Jifunafu
Senior Member
- May 25, 2020
- 182
- 693
Ndugu wanajamvi,
Ni siku nyingine ndugu zangu tumeamka salama na pilika za kusaka mkate wa Leo.
Husika na madam hapo juu, ndugu zangu nimeamua kuja kwenu kupata mawazo ya namna ninavyoitaji kuingiza katika kilimo hususani kilimo Cha mahindi na maharage.
Katika kuangalia mikoa nilivutiwa Sana na mkoa wa KATAVI kwani niliwai kufika Kule ingawa sikutembea Sana lakini nilivutiwa na Hali ya hewa na pia mapori makubwa na mashamba na ikionyesha wazi Kuna furusa nzuri za kilimo.
Japo nilipitia wilaya ya uvinza Kuna njia Barabara inapita porini Hadi mpanda nikaenda Hadi sehemu moja panaitwa kalemie inapojengwa bandari,nilivutiwa Sana na maeneo makubwa na aridhi yenye rutuba nzuri.Kimsingi ninahitaji kuingiza katika kilimo maana nikiangalia Hali ya Sasa hakuna namna ni kukaza mkanda tu,Bora niteseke kuliko kuendelea kukumbatia jiji wakati maisha yanazidi kuwa magumu Kila kukicha na ramani zenyewe hazipatikani.
Kuna jamaa yangu yupo KATAVI niliongea nae akaniambia mashamba yanapatkana Sana na mara nyingine wenyeji wanamaeneo makubwa anaweza kukupatia kulima Kwa ajiri ya kusafisha eneo.Kikubwa nalenga kilimo Cha Maharage na mahindi.
Ndugu zangu mlioko KATAVI naombeni mnipe ABC kuhusu maeneo gani yanafaa Kwa kilimo hiki na unafuu wa upatikanaji wa aridhi ya kukodi Kwa bei nafuu.
Michango yenu ni mhimu ndugu zangu katika safari ninayotaka kuianza.
ASANTENI.