Nahitaji kwenda kuanzisha kilimo mkoa wa Katavi

Nahitaji kwenda kuanzisha kilimo mkoa wa Katavi

Jifunafu

Senior Member
Joined
May 25, 2020
Posts
182
Reaction score
693
Ndugu wanajamvi,

Ni siku nyingine ndugu zangu tumeamka salama na pilika za kusaka mkate wa Leo.
Husika na madam hapo juu, ndugu zangu nimeamua kuja kwenu kupata mawazo ya namna ninavyoitaji kuingiza katika kilimo hususani kilimo Cha mahindi na maharage.

Katika kuangalia mikoa nilivutiwa Sana na mkoa wa KATAVI kwani niliwai kufika Kule ingawa sikutembea Sana lakini nilivutiwa na Hali ya hewa na pia mapori makubwa na mashamba na ikionyesha wazi Kuna furusa nzuri za kilimo.

Japo nilipitia wilaya ya uvinza Kuna njia Barabara inapita porini Hadi mpanda nikaenda Hadi sehemu moja panaitwa kalemie inapojengwa bandari,nilivutiwa Sana na maeneo makubwa na aridhi yenye rutuba nzuri.Kimsingi ninahitaji kuingiza katika kilimo maana nikiangalia Hali ya Sasa hakuna namna ni kukaza mkanda tu,Bora niteseke kuliko kuendelea kukumbatia jiji wakati maisha yanazidi kuwa magumu Kila kukicha na ramani zenyewe hazipatikani.

Kuna jamaa yangu yupo KATAVI niliongea nae akaniambia mashamba yanapatkana Sana na mara nyingine wenyeji wanamaeneo makubwa anaweza kukupatia kulima Kwa ajiri ya kusafisha eneo.Kikubwa nalenga kilimo Cha Maharage na mahindi.

Ndugu zangu mlioko KATAVI naombeni mnipe ABC kuhusu maeneo gani yanafaa Kwa kilimo hiki na unafuu wa upatikanaji wa aridhi ya kukodi Kwa bei nafuu.

Michango yenu ni mhimu ndugu zangu katika safari ninayotaka kuianza.

ASANTENI.
 
Watakuja washauri wa kwenye vitabu watakuvunja moyo lakini wazo lako ni zuri. Kaza mkanda.
 
Uzi km huu Mara nying hunifanya nkose usingz! Mim kwa mda wote nawaza kilimo! Nmeamua kuwekeza songea ndiko nmenunua heka Mia moja y shamba pori nitalima mpunga, mahind, maharage, soya, alzet nk. Kwa upande wangu nmeamua nianzie porn ndio niende mjin! Bei za ardh ni ndogo Sana ni wastan wa 40000 hd 50000 kwa heka! Kwa heka unavuna 25 hd 30 z mahnd japo unatumia mbolea! Na mi napenda nckie ni mkoa gan hawatumii mbolea na Bei y ardh ni ndogo nizd kuongeza mashamba
 
Kwa hiyo mkuu bila mbolea haulimi huko
 
Mkuu naitaji unipe ABC na Mimi naitaji kuzama huko.
 
Mkuu naitaji unipe ABC na Mimi naitaji kuzama huko.
Mkuu tutafutane tuyajenge,na Mimi silali kabisa,akili yangu inawaza shambani tu maana naona labda nawezakuchomokea huko. Tuyajenge mkuu.
 
Mkuu tutafutane tuyajenge,na Mimi silali kabisa,akili yangu inawaza shambani tu maana naona labda nawezakuchomokea huko. Tuyajenge mkuu.
Mungu akuongoze...kama hujapata info humu jitahidi uende mahali husika..wenyeji watakupa ramani ila jitahidi hasa kujua kuhusu changamoto ili uweze kuzi overcome mapema.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mungu akuongoze...kama hujapata info humu jitahidi uende mahali husika..wenyeji watakupa ramani ila jitahidi hasa kujua kuhusu changamoto ili uweze kuzi overcome mapema.

#MaendeleoHayanaChama
Asante jiweangavu
 
Mkuu vp ulifanikiwa?
Mkuu bado sijapata wadau kutoka katavi wa kunipa mrejesho kuhusu kilimo huko,naona bado wanamalizia mavuno.Wadau waliopo katavi njooni mtupe mrejesho wa KILIMO huko na maeneo ya kilimo.
 
Mkuu bado sijapata wadau kutoka katavi wa kunipa mrejesho kuhusu kilimo huko,naona bado wanamalizia mavuno.Wadau waliopo katavi njooni mtupe mrejesho wa KILIMO huko na maeneo ya kilimo.
Kwa katavi fanya tuwasiliane nijaribu kukuunganisha na jamaa zangu wapo katavi mimi nipo Rukwa
 
Mkuu vp nipe connection
Mwaka juzi nilizungukia sana maeneo ya Majimoto ukivuka ukaambaa na mlima kama unaelekea Sumbawanga kupitia Muze

Sana nilikua vijiji vya Mkamba, Mpaka Mtowisa, vijiji viko pembezoni mwa ziwa Rukwa

Kuna jamaa ni mtendanji wa kijiji akapropose msimu wa biashara ya mahindi ukiisha na wakulima wanapoanza kulima tunawakopesha, hua wanakopesha kwa kila 15k unapata gunia 1 la mahindi wanapovuna .. Au alizeti

Msimu ulipoisha nikaondoka jumla maana niliona kuna kesi kesi nyingi za migogoro ya kudaina na kutolipwa kwa waliokopana hapo kijijini

Lakini ukanda huo wanalima sana mahindi na alizeti pia

Pia kua stori za ulozi lozi sana pande hizo, wenyeji ni wafipa lakini wamezidiwa na wahamiaji wa kisukuma
 
Back
Top Bottom