Nahitaji kupona mshono haraka

Nahitaji kupona mshono haraka

rosita

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2013
Posts
509
Reaction score
469
Habari zenu wapendwa

Namshukuru Mungu nimejifungua mtoto wa kike tarehe 12/1 lakini nilipasuka msamba namaanisha alinichana sababu alizaliwa na kilo tatu na nusu na ni mara yangu ya kwanza kujifungua.

Hivyo basi nilishonwa na zile nyuzi zisizotolewa but mpaka leo sijapona na nazingatia maelekezo yote niliyopewa ikiwemo usafi.

Naomba mwenye ufahamu juu ya hili anishauri nifanyeje sababu nakosa amani.
 
Dah mama pole sana, subiri soon utapata ushauri mzuri
 
Pole sana pia Hongera kwa kupata mtoto vuta subira wataalamu watakuja kukwambia vizuri cha kufanya ili urudi kwenye hali yako ya kawaida.
 
Pole sana pia Hongera kwa kupata mtoto.
Vuta subira wataalam watakuja kukwambia vzr cha kufanya ili urudi kwenye hali yako ya kawaida.

Ahsante sana
 
Pole na hongera ingawa siyo daktari, ila kwa uzoefu wangu unapokuwa na nyuzi,ni kujitahidi sana,kutogusa maji eneo la mshono,kuzingatia ratiba ya kusafisha kidonda,kuepuka vyakula vya mafuta,kuepuka kukaa sehemu zenye joto,kutobeba vitu vizito,mazoezi mepesi nk
 
Pole Mie nilijifungua kwa CS na kutembea kulinisaidia sana na pia kuepuka maji sehemu husika.

Ila kwa down zea sijui kama its the same.

Ngoja nikuitie watu8, gfsonwin, Lady doctor.
 
Last edited by a moderator:
Well said mayenga,ila mama zetu jamani cha moto wanakipata,lakini yote ni kwa mapenzi ya Mungu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Pole na hongera.Ingawa siyo daktari,I'lla kwa uzoefu wangu unapokuwa na nyuzi,ni kujitahidi sana,kutogusa maji eneo la mshono,kuzingatia ratiba ya kusafisha kidonda,kuepuka vyakula vya mafuta,kuepuka kukaa sehemu zenye joto,kutobeba vitu vizito,mazoezi mepesi nk

Thanx mkuu I got some points..barikiwa!
 
Well said mayenga,ila mama zetu jamani cha moto wanakipata,lakini yote ni kwa mapenzi ya Mungu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Umeona hee,..inabidi tuzidi kuwaheshimu wazazi na wanawake wote kwa ujumla.
 
Last edited by a moderator:
pole mamaa, mkewangu aliwahi kupata tatizo kama hilo nikampeleka hospitali, akiwa anasubiri kuingia chumba cha upasuaji, akaanza kujadili na akina mama wenzake wakamwambia yaani ni tatizo ni hilo tu?

Akajibu ndio, makamwambia sio tatizo hatakidogo, hukuwakimpa mifano ya enzi kulipokuwa hakuna hosp, ukweli tuliondoka na mwisho alipona, ila nilicho jifunza kama unamshono au CS usikubali kukandwa na maji ya moto kwa kidonda huiva nakuchelewa kupona.
 
Nadhani sasa utakuwa unamheshimu mama yako teh, just a joke. ila mwanamke anayeshonwa huwa anapewa maelekezo ya kuepuka maji ya moto kwenye kidonda kwa uzoefu wangu kama mama aliyechanika msamba name kushonwa baada ya mwezi kitu kinakuwa intact.

Sasa kama kuna bacterial infection na panatoa usaha inabidi umuone daktari, lakini kama ni pakavu usihofu patapona turn Mungu awabariki wanawake wote waliotayari kuzaa.
 
Dada, kwa kuzingatia kuwa ulijifungu tarehe 12 January na lalamiko umelitoa 6 February, yaani wiki nne zimepita bado mpasuko ulioshonwa haujapona. Nakushauri urudi hospitali ukafanyiwe uchunguzi makini kwa nini mshono hauponi (watacheck kama kuna infection, una kisukari au compromised medical condition nyingine). Please, zingatia!!!
 
pole mamaa, mkewangu aliwah kupata tatizo kama hilo nikampeleka hosp, akiwa anasubiri kuingia chumba cha upasuaji, akaanza kujadili na akina mama wenzake wakamwambia yaani ni tatizo ni hilo tu? akajibu ndio, makamwambia sio tatizo hatakidogo, hukuwakimpa mifano ya enzi kulipokuwa hakuna hosp, ukweli tuliondoka na mwisho alipona, ila nilicho jifunza kama unamshono au CS usikubali kukandwa na maji ya moto kwa kidonda huiva nakuchelewa kupona.

Ndugu nilikandwa na yale maji ya kunyonyolea kuku manyoya aliyenikanda alijitahidi yasipite kwenye mshono coz alinikanda sehemu nyingine kama tumbo na mgongo kwa one week nahisi it can be one of da factor coz yalikuwa yakipita bahati mbaya
Ahsante kwa kunitia moyo mkuu barikiwa!
 
nadhani sasa utakuwa unamheshimu mama yako. teh, just a joke. Lila mwanamke anayeshonwa huwa anapewa maelekezo ya kuepuka maji ya moto kwenye kidonda. kwa uzoefu wangu kama mama aliyechanika msamba name kushonwa baada ya mwezi kitu kinakuwa intact. sasa kama kuna bacterial infection na panatoa usaha inabidi umuone daktari, lakini kama ni pakavu usihofu patapona turn. Mungu awabariki wanawake wote waliotayari kuzaa.


.

Ahsante mkuu hakuna faraja kama kumwona mwanao uliyembeba kwa miezi tisa haijalishi how much imekucost kumpata but ukimuona tu unasikia raha sana japo naugulia mshono but nikimwona my baby gal maumivu yote kwishney..
 
Dada, kwa kuzingatia kuwa ulijifungu tarehe 12 January na lalamiko umelitoa 6 February, yaani wiki nne zimepita bado mpasuko ulioshonwa haujapona. Nakushauri urudi hospitali ukafanyiwe uchunguzi makini kwa nini mshono hauponi (watacheck kama kuna infection, una kisukari au compromised medical condition nyingine). Please, zingatia!!!

Ahsante sana mama mdogo nitafanya hilo haraka iwezekanavyo japo sina muwasho wala usaha but ni vema nikawa assured kwa issue kama hiyo..ahsante tena na tena
 
Ahsante sana mama mdogo nitafanya hilo haraka iwezekanavyo japo sina muwasho wala usaha but ni vema nikawa assured kwa issue kama hiyo..ahsante tena na tena

Asante sana. Cha muhimu kuzingatia ni kuwa baada ya kujifungua mwanamke anahitaji kufanyiwa check up baada ya wiki moja, nne na wiki sita ili kujua kama anaendelea vizuri au hapana. Je wewe ulihudhuria hizo check tatu?
 
Back
Top Bottom