fursa zipo bhana sema sisi wabongo tunapenda kuigana biashara, wengi hawezi kutafuta fursa mpya wanavizia mtu akifanya akifanikiwa ndo waige, wewe huoni wakenya wengi hawakauki bongo kutafuta fursa mpya hata wainigeria sasa wanajaa bongo, kwanini vitu vingi vya Tanzania vikafanyiwe export kenya? . na pia asilimia kubwa tunapenda kudanganywa na tamaa za kupata faida kubwa ndani ya muda mfupi zinatuponza tunachoma mitaji yetu, kuna jamaa alikuwa mfanyabiashara watu wakamseti congo ukiwa na mtaji mzuri madini ni bei rahisi sana hasa huko ndani ndani basi akapangwa akapangika bila kufanya research yake mwenyewe na kwasababu alishajawa na tamaa jinsi alivyoelezwa faida atayopata ni mara nne ya mtaji wake basi huyo akaenda congo kweli akafanikiwa kukusanya mzigo wa dola laki tano sasa wakati anajiandaa kuanza kuuvusha kidogo kidogo alikamatwa kwasababu hakuwa na vibali vya kununua madini sio kama hamna watu wasio kuwa na vibali wapo ila yeye alikuwa anaingizwa king na wale waliompa mchongo nae akazama mzima mzima.
Toa ujinga wako hapa unasema wabongo eti hawajui kutafuta fursa. Umeitembea hii nchi uone wabongo wanavyochakarika! Kutafuta fursa ni Hadi kutoka nje ya nchi kwani. Nchi yetu Ina Kila kitu kwani ni vibaya mtu kukomaa na nchi yake.
Kipindi cha mwendazake kabla hajachafua soko la korosho ungeenda mtwara ukaona wabongo wanavyosambaza mabilioni kwenye korosho!
Usiongee vitu usivuojua.
Mutual funds ni uwekezaji sio biashara. Sio Kila binadamu anaiweza biashara. Sio Kila mtu anaweza compliance za TRA na regulatory bodies zingine za biashara kwanini asiweke Hela yake BOT au UTT AMIS. Kwani ni dhambi.
Huyo alieenda Kongo na Dola Laki 5 ni sawa na Bilion Moja. Hiyo Hela angepelea BOT akanunua BONDS za miaka 25 angekuwa anavuta milion 10+ Kila mwezi.
Na angeweza kutumia BOND certificate kama collateral kuchukulia mkopo bank hadi nusu kwa alichowekeza BOT. Maana yake bank wangeweza kumpa Hadi mkopo wa milion 500.
Hiyo milion 500 ya mkopo angeweza kuwekeza kujenga nyumba kadhaa Dar akapangisha. Kodi ya hizo nyumba ndio zingelipia mkopo. Na kama Kodi ingekuwa ndogo kwenye kulipa mkopo wa bank angetumia sehemu ya ile milion 10 ya riva ya BOT kusaidia kumalizia mkopo.
Mkopo ukiisha. Anakopa Tena bank Kwa kutumia collateral ya hizo nyumba kujengea hizo nyumba. Kumbuka ile Hela ya BOT milion 10 Iko pale pale.
Matajiri wote duniani hutumia Hela za masikini zihazokaa bank kufanyia projects zao. Wewe masikini unapeleka Hela bank MO DEWIJ anaenda kukopa ajengee ma-apartments.
Sio Kila mtu anaweza kuexport au kufanya biashara. Kila mtu afanye jambo Kwa personality yake. Biashara inahitaji roho ngumu , kujikana na kuwa tayari kwa lolote.
Ukiona huna hizo characters tafuta investment basi. Usione wanaoenda kuwekeza hawajielewi.