA NEEMA).Moja ya Rasilimali tulizonazo kama Taifa ni pamoja na Madini (DHAHABU, ALMASI, TANZANITE, MAKAA YA MAWE n.k)

Shule zetu (Msingi & Sekondari) hadi leo hakuna mtaala unaohusu madini, namna ya kuyatunza na namna ya kuyachimba. Ajabu ni kwamba Nchi zisizo kuwa na Madini ndizo ambazo zinawapatia watoto wao elimu inayohusu madini kisha wanakuja kuyachimba, kuyaandaa na kuyasafirisha ili wakatajirike.

Watoto wetu wakimaliza shule hasa Form 4 na form 6 wanaingia kuwa machinga, kuendesha bajaji na Bodaboda huku wakiwa hawana kabisa ufahamu kuhusu rasilimali zao za madini waliyobarikiwa na Mungu.

Kwakuwa sisi ni washamba kwenye rasilimali zetu, ndiyo maana wakati fulani walitokea waafrika wajinga wakawa wanapasua chupa na kuzifunga vizuri na kuingia mjini kisha kuwahadaa waafrika wenzao kwamba zile zilikuwa ni Almasi na kiukweli wajinga wale walijipatia sana fedha miaka hiyo.

Madini tumebaki kuyatazama huko YouTube na kwenye television.

Pamoja na Madini kuwa ni mali yetu sisi Waafrika lakini wanaonufaika nayo ni watu weupe.

Wao wanachimba (Sisi hatuwezi kuchimba kwasababu kuna wajaa laana huwa wanasema hatuna mitambo,sasa sijafahamu hiyo mitambo inauzwaga kiasi gani cha fedha ambacho hatuna uwezo wa kununua)

Wao wanayafanyia processes (Sisi hatuwezi kufanya processes kwakuwa wajaa laana huwa wanasema hatuna mitambo,Hiyo mitambo inauzwaje kama Taifa tushindwe?)

Wao wanasafirisha (Hapa wajaa laana huwa wanasema tukifanya sisi tutakosa masoko, watazira!)

Haya ndiyo tuyafanyayo ngozi nyeusi.

Kazi tunazoweza ni kusomesha watoto na wakimaliza waingie mitaani kuwa wachuuzi wa bidhaa(Machinga) au kuendesha Boda na Bajaji halafu tuwaminye ki kweli kweli walipe kodi wakati huo huo huku kwenye Madini ambayo tumepewa Neema na Mungu Kodi inayokatwa haiendani na kile tulichonacho na wakati mwingine hao wachimbaji wanakwambia "HATUJAPATA FAIDA, HIVYO HATUWEZI KULIPA KODI".

Kama Ndivyo!?

Kwanini nikisema AFRIKA INA NEEMA ILA WAAFRIKA WANA LAANA mnachukia na kufuta nyuzi zangu?

Hayo niliyoyaainisha ni machache sana miongoni mwa meeeeengi mnooooo ambayo ngozi nyeusi inayafanya,sasa sijui mnataka nitumie lugha gani!.

NIPINGENI KWA HOJA, KWANINI NISISEME NGOZI NYEUSI INA LAANA?

NAHITAJI KUELEWESHWA ILI NIWE NA MTAZAMO CHANYA KUHUSU NGOZI NYEUSI.
 
umeitaja Biblia negatively, unakosea sana. Biblia ni Neno la MUNGU. na hili Neno la MUNGU ndilo linaotuongoza hapa duniani, na kutuelekeza kule tutakapoyapata maisha ya milele na MUNGU wetu. Kama wazungu walichukua almasi wakatuachia Biblia, wenye faida ni sisi. mali za dunia hii tutaziacha hapa hapa duniani. la msingi ni lile la milele.

YESU ni NJIA, KWELI na UZIMA.
😂😂😂😂😂😂 Hapa ndio inaonyesha kabisa tumelaanika wenzetu wanapambania maisha yanayoonekana sisi tunajifariji na maisha ya kufikirika na yenye ubaguzi na masharti sio kua ni ticket ukishakufa ni uhakika wa kuanza hayo maisha fikirika.
 
Elimu ya Shuleni haiendani na Maisha ya Mtaani. Nyumbani Mzazi anataka mtoto amiliki simu ila shuleni hawataki watoto wamiliki simu. Mwanachuo hajui kutuma wala kupokea email.. Mwalimu hajawaji kufanya practical au field ya anachokifundisha... na aliyefundishwa anatakiwa ajiajiri kwa elimu aliyoipata.. TUMELAANIKA HASWAA.!!
Hivi hii 2023 kuna mwanachuo kweli asiyeweza kutuma na kupokea emai?
 
Ni kweli sisi ni ile mbegu iliyodumaa, na sio madini tu ni technology ifundishwe from childhood mana sioni chenye maana kukaririsha kijana mdogo mambo ambayo hana interest nayo
Kama sijakosea, Mr. Blue aliamua kuacha shule kisha akajikita katika music. He's my agemate and his decision paid him off very well.
 
Yesu ni njia na uzima, kama simwamini kama mwana wa Mungu nitapotea??je aliumba wapagani, Wajapani, warusi na wote wasiomwamini ili wapotee? Ni Mungu gani? Labda huyu aliyeletwa na wamisionari. Mimi Mungu wangu wa asili, anatokana na mababu zangu ndiye ninaemwamini. Mungu wa kweli ni yule anatokana na jadi yako.
 
Nina swali:

- Hii inajumuisha watu weusi waliochukuliwa kama watumwa ambao sasa wapo nchi za nje? Au ni sisi tu huku Africa ndani?
Mkuu, kwani hauoni kama kitendo cha kuchukuliwa kwa nguvu na kufanywa mtumwa, hivyo pekee inatosha kuonesha dalili zote za mtu mwenye laana? Kwanini wazungu hawakuwa watumwa huku Africa??
 
Kwani mpaka sasa haufahamu kwanini wacongo wanapigana?

Lakini pia, ungekuwa umeelewa nilichoandika walau usingeandika hivi.
Bro nimesoma ulichokiandia naomba nikuulize kitu
Je nchi zilizoendelea watu wake hakuna walio wa binafsi??
Maana asili mojawapo ya human being ni ubinafsi
Kama wao hawana waliwezaje kutokuwa nao??
 
umeitaja Biblia negatively, unakosea sana. Biblia ni Neno la MUNGU. na hili Neno la MUNGU ndilo linaotuongoza hapa duniani, na kutuelekeza kule tutakapoyapata maisha ya milele na MUNGU wetu. Kama wazungu walichukua almasi wakatuachia Biblia, wenye faida ni sisi. mali za dunia hii tutaziacha hapa hapa duniani. la msingi ni lile la milele.

YESU ni NJIA, KWELI na UZIMA.
Una fikra za kimaskini sana,

Na unadhihirisha kwamba Biblia imeharibu mfumo wako mzima wa kufikiri.

Uko sawa na teja aliye haribiwa na madawa ya kulevya.

Dini ni utumwa wako wa fikra

Jomo Kenyatta alisema kwamba:

"When the Missionaries came to Africa They had a Bible, We had the land. They said let us pray we closed our eyes, When we opened them they had the land, We had the Bible"

Yani ume danganywa kuna maisha bora mbinguni, ili ubweteke wajanja wachukue mali zako!!!!

Mbingu Haipo.

You cannot wish for a house of Gold in Heaven while you have never touched Gold right here on Earth.

If you fail to live on Earth, The fantasy of heaven is an illusion.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Hapa ndio inaonyesha kabisa tumelaanika wenzetu wanapambania maisha yanayoonekana sisi tunajifariji na maisha ya kufikirika na yenye ubaguzi na masharti sio kua ni ticket ukishakufa ni uhakika wa kuanza hayo maisha fikirika.
Huyu amesha haribiwa na dini vibaya mno.

Ni sawa na teja

Ndio maana ana jifariji na maisha ya kufikirika.
 
Mtu mweusi akisoma akija mtaani anajitenga na wenzie kisingizio sio level yake.

MTU mweusi akiwa na mrija wa pesa anapiga na anajenga Nyumba ya kifahari yenye Sweamingpool lihali Jirani yake hana hata Choo kizuri.

Mtu mweusi anaamini sana Ushirikina na Mapenzi kuliko kazi.

Mtu mweusi hapendi kazi ngumu bali kuomba omba
Mtu mweusi ana penda sana vya kupewa
 
Bro nimesoma ulichokiandia naomba nikuulize kitu
Je nchi zilizoendelea watu wake hakuna walio wa binafsi??
Maana asili mojawapo ya human being ni ubinafsi
Kama wao hawana waliwezaje kutokuwa nao??
Ubinafsi ni asili ya mwanadamu, hata Mimi nimesema huko juu. Tofauti yao na sisi, ni uzalendo na kujitambua kwa raia wao. Kiasi kwamba anayeingia madarakani, anakuwa anatanguliza maslahi ya nchi kwanza.
 
Nsikuchoshe na Usinchoshe, tusichoshane.

Huwezi kuniambia niendelee kuusifu Uafrika wakati kuna mambo ya kutumia tu akili ndogo tumeshindwa kuyafanya.

Mfano.

Taifa la Tanzania ni moja ya nchi inayopatikana kwenye hili bara la Afrika (BARA LILILOJAA NEEMA).Moja ya Rasilimali tulizonazo kama Taifa ni pamoja na Madini (DHAHABU, ALMASI, TANZANITE, MAKAA YA MAWE n.k)

Shule zetu (Msingi & Sekondari) hadi leo hakuna mtaala unaohusu madini, namna ya kuyatunza na namna ya kuyachimba. Ajabu ni kwamba Nchi zisizo kuwa na Madini ndizo ambazo zinawapatia watoto wao elimu inayohusu madini kisha wanakuja kuyachimba, kuyaandaa na kuyasafirisha ili wakatajirike.

Watoto wetu wakimaliza shule hasa Form 4 na form 6 wanaingia kuwa machinga, kuendesha bajaji na Bodaboda huku wakiwa hawana kabisa ufahamu kuhusu rasilimali zao za madini waliyobarikiwa na Mungu.

Kwakuwa sisi ni washamba kwenye rasilimali zetu, ndiyo maana wakati fulani walitokea waafrika wajinga wakawa wanapasua chupa na kuzifunga vizuri na kuingia mjini kisha kuwahadaa waafrika wenzao kwamba zile zilikuwa ni Almasi na kiukweli wajinga wale walijipatia sana fedha miaka hiyo.

Madini tumebaki kuyatazama huko YouTube na kwenye television.

Pamoja na Madini kuwa ni mali yetu sisi Waafrika lakini wanaonufaika nayo ni watu weupe.

Wao wanachimba (Sisi hatuwezi kuchimba kwasababu kuna wajaa laana huwa wanasema hatuna mitambo,sasa sijafahamu hiyo mitambo inauzwaga kiasi gani cha fedha ambacho hatuna uwezo wa kununua)

Wao wanayafanyia processes (Sisi hatuwezi kufanya processes kwakuwa wajaa laana huwa wanasema hatuna mitambo,Hiyo mitambo inauzwaje kama Taifa tushindwe?)

Wao wanasafirisha (Hapa wajaa laana huwa wanasema tukifanya sisi tutakosa masoko, watazira!)

Haya ndiyo tuyafanyayo ngozi nyeusi.

Kazi tunazoweza ni kusomesha watoto na wakimaliza waingie mitaani kuwa wachuuzi wa bidhaa(Machinga) au kuendesha Boda na Bajaji halafu tuwaminye ki kweli kweli walipe kodi wakati huo huo huku kwenye Madini ambayo tumepewa Neema na Mungu Kodi inayokatwa haiendani na kile tulichonacho na wakati mwingine hao wachimbaji wanakwambia "HATUJAPATA FAIDA, HIVYO HATUWEZI KULIPA KODI".

Kama Ndivyo!?

Kwanini nikisema AFRIKA INA NEEMA ILA WAAFRIKA WANA LAANA mnachukia na kufuta nyuzi zangu?

Hayo niliyoyaainisha ni machache sana miongoni mwa meeeeengi mnooooo ambayo ngozi nyeusi inayafanya,sasa sijui mnataka nitumie lugha gani!.

NIPINGENI KWA HOJA, KWANINI NISISEME NGOZI NYEUSI INA LAANA?

NAHITAJI KUELEWESHWA ILI NIWE NA MTAZAMO CHANYA KUHUSU NGOZI NYEUSI.
ufaransa umeme haukatiki 24hrs,wanatumia uranium waliochimba niger,nchi nzima ya niger ni 19% tu wananchi wake wana umeme,misri ni wakulima hodari na matajiri kwa kutegemea mto nile,unaoanzia east africa,kwenye njaa ya chakula..
 
Ubinafsi ni asili ya mwanadamu, hata Mimi nimesema huko juu. Tofauti yao na sisi, ni uzalendo na kujitambua kwa raia wao. Kiasi kwamba anayeingia madarakani, anakuwa anatanguliza maslahi ya nchi kwanza.
unafikiri wao ni wazalendo kiasi hicho unachofikiri?? ebu niambie umetumia kipimo gani au factor gani kusema wao wanauzalendo??

Ikiwa hivyo ndivyo je sisi tumefeli wapi kuiga kujifunza kutoka kwao maan vitu vingi tumetoa kwao
eg system za mahakama
education
tiba
uongozi n.k
 
unafikiri wao ni wazalendo kiasi hicho unachofikiri?? ebu niambie umetumia kipimo gani au factor gani kusema wao wanauzalendo??
Nmetumia observation pamoja na ulinganifu wa yale wanayosema dhidi wanayofanya. Uwazi wa asilimia kubwa wa mambo wafanyao na uwajibikaji. Lakini Pia maendeleo ya nchi zao

Ikiwa hivyo ndivyo je sisi tumefeli wapi kuiga kujifunza kutoka kwao maan vitu vingi tumetoa kwao
eg system za mahakama
education
tiba
uongozi n.k
Tanarudi kule kule, hatuna uzalendo hivyo hatuwezi kuwa na uwajibikaji au Uwazi kwenye mambo tufanyayo, na hayo yote yanatokana na ubinafsi wa kiwango Cha juu tulionao
 
Nmetumia observation pamoja na ulinganifu wa yale wanayosema dhidi wanayofanya. Uwazi wa asilimia kubwa wa mambo wafanyao na uwajibikaji. Lakini Pia maendeleo ya nchi zao

Tanarudi kule kule, hatuna uzalendo hivyo hatuwezi kuwa na uwajibikaji au Uwazi kwenye mambo tufanyayo, na hayo yote yanatokana na ubinafsi wa kiwango Cha juu tulionao
hahaaa ukiona umerudi kwenye circle yako ya jibu la kwanza tambua kuna kitu bado hujakijua
 
Nmetumia observation pamoja na ulinganifu wa yale wanayosema dhidi wanayofanya. Uwazi wa asilimia kubwa wa mambo wafanyao na uwajibikaji. Lakini Pia maendeleo ya nchi zao

Tanarudi kule kule, hatuna uzalendo hivyo hatuwezi kuwa na uwajibikaji au Uwazi kwenye mambo tufanyayo, na hayo yote yanatokana na ubinafsi wa kiwango Cha juu tulionao
Bro fanya fanya basi mpango tupate ile story ya mdogo wake mama mwenye nyumba....
 
Yawekana ukawa na mantiki kwenye content ya unachokiongelea, lakini napingana na wewe hapo kwenye kusema "Waafrika wana laana"

Nchi yoyote unayoiona imepiga hatua kwenye jambo lolote, basi siasa ina mchango mkubwa sana. Kinachotukwamisha Waafrika na Watanzania (to be specific) ni ubinafsi, sio elimu.

By nature, binadamz ni mbinafsi, lakini kiwango Cha ubinafsi kinapozidi Jamii lazima irudi nyuma maana kitakachofatia ni "Every man for himself". Mfumo wa elimu yetu inawezekana haupo vizuri, lakini ukirudi miaka mingi nyuma, mababu zetu hawakusoma, ila Kuna mambo waliweza kuyamudu maana hawakuwa wabinafsi. Kinachofanya niseme elimu sio tatizo kuu, angalia kwenye list ya viongozi wa sekta mbali mbali, wengi wao wamesoma nje ya nchi, tena katika mazingira Bora kabisa. Elimu ya hapa nnchini haijawaathiri, isipokuwa ubinafsi ndio unaziba utashi wao.

Kingine, Watanzania wengi tunajifanya hatupendi siasa, tunaamini kuwa inabidi tuwe busy na utafutaji hela na sio maswala ya siasa. Bila kujua hizo hela tunazoenda kutafuta, zinategemea siasa pia. Matokeo yake wafanya maamuzi watafanya hayo maamuzi bila kuangalia maslahi mapana ya nchi, mwisho wa siku impacts zinawarudia wale wanaosema wako busy na utafutaji hela, hawana muda na siasa.

Mimi nadhani, badala ya mfumo wetu wa elimu ungejikita kwanza kutoa elimu ya uraia na maswala ya uzalendo tangia tukiwa shule za msingi. Kwanini nasema hivi, sababu ni kwamba raia wengi wanajua maana ya neno uzalendo lakini hawawezi kuuishi uzalendo kwa vitendo. Mpaka sasa wapo wanaoamini uzalendo ni kuunga mkono serikali au chama tawala.

Kingine ambacho naweza kukukumbusha, mada yako imeongelea madini, Mimi nitazungumzia maliasili zote (madini yakiwepo). Hizi maliasili zimegawanyika ki Kanda. Kuna Kanda zina madini, zingine mbuga au vyanzo vya utalii. Na hata interest za watu zimejigawa hivyo hivyo kikanda, ndio maana leo ukienda Kanda ya ziwa au sehemu zenye madini, vijana/watu wa maeneo hayo wanapenda sana habari za madini, na hata utafutaji wao umejikita kwenye madini ( bila kujalisha elimu yao), na na unaweza ukakutana na Mzee ambae hana elimu yoyote, ila anauwezo wa kutrace vein na kuipata miamba iliyokuwa na madini, kitu ambacho wataalam wanakaa darasani miaka mingi kupata huo uwezo.

Au nenda Arusha, Kilimanjaro, Saadan,Ngorongoro uone jinsi wakati wa maeneo yale walivyo interested na utalii. Kuna wamasai hawajawahi kuingia darasani, ila wanaongea Kiingereza kilichonyooka kuzidi hata wasomi wengi. Nenda Mtwara uone vijana walivyo interested na kilimo Cha zao la korosho n.k

Kwa mantiki hiyo, serikali ikisema iingize mtaalam wa madini, wapenda kilimo na ufugaji hawatopendezwa sana, wapenda utalii hawatopendezwa sana. Badala yake nadhani elimu yetu ingejikita kwenye somo la kujitambua, uraia na maana halisi ya uzalendo na mzalendo mwenyewe. Kuhusu maliasili imeziongelea sana, tumeimbishwa hadi nyimbo kuhusu mbuga zetu, tumeshaambiwa sana tafsiri ya rangi za bendera zetu, lakini angalia tulipo.

Huwezi kumfundisha mtu uzalendo akiwa chuo au sekondari. Shule ya msingi ni msingi wa kila jambo. Somo la uzalendo lianzie kule.

Waafrika hatujalaaniwa mkuu
Ubinafsi wakujimaliza mwenyewe na kizazi chako utahira AKA laana iliyotukuka
 
Back
Top Bottom