Nahitaji kuwekeza Tsh. Milioni 170

Ni kweli hizo investment zipo sijasema ni mpya ila nimeshangaa miaka hii watu wengi wanashauriwa ku invest huko badala ya kutazama fursa zingine za kibiashara, biashara sio lazima kuwa mchuuzi, kwa miaka ya zamani hizo bonds na mutual funds walikuwa wana invest wafanyabiashara baada ya kupata faida au watumishi wa serikali baada ya ku retire , ni vizuri vijana wakiwekeza huko baada ya kupata faida kubwa kwenye biashara zao na sio kuwekeza mitaji kwa kuogopa kupoteza . ku export sio lazima ulaya ata burundi una export na pia sio lazima ku export vyakula ndo maana nikasema upande huo ukitazamwa vizuri basi kama kuna changamoto ni rahisi kutatuliwa
 
Bond ya miaka 100! Wazungu wapo mbali kweli.

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
Za jioni wadau,

Naomba mchango wa mawazo yenu, nikiwa na milioni 170 za kitanzania naweza wekeza wapi pesa hii nikapata rejesho lenye tija?

Kwangu mimi rejesho lenye tija ni angalau milioni 2 kwa mwezi.

Natanguliza shukrani.
Una uwezo kupata ml 170 na hauna uwezo wa kuziwekeza? Au umepewa urithi hukuzitafuta, au umeuza nyumba au umefanya nini aisee. manake ukiona una akili ya kupata pesa kama hiyo kwa jasho lako, haungehitaji kuuliza wapi ukawekeze, akili yako na uzoefu wako ungekuelekeza tuw api uende.
 
Kama hauna exposure na masuala ya biashara, Government bonds or real estates as other members mentioned above.

Manageable risks.

Investing fresh millions on something like sijui makuku, mbuzi, exports etc you need buch of know-how and time plus it’s risky.
 
Mkuu nina ka milioni 3,nikitaka kuwekeza mfuko wa bond UTT AMIS rate yake ni sh ngap inakua mkuu?
 
Kirahisi ivyo nyumba uuze ndani ya miez 4
 
Watu wamenunua mahindi wanafikisha mipakani inatoka kauli ya waziri hakuna kuuza mahindi nje.


Hiyo risk unaionaje ?


Watu wanawekeza kwenye mutual funds kutokana na security
 
Kirahisi ivyo nyumba uuze ndani ya miez 4

Hakuna biashara rahisi kaka
Lakini nazungumza vitu nnavyovifahamu na ambavyo niko na experience navyo,
Kunawatu wanakaa na nyumba mpaka miezi sita hajauza,
Na kunawatu ndani ya wiki mbili mpaka tatu wanauza,
Kunamambo ya msingi ya kuzingatia ili nyumba ikiisha tuu isikae,
Kama ushawahi kusikia kunamaeneo ukiwa unajenga frem pengine hata kupaua bado kunawatu tayari washalipia utanielewa nnachosema,
Na kunamaeneo mengne wewe ni shahidi unapita unakuta frem nyng hazjafunguliwa muda mrefu,
Yaani hazina watu,
Yote kwa yote hakuna biashara rahisi lakini zipo biashara zisizokuwa na stress
 
Wewe utafaidikaje na hiyo 170m?

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Watu wamenunua mahindi wanafikisha mipakani inatoka kauli ya waziri hakuna kuuza mahindi nje.


Hiyo risk unaionaje ?


Watu wanawekeza kwenye mutual funds kutokana na security
fursa zipo bhana sema sisi wabongo tunapenda kuigana biashara, wengi hawezi kutafuta fursa mpya wanavizia mtu akifanya akifanikiwa ndo waige, wewe huoni wakenya wengi hawakauki bongo kutafuta fursa mpya hata wainigeria sasa wanajaa bongo, kwanini vitu vingi vya Tanzania vikafanyiwe export kenya? . na pia asilimia kubwa tunapenda kudanganywa na tamaa za kupata faida kubwa ndani ya muda mfupi zinatuponza tunachoma mitaji yetu, kuna jamaa alikuwa mfanyabiashara watu wakamseti congo ukiwa na mtaji mzuri madini ni bei rahisi sana hasa huko ndani ndani basi akapangwa akapangika bila kufanya research yake mwenyewe na kwasababu alishajawa na tamaa jinsi alivyoelezwa faida atayopata ni mara nne ya mtaji wake basi huyo akaenda congo kweli akafanikiwa kukusanya mzigo wa dola laki tano sasa wakati anajiandaa kuanza kuuvusha kidogo kidogo alikamatwa kwasababu hakuwa na vibali vya kununua madini sio kama hamna watu wasio kuwa na vibali wapo ila yeye alikuwa anaingizwa king na wale waliompa mchongo nae akazama mzima mzima.
 
Toa ujinga wako hapa unasema wabongo eti hawajui kutafuta fursa. Umeitembea hii nchi uone wabongo wanavyochakarika! Kutafuta fursa ni Hadi kutoka nje ya nchi kwani. Nchi yetu Ina Kila kitu kwani ni vibaya mtu kukomaa na nchi yake.

Kipindi cha mwendazake kabla hajachafua soko la korosho ungeenda mtwara ukaona wabongo wanavyosambaza mabilioni kwenye korosho!

Usiongee vitu usivuojua.

Mutual funds ni uwekezaji sio biashara. Sio Kila binadamu anaiweza biashara. Sio Kila mtu anaweza compliance za TRA na regulatory bodies zingine za biashara kwanini asiweke Hela yake BOT au UTT AMIS. Kwani ni dhambi.


Huyo alieenda Kongo na Dola Laki 5 ni sawa na Bilion Moja. Hiyo Hela angepelea BOT akanunua BONDS za miaka 25 angekuwa anavuta milion 10+ Kila mwezi.


Na angeweza kutumia BOND certificate kama collateral kuchukulia mkopo bank hadi nusu kwa alichowekeza BOT. Maana yake bank wangeweza kumpa Hadi mkopo wa milion 500.

Hiyo milion 500 ya mkopo angeweza kuwekeza kujenga nyumba kadhaa Dar akapangisha. Kodi ya hizo nyumba ndio zingelipia mkopo. Na kama Kodi ingekuwa ndogo kwenye kulipa mkopo wa bank angetumia sehemu ya ile milion 10 ya riva ya BOT kusaidia kumalizia mkopo.

Mkopo ukiisha. Anakopa Tena bank Kwa kutumia collateral ya hizo nyumba kujengea hizo nyumba. Kumbuka ile Hela ya BOT milion 10 Iko pale pale.


Matajiri wote duniani hutumia Hela za masikini zihazokaa bank kufanyia projects zao. Wewe masikini unapeleka Hela bank MO DEWIJ anaenda kukopa ajengee ma-apartments.


Sio Kila mtu anaweza kuexport au kufanya biashara. Kila mtu afanye jambo Kwa personality yake. Biashara inahitaji roho ngumu , kujikana na kuwa tayari kwa lolote.

Ukiona huna hizo characters tafuta investment basi. Usione wanaoenda kuwekeza hawajielewi.
 
..mkuu umeongea sahihi sana na kwa weledi sana.
 
Kaka sio simple kihivyo Ku shinda bid ya bond au treasury bill sio rahisi-unaweza ukawa na fedha zako na usipate hiyo nafasi ya kuzinunua.
Zina ushindani sana,kila MTU anataka kula kwa mrija.
 
Kaka mbona unajichanganya,kwani ukienda kununua hizo bond unatofauti gani na kuweka hela bank,vyote ni vilevile tu-ni kuweka hela wenye biashara zao wanakwenda kuzikopa.
Huwezi ukawa na Nchi ambayo watu wanaogopa kufanya biashara,bila biashara hamna shughuli za kiuchumi zitakazofanyika katika Nchi-ndio maana ukiwekeza huko kwenye financial markets returns zake ni kidogo zaidi.

Haijalishi mazingira ya kibiashara ni magumu kiasi gani,ni vizuri watu kuendelea kutafuta fursa na kuwekeza zaidi.

Kwa MTU asiyekuwa na fedha nyingi na ni kijana,ni hasara kuwekeza kwa kununua treasury bills na bonds.
 
Za jioni wadau,

Naomba mchango wa mawazo yenu, nikiwa na milioni 170 za kitanzania naweza wekeza wapi pesa hii nikapata rejesho lenye tija?

Kwangu mimi rejesho lenye tija ni angalau milioni 2 kwa mwezi.

Natanguliza shukrani.
Mi nina mtaji wa mil20 napata mil3 kwa mwezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…