Nahitaji mbegu nzuri ya mihogo

Nahitaji mbegu nzuri ya mihogo

Mama queen

New Member
Joined
Aug 13, 2013
Posts
4
Reaction score
1
Habari wadau,nina shamba maeneo ya Mapinga karibu na Bagamoyo lenye ukubwa wa ekari mbili,natarajia msimu huu wa kilimo kupanda mihogo,hivyo basi ninaomba mnisaidie ni mahali gani ninaweza kupata mbegu nzuri ya mihogo,au hata kama kunamdau yeyote anaweza kunisaidia kwa ushauri,asanteni na Karibuni.my no 0752729002
 
Kama una nafasi nenda Kibaha pale regional block, uliza idara ya kilimo, watakutajia mbegu bora sawa na eneo lako. Mimi nitakwambia Kiroba ni nzuri kumbe sio compatible na udongo wako, au nitakwambia mbuyu ni bomba kumbe sio ya udongo wako, au nitakutajia Kibanga meno,ikawa sio mwafaka kwako.

Mhogo sasa hivi mali, usifanye kwa majaribio, maanisha kabisa kwa kutaka ushauri wa Bwana kilimo Bagamoyo.
 
Malila kashamaliza manake huyu kawekwa humu na Mungu kwa ushauri thabiti...
 
Kumbe mihogo ina species nyingi hivyo? asante mdau hayo majina ndio nimesikia leo
Kama una nafasi nenda Kibaha pale regional block, uliza idara ya kilimo, watakutajia mbegu bora sawa na eneo lako. Mimi nitakwambia Kiroba ni nzuri kumbe sio compatible na udongo wako, au nitakwambia mbuyu ni bomba kumbe sio ya udongo wako, au nitakutajia Kibanga meno,ikawa sio mwafaka kwako.

Mhogo sasa hivi mali, usifanye kwa majaribio, maanisha kabisa kwa kutaka ushauri wa Bwana kilimo Bagamoyo.
 
Hakikisha unapata mbegu bora kutoka kwenye vituo vya kilimo.

Kuna ugonjwa wa batobato nasikia huo noma
 
Back
Top Bottom