Nahitaji mkopo wa laki 1

Uza smart phone uliyonayo, Toa 100, 000/- Then Hela Itakayo Bakia Nunua Nokia Ya Tochi.
 
Fanyia kazi ushaur huu
 


Mkuu FUSO , heshima kwako ndugu.
Kwa mtu (kijana) mwenye mtaji wa Tsh laki 8 kamili, waweza mshauri afanye biashara gani kwa kipindi hiki? Preferably iwe biashara ya kukimbiza... yani ananunua na kwenda kuuza na kugeuka tena fasta. Ni kijana mpambanaji, yupo tayari kuingia mkoa wowote penye fursa ya biashara.
Ahsante.
 


Hivi hiyo biashara ya kuuza maji, kwa Dar bado inatoka kwa maeneo yepi? Nataka nikomae nayo.

Nimeulizia maeneo ya Ubungo mpaka Kimara, wanasema saahivi hiyo fursa is no more. Dawasco weshatandaza bomba za kutosha.

-Kaveli-
 
Hivi hiyo biashara ya kuuza maji, kwa Dar bado inatoka kwa maeneo yepi? Nataka nikomae nayo.

Nimeulizia maeneo ya Ubungo mpaka Kimara, wanasema saahivi hiyo fursa is no more. Dawasco weshatandaza bomba za kutosha.

-Kaveli-
Nenda kigamboni watu wengi hakuna hata bomba moja la dawasco; nguvu yako tu kusukuma mkokoteni
 
Nenda kigamboni watu wengi hakuna hata bomba moja la dawasco; nguvu yako tu kusukuma mkokoteni


Information is Power. Noted with a bunch of thanks.

-Kaveli-
 
Mkuu dojonase , habari za Kigamboni.
Hebu naomba unipe baseline info kuhusu biashara ya maji huko Kigamboni. Hali ikoje huko upatikanaji wa maji? biashara ya kuuza maji inatoka?

-Kaveli-
Ur not serious.
 
Kwanini unahisi I am not serious ?

-Kaveli-
nimeshakupa hints kwamba biashara kule inalipa sababu hakuna bomba hata moja la dawasco kule; unaweza kupata hadi 50,000 kwa siku kwa kuuza hayo madumu kama una bidii - sasa wewe unataka details zipi zaidi ya hizi - kwa nini usiende na kufanya survey mwenyewe. maana sasa utanipa kazi tena ya kukupigia hesabu zaidi kwamba kukodi mkokoteni bei gani? je madumu nitapata wapi? je wateja wa kuanzia nitawapataje? je nikitumia punda wa kukodi kuvuta mkokoteni wanapatikana wapi? je kutumia punda au mimi mwenyewe kuvuta mkokoteni njia ipi ina faida kubwa nk

Yaani ni hivi ukiona mtu ni tajiri ujue kasota; kama si yeye basi baba yake.

sasa Nenda pale Tungi - utaona vijana na mikokoteni kibao toka saa 10 alfajiri hadi saa 2 usiku wanatafuta pesa!!
 


Kuulizia/kupata taarifa from secondary source siyo kosa wala dhambi.

Ofkoz ni lazima nikafanye survey mimi mwenyewe kwanza ili kuona hali halisi on the ground.

Nashukuru Mkuu for such useful hints, umesomeka vyema kabisa. Soonest naenda kulifanyia kazi.

-Kaveli-
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…