Pole na hongera.Ingawa siyo daktari,I'lla kwa uzoefu wangu unapokuwa na nyuzi,ni kujitahidi sana,kutogusa maji eneo la mshono,kuzingatia ratiba ya kusafisha kidonda,kuepuka vyakula vya mafuta,kuepuka kukaa sehemu zenye joto,kutobeba vitu vizito,mazoezi mepesi nk
Pole Ma. Mie nilijifungua kwa CS na kutembea kulinisaidia sana. Na pia kuepuka maji sehemu husika.
Ila kwa down zea sijui kama its the same.
Ngoja nikuitie watu8, gfsonwin, Lady doctor.
pole mamaa, mkewangu aliwah kupata tatizo kama hilo nikampeleka hosp, akiwa anasubiri kuingia chumba cha upasuaji, akaanza kujadili na akina mama wenzake wakamwambia yaani ni tatizo ni hilo tu? akajibu ndio, makamwambia sio tatizo hatakidogo, hukuwakimpa mifano ya enzi kulipokuwa hakuna hosp, ukweli tuliondoka na mwisho alipona, ila nilicho jifunza kama unamshono au CS usikubali kukandwa na maji ya moto kwa kidonda huiva nakuchelewa kupona.
nadhani sasa utakuwa unamheshimu mama yako. teh, just a joke. Lila mwanamke anayeshonwa huwa anapewa maelekezo ya kuepuka maji ya moto kwenye kidonda. kwa uzoefu wangu kama mama aliyechanika msamba name kushonwa baada ya mwezi kitu kinakuwa intact. sasa kama kuna bacterial infection na panatoa usaha inabidi umuone daktari, lakini kama ni pakavu usihofu patapona turn. Mungu awabariki wanawake wote waliotayari kuzaa.
.
Dada, kwa kuzingatia kuwa ulijifungu tarehe 12 January na lalamiko umelitoa 6 February, yaani wiki nne zimepita bado mpasuko ulioshonwa haujapona. Nakushauri urudi hospitali ukafanyiwe uchunguzi makini kwa nini mshono hauponi (watacheck kama kuna infection, una kisukari au compromised medical condition nyingine). Please, zingatia!!!
Ahsante sana mama mdogo nitafanya hilo haraka iwezekanavyo japo sina muwasho wala usaha but ni vema nikawa assured kwa issue kama hiyo..ahsante tena na tena